Tetesi: Je, ni kweli kuwa siku hizi ukifanya miamala mikubwa benki unafuatiliwa hata akaunti kushikiliwa?

Tetesi: Je, ni kweli kuwa siku hizi ukifanya miamala mikubwa benki unafuatiliwa hata akaunti kushikiliwa?

Lakini kitengo hicho hakifuatilii kiasi kidogo cha fedha kama ulizosema M 5,hicho ni kiasi cha kawaida hata mwendesha bodaboda anaweza kuwa nacho kwenye akaunti yake.FIU wanadeal na amount ya kuanzia 50M and above,Lakini Milioni 5 ni kiasi cha kawaida kabisa.

Sent using Jamii Forums mobile app

Ishu nadhani ni kufuatilia mtiririko wa fedha kwenye akaunti husika na sio kiwango kilichowekwa kwa mkupuo. Unaposema 5m ni ndogo ni sawa, ila watakatisha fedha wanaweza kutumia hiyo loophole. Mfano wengi hua wanatumia hiyo mbinu ya kuweka viwango vidogo vidogo kwa muda mrefu. Mtu ana 500m anakua anadeposit 5m kila siku kwa miezi kadhaa mfululizo. We ukisubiri uone 50m ndio ushtuke unafeli.
 
Mwaka Juzi nilienda kufungua account Bank flani hapa Dar es salaam, na at the same time nikaweka 8 millions Cash....

Sikuulizwa hata kuwa pesa nimetoa wapi..!

Nadhani kuna kiwango flani ukiweka Bank au kupokea ndo unaweza kuulizwa, may be kuanzia 30+ millions......
Kuweka sio shida elewa nawe, shida wakati wakuchukua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwaka Juzi nilienda kufungua account Bank flani hapa Dar es salaam, na at the same time nikaweka 8 millions Cash....

Sikuulizwa hata kuwa pesa nimetoa wapi..!

Nadhani kuna kiwango flani ukiweka Bank au kupokea ndo unaweza kuulizwa, may be kuanzia 30+ millions......
Kuna bank wanakataa pesa wataendeshaje shughuli zao, swala lipo ukitaka kuitoa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nilifungua akanti kama leo, kesho nikajitumia laki tatu na kidogo (300,000+) kutoka kampuni ya kubet ya Urusi. Baada ya siku nne nikapigiwa simu kutoka hiyo bank wananiuliza tena kazi ninayofanya, nikawaambia mi mhangaikaji tu wa mjini.
Unaishi mtaa gani? Nikamwambia si niliandika maelezo yote kwenye fomu hapo? Oh tunataka tuhakikishe.
Nikawaambia nakaa kata ya Mwananyamala. Hoo, mwaka 2014 ulikuwa ulikuwa unaishi Ubungo, ulikuwa unafanya nini? Nikamuuliza hayo maswali yote ni kwa ajili ya hiyo laki tatu au? Hapana, ni utaratibu wetu wa benki. Ila nashukuru tulimalizana ila nilijihisi kama mwizi hivi.
 
Huo utaratibu upo tokea zamani. Ulianzishwa kudhibiti utakatishaji wa pesa haramu (Anti Money Laundering). Ukipokea pesa kuanzia hata 5 M kama sio kawaida yako, utatakiwa utoe maelezo ya kuridhisha hizo pesa ni kwa ajili ya kitu gani. Utoe vilelezo umezipataje. Hilo ni takwa la BoT.

Sasa kwa mfano akaunti yangu wamezoea kuona mshahara unaingia mara moja, natoa ATM mara mbili tu unakata, ghafla inawekwa Milioni 10, lazima wahoji. Hapo TRA hata hawahusiki.
Ni kweli kabisa kuna 7m nilitaka kutoa na ilitumwa kumi alafu ndan ya nusu SAA ndiyo nilienda kutoa toka itummwe! Yaan ilichukua lisaa mpaka aliyetuma alipigiwa simu!
 
acheni kudanganya umma. hakuna wa kukuuliza , nimeuza toyota harrier new model this january jamaa kaingia CRBD internet banking kahamisha mzigo wa kutosha kwa accnt yangu (more than 19M) , hakuna wa kuniuliza wala jamaa hajaulizwahadi leo. ...hzo mambo za kuulizana pesa umetolea wapi ni kama unafanya transaction counter ama vp ?

All is Well
Ungeenda kutoa ndiyo ungejua!
 
Huh! KCB ni worse. Ukitumiwa hela mpaka itoke umefanyakazi aisee, wanasumbua sana wakati mwingine taarifa zote zpo.
 
Naomba ufafanuzi kwa wajuvi tafadhali;
Nasikia tetesi kwamba ukiwa na pesa ndefu kwenye Akaunti au Akaunti ikitumiwa (ikiingiziwa)au kupokea pesa ndefu mathalani kuanzia 15milion nakuendelea unafuatiliwa kujieleza na TRA?

Nasikia hususani aliyetuma akiwa mfanya biashara mkubwa pesa hiyo inashikiliwa kwa kosa la utakatishaji fedha!?
Naomba mwenye taarifa zaidi anifahamishe kabla sijaingiziwa pesa ya nyumba yangu niliyoiuza!!

Nitafurahi zaidi kama nitapewa na mwongozo unaotakiwa kuzingatiwa kisheria kabla ya kuingiziwa pesa ndefu hususani hizi pesa za malipo au hata zile za Kubet!
Ni kweli lakini inategemea na hadhi, biashara yako nk..! Inshort mtu kama Mo Dewji anaweza kutoa na kuweka zaidi ya milion 500 bila ata kuulizwa na mtu yeyote lakini kama wewe mwenzangu namimi kwenye A/C yako kuna milion 5 na miamala yako kila mwezi labda ni laki 2 au laki 3 then siku unaenda unaweka milion 50 hapo utasumbuliwa mpaka useme hiyo hela umetoa wap..! Na si Tanzania tu suala hili ata huko Ulaya wanafanya hivyo kuhofia utakatishaji wa fedha.
 
Back
Top Bottom