Je, ni kweli kuwa ulimwengu huu ni kifungo cha nafsi?

Je, ni kweli kuwa ulimwengu huu ni kifungo cha nafsi?

Nadhani ndio maana mjani unatumiwa kama ibada kwa baadhi ya imani,

Ile kitu hata bila ya kujiuliza inafanya wewe ujijue ni nani.
Yes kwa namna moja au nyingine Ile kitu Ina faida zake nyingi tu mwilini, sema ndio hivyo propaganda ndio zimetawala
 
Binafsi napenda hawa watu wa dini na vitabu vya injili na vingne wabaki na ujinga wao tu.

Kwa sababu ata ukiwaambia ukwel upo ndani yao hawata kuelewa kamwe .
Wanakuona we hufai kumbe ambao hawafai ni wale wanaowalisha matango pori huko wanakokutania
 
Hizi hadith za kuona nilizisikia kabla sijapata spiritual initiotion na kuzani kwenye meditation kunakuona kama theator za cinema hivi. Nimefanya meditation Lights and Sound kwa miaka 40 sasa uzoefu umenionyesha kwamba ukiona kitu au kusikia chochote wakati wa meditation unakuwa bado unastragle kwenye state of mind hiyo illusination or imagination. Real meditation states you see or hear nothing. Third eye ni additional sense of realizing things ambazo under normal awareness can not be easily complihanded kama vile kuiona kweli kwenye uongo.
Uko sahihi kabisa mkuu
 
Jimena shukran mkuu, elimu umeitoa 2016 nilkuwa mdogo kiufaham enzi hizo

yote ulioeleza nimejifunza 2023
umeongea ukweli ambao mtu aliemezeshwa fikra za uhalisia hawezi kuubeba

njia pekee ya kuweza kuujua ukweli ni kuweza "kuuwa natural fear" ambayo watu wamekuwa conditioned kuishi nayo

note:The third eye is you mind
Karibu sana mkuu, nimefurahi kupata uzoefu kutoka kwako
 
Wewe hayo umeyapatia wapi nyinyi ndo mnaanini vitabu vya maprofessa je hao nd wamekuumba wewe walikuwepo kipind Cha Adam na Hawa ujielewi acha kucopy na kupaste mungu akosei ss misingi yetu hpo katika dini na dini hyo nd umetupa upendo na ustaarabu sisi wenyewe nd tunafanya mzaa lkn bila dini we ungekuwa sio hpo mpk sasa maisha yko yangekuwa kama mnyama
Mkuu, dini sio lolote kwenye haya maisha.
 
Honestly, nimeusoma uzi mara moja, na kuuelewa vema kabisa. Nipe changamoto na experience ya maisha yako kabla ya kufahamu maarifa haya, na baada ya kuyaelewa

(Ukipata muda mtafute Dr. Bruce Lipton vitabu vyake vya kufaaa sana)
Mi nimejifunza maarifa haya mapema kidogo sababu mshua alikuwa anamfatilia Munga tehenan. Bruce Lipton namfahamu vyema na namfuatilia sana you tube, yule Mzee anajitambua na anajitahidi sana kufundisha watu waamke
 
Mkuu apa duniani mwanadamu hawezi kuwa huru kamwe! Kuna kosa kubwa sanaa tumefanya wanadamu wote tunaozaliwaa kwenye hii dunia. Ndio maana tupo hapa kuadhibiwa, ukifuatilia vitabu utaona kuna kosa mwanadamu alifanya.

Kuna vifungo viwili vikuu kifungo cha mwili na kifungo cha akili. Mfano wa vifungo vya mwili n kama ukomo wa kuishi, bahari, msitu mnene, jangwa, anga, bonde. Mfano vifungo vya akili kila wazo kufungamana na mda huwezi ukawaza kitu kisicho na mda na nafasi.
 
Mkuu apa duniani mwanadamu hawezi kuwa huru kamwe! Kuna kosa kubwa sanaa tumefanya wanadamu wote tunaozaliwaa kwenye hii dunia. Ndio maana tupo hapa kuadhibiwa, ukifuatilia vitabu utaona kuna kosa mwanadamu alifanya.

Kuna vifungo viwili vikuu kifungo cha mwili na kifungo cha akili. Mfano wa vifungo vya mwili n kama ukomo wa kuishi, bahari, msitu mnene, jangwa, anga, bonde. Mfano vifungo vya akili kila wazo kufungamana na mda huwezi ukawaza kitu kisicho na mda na nafasi.
Mkuu unaposema mwanadamu hawezi kuwa huru ni uhuru gani unaoumaanisha🤔🤔
 
Mkuu unaposema mwanadamu hawezi kuwa huru ni uhuru gani unaoumaanisha🤔🤔
Kuishi kwa amani ya kweli, kipindi chochote tulivu utakachopataa kina mwisho, mda wowote kipindi hicho cha heri kimaisha. ni jambo la mda tuu. Ndio maana huwezi kuwa na furaha siku nzima.
 
Kuishi kwa amani ya kweli, kipindi chochote tulivu utakachopataa kina mwisho, mda wowote kipindi hicho cha heri kimaisha. ni jambo la mda tuu. Ndio maana huwezi kuwa na furaha siku nzima.
 
Kuishi kwa amani ya kweli, kipindi chochote tulivu utakachopataa kina mwisho, mda wowote kipindi hicho cha heri kimaisha. ni jambo la mda tuu. Ndio maana huwezi kuwa na furaha siku nzima.
Unaweza kuwa na furaha sio tu siku nzima Bali siku zote.
Hata hivyo katika maisha hakuna kitu permanent hata haya maisha yenyewe ni temporary mkuu
 
Kwa kipindi kirefu sasa nimesikia mafundisho ya kwamba dunia hii ni kifungo cha nafsi na roho za watu... na pia wapo watu mahsusi kwa kazi ya kufungua hizi nafsi na roho zilizofungwa.

Kwanza kabisa ningependa ndugu zangu tutambue ya kwamba sisi binadamu tupo katika ASTRAL, inamaana kwamba hakuna tofauti yeyote ile katika ulimwengu unaoonekana na usiooneka, Vitu ambavyo unaweza kuvijua au kuexperience wakati umekufa pia unauwezo wa kuvitambua sasa, hivyo basi jukumu ni lako kama utataka kuvijua sasa au hadi pale utakapoonja mauti,

Katika hii dunia tunayoishi kila kitu kipo katika kanuni au sheria ambazo zinawezesha huu ulimwengu kufanya kazi zake sawia, hivyo kwa kila jambo ambalo linapata kutokea hapa duniani lina sababu zake, na sababu ndio huleta matukio... sasa ningependa mtambue hapa duniani hakuna aina yeyote ile ya miujiza, kwa sababu miujiza ni kitu ambacho hutenda kazi kinyume cha sheria za ulimwengu huu, hivyo basi ili miujiza ili iweze kutenda kazi ni lazima ifuate kanuni na sheria...

Je, tutaendelea kuita ni miujiza? Kuibuka kwa neno muujiza ni kukosa kwetu maarifa ya kutambua kanuni na sheria za ulimwengu huu.

Hii dunia au ulimwengu sio jela wala kifungo cha nafsi wala roho za watu na wala haitakuja kuwa hivyo.

Kama utakuwa unajua chochote kuhusu LAW OF ATTRACTION utaweza kutambua ya kwamba kitu chochote unachokielekezea nguvu(energy) ndivyo kitu hicho kitazidi kukua au kuongezeka, ina maana kwamba kama watu watazidi kuelekeza nguvu zao katika mambo wasiyoyataka au mabaya ndivyo watakavyozidi kuzalisha na kuyakaribisha wasiyoyataka na mabaya zaidi ya hapo mwanzo, au utashangaa kitu gani kuona mpingaji au mkemeaji wa vitu asivyovitaka akivifanya hivyohivyo anavyopinga?

Jaribu kuchunguza maeneo ambayo kuna mafundisho mengi ya kukemea vitu vibaya au vile wasivyovitaka hali ikoje? Ndugu zangu ningependa mtambue ya kwamba vitu vibaya au vile tusivyovitaka kamwe haviwezi kuondolewa kwa kuvifikiria vitu hivyo au kuviwekea nguvu... labda kama tutakuwa na uhitaji wa makubwa yake.

Ni watu pekee ambao huleta matatizo na kukimbia matokeo ya kile walicho kileta ndio hukimbilia kusema uwepo wa kufungwa kwa nafsi na roho zao katika huu ulimwengu, na ndio aina ya watu hawahawa hubaki kunyosha vidole vyao katika mambo mabaya tu, huona mabaya yanayofanya na papa au vatican, huona mabaya ya Rothischilds family, huona mabaya ya malkia wa uingereza, huona mabaya ya U.S.A n.k bila ya kujua watu hawa huelekeza nguvu(energy) zao katika maisha na mambo yao wenyewe kuwa kweli, na sisi pia kwa kiasi kikubwa huendeleza maisha yao kuwa kweli kwa kuwekeza nguvu(energy) zetu kwao.

Ndugu zangu hapa duniani hakuna nafsi wala roho ya mtu yeyote iliyo kifungoni... ila matatizo yote haya yameanzia pale tulipo ukimbia mwanga,mwanga wa kweli hivo tukaanza uoga na kuamini tusivyovijua, na kwa uoga huohuo hatuwezi kuhoji juu ya kile tunachoamini, imefika hatua kwamba watu wanatamani kufa na kwenda kuishi mbinguni, lakini swali la kujiuliza ni kwamba kama maisha ya duniani umeyashindwa je una uhakika upi kama ya mbinguni utayaweza? Maana mbinguni ni kama duniani(As above as below).

Ndugu zangu baada ya kupita na kukua kimwili huu ni wakati muafaka wa kukua kimaarifa, tuache kuwa kama watoto wadogo wanaolalamika bila ya kuchukua hatua zozote zile, huu ni wakati wa kushika majukumu yako na kuacha kunyosha vidole na kuhukumu wengine, maana pale unavyomhukumu mtu pia ujue hata wewe pia unajihukumu, ila mbaya zaidi hutaishi.....

Watu ambao huwataki ndivyo wao wenyewe walivyoamua kuwa hivyo, je ni vipi kwa wale ambao hawakutaki pia? Je si kwa jinsi wewe ulivyoamua kuwa hivyo?... Ni vigumu sana ndugu zangu kuibadilisha dunia ila dunia ni rahisi sana kukubadilisha wewe, lakini jambo la kufurahi ni kwamba dunia haiwezi kukubadilisha bila mwenyewe kukubali, hivyo lengo la mhimu ni kubadilika mwenyewe, Vatcan sio wamiliki wa hii dunia, Alpha draconis hawatatengeneza maisha yako, Reptlians hawana mamlaka yeyote juu yako, Freemasons, Illuminat Rosscrucian, Skull & bones je hawa wote wana nini na wewe? Kwanini unapoteza nguvu zako kwao?

Wana jamvi mimi nimeona wakati unakuja, na saa imeshafika na ndio tunayo sasa ya kila mmoja wetu kuitambua kweli, kweli ambayo itakuweka huru, na hii kweli ndio itakuwa mwanga wako, nawe utakuwa nuru hapa ulimwenguni, na jambo la kuzingatia ni kuwa hii kweli haiuzwi wala haitolewi bure.

Huu si wakati tena wakushika vitu usivyovijua wala kuwa na uhakika nao, ila kweli ya kweli ipo ndani yako mwenyewe... je hamkusikia ya kwamba unabii hutoka ndani ya mtu mwenyewe? Maana humo ndimo kuliko na kweli yake. Huu ndio wakati wa kila mtu kujiunganisha na chanzo halisi kutoka ndani yako mwenyewe bali si kutoka nje...

Hapo ndipo utagundua uwezo na nguvu ulizonazo, hapo ndipo utagundua wewe ni nani na umetoka wapi na kwanini upo hapa duniani.

Najua itakuwa ni vigumu kueleweka maana lengo la mtumwa ni kuwa huru ila sio habari za kufikiri kuurithi ufalme. Na hapa duniani hakuna mtu yeyote aliyemfungwa, na kama ingekuwa hivyo basi watu wote tungekuwa wafungwa wenye hali sawa, je hizi tofauti zilizipo zinatokea wapi? Je nitakuwa nimekosea kusema hawa wanaotutoa kifungoni ndio waliotuweka? Je wanashindwa nini kumkamata na kumfunga yule anayetufunga? Na je kama ni kweli wanatoa watu vifungoni inakuwaje tena ufalme wao unazidi kuimalika siku hadi siku? (Hamtachelewa kusema nakufuru)

Ndugu zangu sisi tu huru, na hakuna mtu yeyote awezaye kutufunga zaidi ya sisi wenyewe, hakuna kiongozi yoyote wa dini wala mganga yeyote mwenye mamlaka juu yako isipokuwa wewe mwenyewe... na hakuna mtu yeyote awezaye kuifungua kweli iliyo ndani yako zaidi yako mwenyewe, ni wewe tu uliye na hizo funguo, je mpaka sasa hujatambua wale wa kutoka nje wanaosema kukufungua ndivyo huzidi kukufunga zaidi kwa kukuamrisha kipi ufanye na kipi usifanye, na hata wao ndio huamua ni jinsi gani wewe uishi?

Hii ndiyo kweli ambayo leo kwa ujasiri nimepata kuja kuishuhuduia mbele yenu, kwa sababu sasa umefika wakati wa kuamka... AMKA...AMKA...AMKA. sitaweza kukwambia hiyo kweli ni nini, na inatafutwaje maana ipo ndani yako wewe na wala sio kwangu... sitataka kuendeleza kukupa mafunzo ya uongo ili uipate hiyo kweli yako... ila cha kukusaidia ni wewe kufungua macho na ubongo wako na sasa jaribu kuangalia dunia yako katika kona tofauti...

Ni kwa njinsi hii tuliupenda ulimwengu... hivyo tupo hapa kwa dhamira zetu wenyewe... na hakuna yeyote anayepaswa kulaumiwa kwa chochote kile.

Msisahau ya kuwa hakuna kitu kinachotokea kwa bahati mbaya, kila unachokifanya kina matokeo yake yawe ni mabaya au mazuri.

TUENDELEE KUISHI KWA AMANI NA UPENDO!!
Huu ujumbe nilikua sijaupata lkn kadri nilivyozidu kusoma ndivyo nilianza kuelewa hongera na asante kwa ujumbe mzito
 
Back
Top Bottom