- Source #1
- View Source #1
Kumekuwepo na video iliyochapishwa kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook ikidai kuwa kutokana na wimbi kali la joto linaloendelea kulikumba bara la Ulaya, hususan nchini Ujerumani, baadhi ya mataa ya kuongozea magari yaliyowekwa kandokando ya barabara yameanza kuyeyuka kutokana na kiwango kikubwa cha joto.
kutokana na hilo ni upi uhalisiawa videi hiyo?
kutokana na hilo ni upi uhalisiawa videi hiyo?
- Tunachokijua
- Ufuatiliaji wa JamiiCheck kupitia Google reverse image search umebaini video iliyochapishwa katika mtandao wa X, inayonekana kurekodiwa sehemu mbili tofauti ikiwa na madai pia yanayoeleza kiwango cha joto kilichoongezeka na kukaribia kufikia nyuzi 40°C hadi 45°C kwamba tayari yameanza kuonesha athari zake barani Ulaya.
Hata hivyo baadhi ya wasomaji katika chapisho hilo wanabainisha muktadha tofauti kuwa video inayosambazwa ikidai kuwa inaonesha taa za kuongozea magari zilizoyeyuka kutokana na wimbi hilo la joto si ya tukio la sasa na kueleza video hiyo inatokana na ajali ya moto wa iliyotokea mjini Milan, Italia, mwaka 2022.
Kadhalika sehemu ya maoni katika chapisho hilo mdau mwingine anabainisha kuwa video hiyo ilirekodiwa mbele ya ukumbi wa burudani wa Wilde Renate, ulioko kandokando ya Mto Spree mjini Berlin, Ujerumani.
Ukumbi huo uliharibiwa na moto uliozuka katika majira ya joto ya mwaka 2025. Joto kali lililotokana na moto huo ndilo lililosababisha taa ya kuongozea magari iliyokuwa nje ya jengo kuharibika.
Kadhalika anaeleza kuwa taa hiyo iliyoharibika haitumiki tena, na kwa sasa imebadilishwa kwa kuwekwa taa ya muda, ambayo inaonekana nyuma yake kwenye video.
Tazama hapa muonekano wa eneo hilo nchini Ujerumani kwenye ramani.
Aidha sehemu ya mwanzo ya video hiyo inaelezwa kuwa idara ya zimamoto ilithibitisha kuwa 'scooter' iliwaka moto karibu na Viale Regina Margherita mjini Milan. Ingawa joto kali huenda lilichangia kuanzisha moto, hasa baada ya skuta hiyo kujazwa mafuta, taa ya kuongozea magari haikuwaka kutokana na joto moja kwa moja, bali iliharibiwa na moto uliotokana na skuta hiyo. Polisi pia walithibitisha kuwa eneo hilo lilisafishwa mara moja na hali kurejea kuwa ya kawaida.
Tazama eneo hili ilipo taa hiyo hapa.