Tetesi: Je, ni kweli kuwa siku hizi ukifanya miamala mikubwa benki unafuatiliwa hata akaunti kushikiliwa?


Ishu nadhani ni kufuatilia mtiririko wa fedha kwenye akaunti husika na sio kiwango kilichowekwa kwa mkupuo. Unaposema 5m ni ndogo ni sawa, ila watakatisha fedha wanaweza kutumia hiyo loophole. Mfano wengi hua wanatumia hiyo mbinu ya kuweka viwango vidogo vidogo kwa muda mrefu. Mtu ana 500m anakua anadeposit 5m kila siku kwa miezi kadhaa mfululizo. We ukisubiri uone 50m ndio ushtuke unafeli.
 
Kuweka sio shida elewa nawe, shida wakati wakuchukua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna bank wanakataa pesa wataendeshaje shughuli zao, swala lipo ukitaka kuitoa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nilifungua akanti kama leo, kesho nikajitumia laki tatu na kidogo (300,000+) kutoka kampuni ya kubet ya Urusi. Baada ya siku nne nikapigiwa simu kutoka hiyo bank wananiuliza tena kazi ninayofanya, nikawaambia mi mhangaikaji tu wa mjini.
Unaishi mtaa gani? Nikamwambia si niliandika maelezo yote kwenye fomu hapo? Oh tunataka tuhakikishe.
Nikawaambia nakaa kata ya Mwananyamala. Hoo, mwaka 2014 ulikuwa ulikuwa unaishi Ubungo, ulikuwa unafanya nini? Nikamuuliza hayo maswali yote ni kwa ajili ya hiyo laki tatu au? Hapana, ni utaratibu wetu wa benki. Ila nashukuru tulimalizana ila nilijihisi kama mwizi hivi.
 
Ni kweli kabisa kuna 7m nilitaka kutoa na ilitumwa kumi alafu ndan ya nusu SAA ndiyo nilienda kutoa toka itummwe! Yaan ilichukua lisaa mpaka aliyetuma alipigiwa simu!
 
Ungeenda kutoa ndiyo ungejua!
 
Huh! KCB ni worse. Ukitumiwa hela mpaka itoke umefanyakazi aisee, wanasumbua sana wakati mwingine taarifa zote zpo.
 
Ni kweli lakini inategemea na hadhi, biashara yako nk..! Inshort mtu kama Mo Dewji anaweza kutoa na kuweka zaidi ya milion 500 bila ata kuulizwa na mtu yeyote lakini kama wewe mwenzangu namimi kwenye A/C yako kuna milion 5 na miamala yako kila mwezi labda ni laki 2 au laki 3 then siku unaenda unaweka milion 50 hapo utasumbuliwa mpaka useme hiyo hela umetoa wap..! Na si Tanzania tu suala hili ata huko Ulaya wanafanya hivyo kuhofia utakatishaji wa fedha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…