- Source #2
- View Source #2
Kumekuwa na madai kwamba Bill Gates na baadhi ya mabilionea pamoja na wanasayansi wanaingiza kwa makusudi katika mfumo wa chakula matunda yasiyo na mbegu au yasiyoweza kuzaliana, kwa lengo la kuwafanya watu wategemee mbegu zinazodhibitiwa na makampuni yao.
Katika chapisho hilo, mdai anasema kuwa mabilionea hao wanaingiza hatua kwa hatua matunda yasiyo na mbegu na yasiyoweza kuzaa katika vyakula vya kila siku. Anaongeza kuwa tunda ambalo haliwezi kupandwa tena kutoka kwenye mbegu zake na ambalo linapatikana kupitia makampuni fulani linapaswa kuwafanya watu kujiuliza kuhusu chanzo na madhumuni ya teknolojia hiyo.

- Tunachokijua
- Hakuna ushahidi wowote wa kisayansi, kisheria, au kiserikali unaothibitisha kuwa makampuni au taasisi za Bill Gates zinaingiza matunda yasiyo na mbegu barani Afrika kama mpango wa kudhibiti chakula au kilimo.
Madai haya ni miongoni mwa nadharia za njama (conspiracy theories) zinazosambazwa mara kwa mara kwenye mitandao ya kijamii. Ukweli kuhusu suala hili unajumuisha mambo yafuatayo.
Matunda yasiyo na mbegu (kama vile tikiti maji yasiyo na mbegu, zabibu, au ndizi tunazokula kila siku) hayatokani na maabara za siri za Bill Gates. Yanatengenezwa kwa kutumia mbinu za kawaida za kibaolojia za uboreshaji wa mimea (cross-breeding au triploidy).
Taasisi ya Bill & Melinda Gates (BMGF) inafadhili miradi mbalimbali ya utafiti wa kilimo barani Afrika kupitia mashirika kama AGRA (Alliance for a Green Revolution in Africa) na CGIAR. Miradi yao kuu inajikita kwenye:
- Mbegu zinazostahimili ukame: Mfano wa miradi ya mahindi yanayoweza kuvumilia ukame na joto kali (k.m. miradi ya WEMA/AATF).
- Mazao yenye lishe iliyoongezwa (Biofortification): Mfano wa viazi lishe vya zambarau/njano vilivyoongezwa Vitamini A, na aina za muhogo unaostahimili magonjwa ya milipuko (kama Cassava Mosaic Virus).
- Kusaidia wanasayansi wa ndani ya Afrika: Kutoa ufadhili wa maabara za utafiti wa kilimo nchini Tanzania (k.m. TARI), Kenya, na Uganda.