Je, ni kweli kuwa Dodoma CBD inaipiku Mwanza CBD?

Je, ni kweli kuwa Dodoma CBD inaipiku Mwanza CBD?

Najua ni mara chache sana watu kuizungumzia Dodoma kwa sababu wanai-underrate nakudhani kuwa Dodoma imelala ukweli mchungu ni kuwa kwa kasi ya ukuaji wa mji huu kuna majiji mengi nchini yajiandae kukabidhi crown very soon akiwemo mbabe Mwanza ambaye so far bado anahold title la jiji kubwa after DSM wakati DOM yeye akishikilia title la jiji la Kisasa zaidi after DSM hayo ndo maoni yangu utaki leta evidence kuwa MWANZA CBD nizaidi ya DODOMA CBD

Hivyo kwa heshima ya Dodoma mpya na ya kisasa ambayo kwa mtizamo wangu binafsi inaichapa Mwanza 3-0 kwenye ukubwa wa City Center (CBD)

Kuanzia majengo mengi ya ghorofa, ukisasa, mpangilio, bustani na round about nzuri, purchasing power (vitu bei ni juu na watu wana-afford) ndiyo maana mabasi makali na ghali mengi uanzia safari zake hapa kuelekea Dar nasiyo vinginevyo.

Kingine Dodoma CBD bado inakuwa kila sekunde mijengo inazidi chepushwa tena project za maana, ila Mwanza CBD haina jipya sana zaidi ya soko linalojengwa pale hamna kingine chakutarajia kwa sasa, kinachoiangusha Dodoma CBD ni ubaya wa soko lake kuu la majengo(ombi langu kwa mamlaka husika walifanyie mpango wa maboresho linafubaza jiji) ila kwingine huko kote ni fire.

CBD ya Dodoma inaichapa mwanza upande wa barabara za lami, private cars na magari ya kifahari,mandhari ya kimjini mjini kama ni mgeni ukiwa mazengo ukajichanganya majengo huko kwa kina vunja bei bila kusahau uhindini n.k wawezadhani uko kariakoo ndogo, Dodoma CBD ina city vibes ukilinganisha na mwanza CBD.

MADHAIFU:
I. Ukarimu na kauli za kibiashara(customer care) ni "F"

II. Usafi ni "F'' mifereji inanuka vinyesi plus taka zinatupwa tu ovyo na hakuna hatua yeyote inachukuliwa mara mia na halmashauri ya manispaa ya Singida.

III. Upande wa Mahoteli na viwanja nawapa "D" demand bado nikubwa kuliko kilichopo, ukiiondoa Morena ambayo nayo ni yakawaida sana bado hakuna hotel za maana.

IV. Hali ya hewa ya vumbi la kuwasha macho, ukame na unusu jangwa, hata kama umetupia nguo mpya na Kali vipi zinaappear zimefubaa nakupaukiana achilia mbali baridi kali usiku. (Tushirikiane wote kuakikisha Sera ya Dodoma ya kijani inatekelezwa kwa vitendo)

V. Shida ya MAJI hapa usishangae chumba kimoja kikilipiwa 15k na kingine kinachofanana nacho kwa kila kigezo kikilipiwa 30k kumbe kigezo ni kimoja kina maji na kingine hakina. Jamani SERIKALI timizeni majukumu yenu mruhusu jiji hili lifunguke zaidi na likuwe maana kikwazo kikuu ni hiki kabla ya vingine.

But all in all ukiondoa mapungufu hayo machache, mwanza CBD inakalishwa benchi kipindi cha kwanza cha mchezo hata kabla ya kipyenga cha mwamuzi kuamuru game lianze.

TAKE HOME
Ninachoipendea Dodoma; UZALENDO kwani karibia asilimia 95 ya majengo yote, mabango na mapambo CBD lazima neno DODOMA litaappear unlike mwanza na sehemu zingine za Tanzania hii.
Upo Sahihi kabisa

Jiji la Mwanza linahujumiwa maendeleo kimaksudi na serikali (Mtazamo)
Hawaleti maendeleo ya miundombinu kwa maksudi licha ya kuchangia mapato makubwa serikalini
 
Mwanza kiuchumi na hata majengo Ipo mbali, licha ya kuwa miradi mingi inajengwa Dodoma Kwa kisingizio cha miji mkuu, Mwanza inahujumiwana na kufanyiwa fitina kimakusudi licha ya kuwa ndo mji WA pili Kwa kuingiza mapato, Dodoma inapendelewa japo haijafika Kwa mwanza

Ukitaka kuthibitisha Fanya tafiti waulize Watu 20 kuwa Kati ya Dom na Mwanza wangetamani kuishi wapi jibu utalipata
 
Miradi mipya mikubwa kama

1. Ring Road (watu wanaosafiri miji mikubwa wanajua umuhimu wake)

2. Magufuli Government city (watu wa fursa wanajua namaanisha nini)

3. SGR (urahisi wa ku connect na Dar)

4. City planning/ zones (Bara bara nyingi ndani ya jiji zenye option kibao foleni huko dodoma ni ndoto)

5. New International Airport na Stadium

Hivi vinaifanya DODOMA ivutie kimakazi kuliko hata DAR ambayo ipo Over-congested kwa kero za foleni na biashara/ maeneo yasiyo rasmi

So kwa TANZANIA nadhani Dodoma hivi sasa ni the BEST
 
Mwanza kiuchumi na hata majengo Ipo mbali, licha ya kuwa miradi mingi inajengwa Dodoma Kwa kisingizio cha miji mkuu, Mwanza inahujumiwana na kufanyiwa fitina kimakusudi licha ya kuwa ndo mji WA pili Kwa kuingiza mapato, Dodoma inapendelewa japo haijafika Kwa mwanza

Ukitaka kuthibitisha Fanya tafiti waulize Watu 20 kuwa Kati ya Dom na Mwanza wangetamani kuishi wapi jibu utalipata
Stori za kishabiki na vijiweni hizi unaleta eti majengo😀😀 unajua idadi ya maghorofa yaliyopo Udom,Magufuli City,Medeli,Tambukareli,Kisasa,Njedengwa,Mji Mpya,City Centre nk. Kwa sasa Mwanza Jiji haifiki hata nusu ya maghorofa yote ya Dodoma Jiji.
Alafu kwa taarifa yako tu Dodoma ndio Jiji la pili Tanzania linaloongoza kwa mapato ya halmashauri na TRA .Tatizo huwa mnachanganya kati ya halmashauri ya Jiji na mkoa, ni kweli mkoa wa Mwanza(wenye halmashauri 8) umeupita mkoa wa Dodoma kwenye GDp lakini Mwanza kama Jiji haifiki hata nusu ya Dodoma Jiji kama Jiji👇👇

 
Miradi mipya mikubwa kama

1. Ring Road (watu wanaosafiri miji mikubwa wanajua umuhimu wake)

2. Magufuli Government city (watu wa fursa wanajua namaanisha nini)

3. SGR (urahisi wa ku connect na Dar)

4. City planning/ zones (Bara bara nyingi ndani ya jiji zenye option kibao foleni huko dodoma ni ndoto)

5. New International Airport na Stadium

Hivi vinaifanya DODOMA ivutie kimakazi kuliko hata DAR ambayo ipo Over-congested kwa kero za foleni na biashara/ maeneo yasiyo rasmi

So kwa TANZANIA nadhani Dodoma hivi sasa ni the BEST
Exactly, Kwa sasa Dodoma ndio kipimo halisi cha ubora wa mipangomiji na miundombinu sio tu kwa miji ya apa Tanzania bali hata kote East&Central Africa...👇👇


View: https://www.instagram.com/reel/DbX-iSAMPsY/?igsh=ZXF3YnduY3JieWFu
 
Back
Top Bottom