Je, ni kweli kuwa Dodoma CBD inaipiku Mwanza CBD?

Je, ni kweli kuwa Dodoma CBD inaipiku Mwanza CBD?

Bilion nne nazo ni za kujisifu kweli? Yaani hospital ya rufaa ya mkoa inajengwa kwa bilion nne nazo unaona nongwa, mabilion mangapi yanaenda huko Dar na mikoa pendwa hatusemi.
Acha kuhoji kama mbumbumbu,hizo ni.pesa za.kuanzisha ujenzi Hadi ikamilishe si chini ya Bilioni 25
 
Acha kuhoji kama mbumbumbu,hizo ni.pesa za.kuanzisha ujenzi Hadi ikamilishe si chini ya Bilioni 25
Watajua wenyewe huko, kwanza inakuwaje hospital ya sekoe toure inashushwa daraja na ilo la ukerewe ndio litakuwa ni hospital ya rufaa ya mkoa, na kwanini wasijenge sekoe toure na huko ukerewe wajengewe hospital kubwa ya wilaya.
 
Huu ni kweli japo kuna miji itajikongoja na mingine itakufa kabisa, serikali ina nguvu sana kwenye uwekezaji, we angalia Dodoma ndio utajua.
Wacha visingizio.Dom inaendelea Kupeleka kichapo Kwa Mwanza 😁😁👇👇
 
Najua ni mara chache sana watu kuizungumzia Dodoma kwa sababu wanai-underrate nakudhani kuwa Dodoma imelala ukweli mchungu ni kuwa kwa kasi ya ukuaji wa mji huu kuna majiji mengi nchini yajiandae kukabidhi crown very soon akiwemo mbabe Mwanza ambaye so far bado anahold title la jiji kubwa after DSM wakati DOM yeye akishikilia title la jiji la Kisasa zaidi after DSM hayo ndo maoni yangu utaki leta evidence kuwa MWANZA CBD nizaidi ya DODOMA CBD

Hivyo kwa heshima ya Dodoma mpya na ya kisasa ambayo kwa mtizamo wangu binafsi inaichapa Mwanza 3-0 kwenye ukubwa wa City Center (CBD)

Kuanzia majengo mengi ya ghorofa, ukisasa, mpangilio, bustani na round about nzuri, purchasing power (vitu bei ni juu na watu wana-afford) ndiyo maana mabasi makali na ghali mengi uanzia safari zake hapa kuelekea Dar nasiyo vinginevyo.

Kingine Dodoma CBD bado inakuwa kila sekunde mijengo inazidi chepushwa tena project za maana, ila Mwanza CBD haina jipya sana zaidi ya soko linalojengwa pale hamna kingine chakutarajia kwa sasa, kinachoiangusha Dodoma CBD ni ubaya wa soko lake kuu la majengo(ombi langu kwa mamlaka husika walifanyie mpango wa maboresho linafubaza jiji) ila kwingine huko kote ni fire.

CBD ya Dodoma inaichapa mwanza upande wa barabara za lami, private cars na magari ya kifahari,mandhari ya kimjini mjini kama ni mgeni ukiwa mazengo ukajichanganya majengo huko kwa kina vunja bei bila kusahau uhindini n.k wawezadhani uko kariakoo ndogo, Dodoma CBD ina city vibes ukilinganisha na mwanza CBD.

MADHAIFU:
I. Ukarimu na kauli za kibiashara(customer care) ni "F"

II. Usafi ni "F'' mifereji inanuka vinyesi plus taka zinatupwa tu ovyo na hakuna hatua yeyote inachukuliwa mara mia na halmashauri ya manispaa ya Singida.

III. Upande wa Mahoteli na viwanja nawapa "D" demand bado nikubwa kuliko kilichopo, ukiiondoa Morena ambayo nayo ni yakawaida sana bado hakuna hotel za maana.

IV. Hali ya hewa ya vumbi la kuwasha macho, ukame na unusu jangwa, hata kama umetupia nguo mpya na Kali vipi zinaappear zimefubaa nakupaukiana achilia mbali baridi kali usiku. (Tushirikiane wote kuakikisha Sera ya Dodoma ya kijani inatekelezwa kwa vitendo)

V. Shida ya MAJI hapa usishangae chumba kimoja kikilipiwa 15k na kingine kinachofanana nacho kwa kila kigezo kikilipiwa 30k kumbe kigezo ni kimoja kina maji na kingine hakina. Jamani SERIKALI timizeni majukumu yenu mruhusu jiji hili lifunguke zaidi na likuwe maana kikwazo kikuu ni hiki kabla ya vingine.

But all in all ukiondoa mapungufu hayo machache, mwanza CBD inakalishwa benchi kipindi cha kwanza cha mchezo hata kabla ya kipyenga cha mwamuzi kuamuru game lianze.

TAKE HOME
Ninachoipendea Dodoma; UZALENDO kwani karibia asilimia 95 ya majengo yote, mabango na mapambo CBD lazima neno DODOMA litaappear unlike mwanza na sehemu zingine za Tanzania hii.
CBD ndo kitu gani mkuu. Hebu tupe ufafanuzi
 
Shida ya Mwanza ni kukosa uwanja wa ndege wa kimataifa vinginevyo Mwanza ni kubwa by population,mzee
Population ndio nini? Dar ni kubwa Kwa population kuzidi Nairobi,vipi Dar inaifikia Nairobi Kwa kipi? 🤪🤪

Ndivyo ilivyo hata Kwa Dom vs Mwanza .

Go Dom go 👇👇

View: https://www.instagram.com/p/C4ishbqNqBg/?igsh=ZWN0MzF6ODZjcWdz
1432947823.jpg
228353673.jpg
-1464378417.jpg
 
Back
Top Bottom