Je, ni kweli kuwa ulimwengu huu ni kifungo cha nafsi?

Na kuna ambao wanawaamini wasoma vitabu vya majini wanajifanya ni witchcraft intelligent humu JF kumbe fix
[emoji3] [emoji3] [emoji3]
Kitu kikubwa ni kujitambua, kujua wewe ni nani? Na ukishatambua kweli basi hutohitaji kutumia nguvu nyingi katika maswala yako, kwasababu tayari utakuwa unaijua kweli,
 
Dada nikupongeze sana kwa kuleta elimu hii ya utambuzi.
Ni kwanini watu wengi hushikilia mawazo yao hasa mawazo mabaya badala ya kushikilia mawazo mazuri?

Umeshawahi kuongea na nafsi yako kibinafsi? Umeshawahi kujaribu kuchunguza kinachoendelea akilini mwako? Mfano kuchunguza unawaza nini? Kuna wakati unakuta unawaza mawazo mabaya na unaweza ukajisemea mwenyewe "Acha kuwaza mawazo mabaya, hayana umuhimu" huku ukijiambia mwenyewe.Unaweza kuwa makini na mawazo yako na kujiuliza kama unavyouliza mtu mwingine au kuyachunguza kama unavyochunguza hali ya nje.

Kushindwa Kuwa makini na Jambo.
Tunaposhindwa kuelewa jambo kwa kina wengi hujikuta wanaweka fikra duni na kushikiliwa na mawazo hasi. Tunaposhindwa kuelewa hali iliyopo basi tunaweza kuzidi kutawaliwa na wasiwasi, hasira, ujinga woga n.k lakini tukielewa jambo au hali kwa uhalisia wa pande zote mbili yaani kwa upande unaotetea na upande unaopinga au kwa upande hasi na upande chanya tunaweza kufanya maamuzi sahihi na kutoshikiliwa na mawazo bila kujiongoza.

Badili wazo au Fikra mbaya kwa Kuipa Fikra nzuri/chanya kipaumbele.
Huwezi kuondoa mawazo au fikra mbaya kwa fikra mbaya bali vyote hivyo huondolewa kwa fikra nzuri. Mfano unapoona hasira inakutawala, ili kuiondoa hasira weka mtazamo wako kwenye upendo na hasira yenyewe itaondoka bila kipingamizi. Ibadili hasira kwa kutanguliza upendo na hasira yenyewe itaondoka kwani hakuna upendo unaokaa na hasira. Kama vile hakuna giza linalokaa na mwanga ndivyo hakuna mawazo au fikra mbaya inayoweza kukaa na fikra nzuri. Fikra nzuri huondoa fikra mbaya na mawazo mazuri huyaondoa mawazo mabaya.
Vivyo hivyo kinyume chake pia.

Ni vyema kujitawala kwa kinachoendelea akilini na kukishinda badala ya kukiruhusu kitoke katika ulimwengu wa nje. Na ndio maana wengi hujifunza meditation/taamuli kuweza kujizoesha kujitawala na kutawala hisia zao.

Mawazo huumba!
Unapokuwa unayapa kipaumbele mawazo mabaya au mazuri, basi yataumbika kwenye maisha yako. Yawe ya uongo au ya kweli, basi tegemea matokeo yake. Na matokeo hayo ni moja ya kazi ya ufahamu wako lakini wengine wanakuwa wanalalamika na kutupia lawama mara kwa shetani, mungu, binadam wenzao nk jambo ambalo sio.
Kuna matokeo ya mawazo yetu ya aina nyingi

Kuna matokeo ambayo hujitokeza ambayo ndio mabaya sana! Matokeo hayo ni yale yanayomuwekea mtu kizuizi cha kupokea ukweli.
Kuna mawazo mengine pia humfanya mtu kuwa huru kupokea ukweli muda wowote.

Wazo ni mbegu.
Unapopanda wazo na kulipalilia hugeuka neno na hatimae kitendo. Hivyo chunga sana ufahamu wako usijekutekwa na mawazo mabaya maana ndio yatakuwa maisha yako.

Kusema dunia ni kifungo cha nafsi sio kweli.
Tunaposema nafsi tunamaanisha mtu halisi/ufahamu au yule mtu wa ndani. Hivyo mtu huyo nafsi/binafsi aweza kujifunga mwenyewe kwa kujua au kwa kutokujua kwa mawazo yake mwenyewe. Nasema yake mwenyewe kwasababu hata akiyasikia kwa watu/mtu lazima kwanza yatapita kwenye ufahamu wake ndio achague kuyaamini au kwa kutokuyaamini.
Mfano unaambiwa kuna kiumbe anaeitwa shetani, wewe badala uchunguze, upime, na kuhoji, unayaamini moja kwa moja alafu hutaki kusikia zaidi ya hayo. [emoji30]UMEJIBLOCK.

Ishi ukiwa upo tayari kupokea ukweli muda wowote. Hapaswi kujifungia ndani ya sheria walizoweka watu fulani.sheria zao zipokee na uzichunguze... Je? Ni za kweli? Kama sio za kweli jiulize zina walau ukweli kidogo? Kama upo ukweli walau kidogo, uchukue uuishi huku ukijua siku zote ukweli unaendelea kuvumbuliwa.

Nimalizie kwa kusema kwamba hakuna mtu yoyote awezae kuufunga ufahamu wa mtu mwingine. Aweza kufunga ufahamu wake lakini sio wako.
Hata akikufundisha mafundisho gani! Ni hiyari yako kuyaamini au kuyakataa.
Aweza kuufunga mwili lakini sio nafsi. Nafsi yako wewe mwenyewe ndio waweza kuifunga na kuifungua au kuifunga na kuifunga zaidi.

Binadamu wenzako waweza kuufunga mwili wako lakini sio wewe halisi.
 
hiyo falsafa ni ya uongo kabisa tuliumbwa tukiwa wakamilifu katika kweli lakin tulipoingia kwenye giza tukapoteza ukamilifu lakin bado tuna dhamiri(kifungo cha ndani) mfano mzur watu wengi wanaoua mtu huwa naye anataka bado kumfuata aliyemuua hii ni tofauti na viumbe wengine wasio na dhamiri.Pia tunajua kumbukumbu hukaa kwenye ubongo na pia mtu anapokufa huoza na kumbukumbu hupotea Muhubir 9:5 mfu hawez kupenda, wala hateseki , hana hisia zozote.
 
mkuu unataka kufa nini,huu wosia aisee...
 
Asante sana kaka aretasludovick kwa mchango yakinifu ulioshiba maelezo.
Kwa hakika umeongea mambo ya msingi sana katika kujitambua
 
Hivi umeelewa nilichoandika au?
 
1:uongo wa hii falsafa ni nini?
2:NI KWELI ndugu tuliumbwa tukiwa wakamilifu, na swala la kuingia gizani si kweli tuliingia wote... labda ungesema uliingia wewe na baadhi ya unaowajua ulioingia nao, hilo linajidhihirisha katika mfano wako wa kuua kwamba si wote walio gizani ila ni wachache tu walioamua kuingia kwa mapenzi yao binafsi
3:upo sawa kusema ukamilifu bado tunao, nakupongeza kwa hilo hivo basi wakati wa kurudi kwenye chanzo chako halisi upo pia
4:kumbuka kinachokufa ni mwili tu bali ufahamu wako utaendelea kubaki hivyohivyo... je unaamini mungu ataweza kukuhukumu wakati ufahamu wako wote umepotea na huna kumbukumbu yoyote ile ya kile ulichofanya duniani... je hii huoni kama itakuwa uonevu?
#nategemea maswali zaidi kutoka kwako mpaka pale utakaporidhika...
 
Hawezi kulijibu kwasababu hakuna uongo mahala popote katika hilo bandiko
 
ww hujui nachoongelea ni nini kuingia gizani namahanisha ni kutenda dhambi ndio maana tunakufa kama upo kwenye mwanga ww utakuwa haufi na ni mkamilifu 100% na haukosei chochote kwa ufupi umekamilika kila kitu!!
je ni kweli ww ni mkamilifu, haufi, haukwazi mtu yeyote, hisia zako vp!!!
Dini nyingi zinafundisha uongo eti kwamba kumbukumbu hubaki mtu anapokufa ha uendelea kuhisi, kupenda na kuchukia je ni kweli Biblia inasema ivyo ukisoma

Kwa maana walio hai wanajua kwamba watakufa;+ lakini wafu, hawajui lolote kamwe,+ wala hawana malipo tena, kwa maana kumbukumbu lao limesahauliwa.+ 6 Pia, upendo wao na chuki yao na wivu wao tayari zimepotea, 10 Yote ambayo mkono wako unapata kufanya, yafanye kwa nguvu zako zote, kwa maana hakuna kazi, wala utungaji wala ujuzi wala hekima katika Kaburi, mahali unapokwenda.” *Mhubiri 9:5, 6 10.

Pia, upendo wao na chuki yao na wivu wao tayari zimepotea


zaburi 146:4
Roho yake hutoka,+ naye hurudi kwenye udongo wake;+
Siku hiyo mawazo yake hupotea.+

hiyo ni baadhi ya mistari michache tu

PAKUA KITABU HIKI UTAELEWA KUSUDI HASA LA MUNGU NA UTAMPENDA ZAIDI HAUTAMWONA MKATILI KAMA DINI ZA UWONGO ZINAVYOFUNDISHA
PAKUA HAPA
 
Hivi umeelewa nilichoandika au?
nimekuelewa sana falsafa yako ni kwamba kuna mwili na nafsi ambayo inaweza kutenganishwa na pia nafsi hutoka mtu anapokufa LAKINI HICHO KITU SI KWELI
 
nimekuelewa sana falsafa yako ni kwamba kuna mwili na nafsi ambayo inaweza kutenganishwa na pia nafsi hutoka mtu anapokufa LAKINI HICHO KITU SI KWELI
[emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15]
Kwani we unazungumzia uzi upi? Maana huu hauna uhusiano kabisa na maswala ya watu.....
Mi nimesisitiza watu kujua kweli tu, na kusisitiza kuwa kweli hiyo itawafanya wajitambue.
Wakati naandika pia nilijua kuwa kuna watu hamtaelewa hivyo it's alright
 
Siku nyingine ukiwa hujaelewa kitu uwe unauliza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…