Je, ni kweli kuna Waziri anaugua Corona inafanywa Siri? Tunaficha nini? Hala hala kisa cha mficha maradhi! Truth & Transparency the only way out!

Yaani analeta mapozi kwenye gonjwa kama hili mbona angejitibia mwenyewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Do you mean bongozozo?
 

Sio aibu mkuu. Ni hofu.
 
kuku anakufaje mkuu ?

*MAWAZIRI WETU SMZ BAADHI YENU KWANINI MNAKUA HIVI.*

Inasikitisha sana baada kuisikia na kuipata taarifa hii.
Jana tulisikia jinsi waziri alotoka safari na kuingia hapa kupitia VIP na kukaa Nyumbani akiwa anaumwa na kupelekwa Hosptl ya mnazi mmoja na mwishoe kuishia Kidimni.

Baada ya hili kutokea Purukuchu unapata taarifa za kuaminika Waziri mwengine wa SMZ kayafanya mengine yanayofanana na yale yale.

Kuna mgeni kaingia kutoka Uengereza mgeni wa kike kuna waziri wakiume kaenda uwanja wa ndege kumpokea mgeni uyo na kumpitisha VIP wakati hana hadhi ya kupitia VIP mtu huyo.

lakusikitisha VIP nao kwakua kapitishwa na waziri wakamruhusu na baadala ya kumuandika kaingia wakamuandika katoka baada ya apo akapelekwe kwa maofisa wa immigration Nao wakataka taarifa zake anapokwenda Akaandikwa anakwenda Bububu.

matokeo yake mtu huyo kapelekwa Chukwani Nyumbani kwao. Shida mwanamke baada ya kupitishwa kwamsaada wa waziri akaanza kuwataarifu wenzie walipo ulaya kama kishapita na yupo Nyumbani anafanya shuhuli zake.

Watu wa ulaya ndio walotoa taarifa znz ya hayo yote yalotokea huku hapo ndio taarifa zikaenea mpaka kufika maeneo husika na kufatiliwa uyo mtu na kupatikanwa Chukwani.

Tumuombe mungu awe hana maambukizi je kama atakua nayo nani hasa wakumlaumu kwenye hili?

Kwann tunaowapa dhamana na kuwaamini kwenye hili wanatuangusha haliyakua yote wameyapanga wao watu wakija wafikie wapi na Siku ngapi au Amri hii kwetu sisi tu wenye uluwa haiwahusi.

Hivi kwann mtu hajiambii ikiwa Makamo wa pili wa Raisi wetu Ambae ni mtendaji Mkuu wa shuhuli za serekali na mkewake na watumishi wake wote alokua Nao safari wamezingatia hili na kutii Amri ya Serekali. inakuwaje mtu tu wakawaidi waziri anajitwisha kumpitisha tu Jaman mnalengo gani na sisi tunaoishi humu visiwani?

Inakuwaje mnajipangia mikakati mnashidwa kuitekeleza wenyewe serekali kupitia vikosi vya ulinzi na Salama havilali kwa kulinda mipaka ili watu wasipitishe Kumbe nyie mnawapitishia kwa VIP kuna haja gani ya kuwafanya wasialale majumbani kwao kwa kulinda Taifa.

kwakweli inasikitisha sana Tunaowaamini na kuwaheshim ndio wanaotuhatarishia Maisha yetu haya mkuu ila kwasasa mgeni alopokea kisha chukuliwa yupo KAMILA tuombe mungu awe mzima ili ndugu zetu waokoke Ukanda wa chukwani.
 
*KWENYE LA WAZIRI SALAMA SHUJAA WETU NI DR MARIJANI*

DR Marijani ndio aliongoza kikosi cha Madaktari waliomkatalia Waziri Salama kulazwa Hospital ya mnazi mmoja Licha ya vitisho vingi alivyopewa na Waziri huyo na Baadae KATIBU MKUU KIONGOZI ambae kifamilia ni Baba wa Waziri huyo,Taarifa zinasema Katibu Mkuu kiongozi indiye aliyetaka kulazimisha taratibu za Serikali zipindishwe ili Waziri huyo apewe huduma za VIP hospital hapo badala ya Kwenye kambi iliyotengwa na Serikali,pamoja na Amri hiyo ambayo ilipingwa vikali na Dr MARIJANI ambae aliapa kua yupo Tayari kufukuzwa kazi lakini aokoe maisha ya Wazanzibari wengi,Dr Marijani aliamua kusimamia taaluma yake na kumkatalia katakata Waziri huyo ambae inasemaka alimwagia Dr huyo matusi yasioyoandikika na vitisho kadhaa na pia kufanya vituko kadhaa hospital hapo ambavyo viliashiria kua alikua na dhamira ya makusudi ya kueneza virusi vya Corona kwa Wananchi wengine,ikiwemo kugusa vitu hovyo,kukohoa hovyo akiwa katika wodi na kukataa kuvaa vifaa tiba vya kukinga kuenea kwa maambukizi.

Kwenye Hili Tunampongeza sana Dr Marijani kwa weledi wake na kutohofia vitisho vya Waziri huyo .

Pia Tunamuomba Rais wetu amchukulie hatua kali za kinidhamu Waziri Salama na Katibu Mkuu kiongozi kwani imekua ni kawaida kwa Katibu Mkuu huyo kuingilia maamuzi ya Viongozi au watendaji wengine katika mambo yenye maslahi nae.

*HONGERA DR MARIJANI kwa kunusuru maisha ya wengi*

Itaendelea......
 
Mkuu,huu unaoufanya ndio uzalendo halisi. Mungu akubariki.
Sent using Jamii Forums mobile app
 

Pascal Mayalla nimepata habari za kuwa SMZ walikua wana zingua kutaka kulinda na kumlinda sijui kwa sababu ila habari ilimfikia JPM aka amrisha JW wamtoe hapo apelekwe kunako husika. Na ambulance ya jeshi imemtoa hapo na kumpeleka Kidimni.



Sent from my iPad using JamiiForums
 
Ameikimbia Dar kaenda Dodoma,corona ikamfata Dodoma kakimbia Chattle,Aijui Habari zinaelezeaje kuhusu maendeleo yake?
 
Maendeleo hakuna kwani tayari ameambukiza wengine nyumbani na wauguzi..it is very unfortunate uzembe kufanywa na Waziri wa serikali . Lazima achukuliwa hatua za kinidhamu


Sent from my iPad using JamiiForums
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…