Je, ni kweli kuna Waziri anaugua Corona inafanywa Siri? Tunaficha nini? Hala hala kisa cha mficha maradhi! Truth & Transparency the only way out!

Kaka Pascal mayalla. Haya Mambo inawezekana ni ya kweli na Kama ni hivi Hawa viongozi wetu wanataka tufe wote? Halafu watamtawala Nani? Yaani kwa staili hii Bora ugonjwa umeanza kule wanakokimbiliaga na hivyo lazima wabaki hapahapa. Hivi wanatuficha taarifa inapelekea watu wanajiachia wakijua hakuna korona kumbe ipo. Leo nimekutana na wazee wa mji hapa kwetu wanasema Hali si shwari maana wametoa mfano kwamba Kuna watu wapo lockup kwamba waliona mgonjwa na wakasema mtaani. Sawa walitoa taarifa ni kosa je vipi idadi mbona haiongezeki? Kiukweli nimeumia Sana baada ya kusikia habari hizi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa
Kama haya yana ukweli basi waziri huyu anahitaji kujua kuwa uwaziri sio kinga dhidi ya covid-19 na atambue yeye ni binadamu kama binadamu wenzake! Asione aibu wala fedheha kwa yy kuambukizwa, bali amshukuru Mungu kwa kuwa angalau anapata matibabu husika na kwa wakati! Aende tu huko alikopangiwa kwenda na hao madaktari!
 

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…