Je, ni kweli kuna Waziri anaugua Corona inafanywa Siri? Tunaficha nini? Hala hala kisa cha mficha maradhi! Truth & Transparency the only way out!

Huko instagram wameshamtaja jina na picha yake wameiweka.
Asante pascal kwa kuwafungulia njia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kumbe ndio ndege zinaondoka kimya kimya.
 

yule mkuu mwenye mamlaka ya kutoa taarifa za wagonjwa bila kibali cha hao wanne ilowaorodhesha hajapata hizo taarifa ili azitoe kinyume na utaratibu wa sheria?
 

CCM inahusika sana kwa kuwaweka vibaraka hao wasojua nini wanafanya ,uchu wao na chuki zao ndio zinatufikisha hapa kwenye janga, Mungu atuepushe.Aamin
 
Nasema ivi, Mgonjwa wa korona atajwe tu! hamna kuficha jina wala wizara yake. China kuna app kabisa inakuonesha nani ana corona na umbali uliopo baina yako na mwenye corona.

Huu sio ugonjwa wa mtu kufichwa jina asijulikane. Akijulikana jina na wizara, basi waliokuwa wanafanya nae kazi pamoja na familia zao zitaweza kuchukua tahadhari mapema kabla hakijanuka.
 

Mkuu wanatuchombeza na uchaguzi mkuu. Hawa ni wakutaarifu wazi.

Wako busy kutuaminisha kuwa huu ugonjwa si kitu. Wamezuia taarifa kuhusiana na huu ugonjwa kuwekwa hadharani.

Kwa nini mashule na vyuo vimefungwa kama kila kitu ni sawa?

Hizi habari za uchaguzi mkuu, au jiwe yuko kwenye kijiwe cha kahawa na tangawizi zote ni geresha tu.

Wanapaswa kujua wanaongoza hii nchi kwa dhamana yetu. Kutuficha mambo nyeti yenye kuhusiana na uhai wetu ni kupoka haki yetu ya msingi sana ambayo 'by any standard' ni kinyume sana cha Katiba ya nchi hii.
 
Mgonjwa mkaidi, ajitibu mwenyewe!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pascal Mayalla,
Sijui ni kwa nini umeshindwa kuweka jina la huyu waziri wakati jina lake, wadhifa wake na picha yake vyote vimeshasambaa mitandaoni.
Kumbuka mada yake kaileta kama na yeye anaukiza hivyo hata wakimkamata anaweza jitetea kuwa na yeye hajui kauliza sasa kazi kwenu mnao coment yeye kakaa pembeni anawachora tuu hapo kesi hana
 
Soma gazeti ilo


Salama Aboud Talib (Waziri wa Nishati - SMZ) ashukiwa kuugua CORONA

Waziri wa Nishati wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) ambae alikuwa safarini kutokea London (Uingereza [emoji636]) na kupitia Italy [emoji634] kisha kurejea Zanzibar wiki tatu zilizopita, amelazwa katika hospitali ya Mnazi Mmoja akiwa katika hali mbaya huku akishukiwa kuwa ana maambukizi ya virusi vya CORONA..

Dr. Mkuu wa Hospitali ya Mnazi Mmoja baada ya kumpima vipimo vya awali na kutokana na dalili alizonazo mgonjwa huyo, aliamuru mgonjwa huyo kupelekwa katika eneo maalum la uangilizi kwa ajili ya wagonjwa wote wenye virusi vya corona, lakini Waziri huyo aligoma kuondoka katika Hospitali ya Mnazi mmoja akiwaeleza madaktari kuwa yeye kutokana na hadhi yake ya Uwaziri hastahiki kwenda kulazwa katika Hospitali ya Kidimni.

Mmoja wa wauguzi anaemshughulikia Waziri huyo amesema, Waziri huyo alipokelewa jana akiwa hali tete, huku akichuruzikwa na wingi wa mafua na kikohozi kisichonyamazika. Uchunguzi wa awali unaonesha kuwa na dalili zote za virusi vya CORONA 🦠

Hali hiyo imepelekea wauguzi na madaktari kuwa katika wakati mgumu huku kila mmoja akikhofia kuambukizwa ugonjwa huo na kuweza kuenea kwa watu wengine, kwa kile kilichotajwa kuwa mbali ya kugoma kwenda Kidimni, lakini pia Waziri huyo amegoma kuvaa mask na vifaa vyengine vya kudhibiti kueneza virusi vya CORONA anavyoshukiwa kuathirika navyo kutokana na Safari yake ya London kisha kupitia Italy na kurejea Zanzibar akiwa na homa kali.

Mmoja wa wauguzi katika Hospitali ya Mnazi Mmoja alisema amesikitishwa sana na kitendo cha Waziri huyo kugoma kupelekwa kwenye kituo cha uangalizi, huku Serikali ikimfumbia macho kwa sababu tu ya cheo chake.

Muuguzi huyo alisema kuwa licha ya taarifa hiyo kupelekwa kwa Waziri wa Afya hadi sasa, hakuna hatua zozote zilizochukuliwa, na mgonjwa huyo bado yupo katika Hospitali ya Mnazi Mmoja pasi na kuvishwa vifaa vya kuzuia maambukizi yasienee kwa wengine.

Kutokana na taharuki hiyo, muuguzi huyo ameiomba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuacha UBAGUZI katika mambo ya msingi yanayoweza kuhatarisha maisha ya Wazanzibar wote!... Ameitaka SMZ kupitia Wizara ya Afya kuhakikisha mgonjwa huyo anaondoshwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja kama ilivyofanyika kwa wagonjwa wengine ili kuepusha kuenea kwa haraka maambukizi ya ugonjwa huo hatari.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…