Je, ni kweli kuwa Wayahudi walikuwa weusi?

Je, ni kweli kuwa Wayahudi walikuwa weusi?

MALCOM LUMUMBA

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2012
Posts
21,113
Reaction score
65,124
Wayahudi na Wapalestina ni watoto wa baba moja lakini mama tofauti. Baba yao ni mtu wa Ukaldayo ambako ndiyo Iraki ya sasa. Mtoto wa kwanza wa Abraham, Ishmael alikiwa na mama mwafrika aliyetokea nchi ya Misri au Kemet.

Sasa kuna ile nadharia ya kusema hawa Wayahudi wenye asili ya Ashkenazi siyo watoto wa Abrahamu bali ni wazungu wa Ulaya. Bila kusahau kwamba kuna Wayahudi wa kiserphadi ambao wao hawakuwahi kutoka nje ya Palestina.

Kuna msemo unaotumika na baadhi ya watu na kudai kwamba Raisi wa zamani wa Misri Gamal Abdi Nasser aliwahi kusema hivi kuhusu Wayahudi "You left here black but returned white, we cannot accept that" Sasa kama jamii hii ilikuwa ya watu weusi kwanini leo hii ndugu zao wapalestina wawe ni waarabu na hakuna watu weusi kabisa ndani ya jamii ile.

Tatizo ni nini hapa, naomba kueleweshwa ?
 
Kwa Kutumia Bibilia. Sipingi kuwepo kwa Wayahudi Weusi ila sioni kama wote walikuwa weusi.

Ile nchi hakuahidiwa kila mtu bali Watoto wa Ibrahimu Uzao wa Isaka, Aliyemzaa Yakobo. Ibra na Sara wote walitokea huko Ur hivyo ni kabila Moja. Isaka alipotaka Kuoa alirudishwa kwa Ndugu zake, Yakobo Pia. Hivyo michanganyiko ilianza hapo Baada ya watoto wq Yakobo.
Kama Ibrahimu alitokea Huko karibu na Iran na Iraq. Atakuwa alikuwa kama mwarabu flani au muajemi.
Kama Mke wa Ketura alikuwa Mmisri alikuwa ni Mweusi na Ibrahimu alizaa watoto weusi.
Musa Alimuoa Sipora ambaye Bibilia inasema alikuwa Mweusi, Hivyo Watoto wa Israel baadhi lazima wawe weusi.
Suleiman alioa wake 1000, miongoni mwao kwa mujibu wa masimulizi aliozwa watoto wa malkia wa Sheba, Hivyo lazima mbegu nyeusi iwepo.
Kwa Sababu Pia walienda utumwani Misri, Yusufu akapewa mke wa kimisri kuna uwezekano wa watu weusi kuzaliwa.

Kuna uwezekano kukawa na waisrael wa karibu race zote maana wamejichanganya tangu miaka ya zamani.
Mfano, Boazi alioa Ruth Mmoabu. watoto lazima wawe chotara.
Irani waliishi utumwani wayahudi.
Ulaya walisambaa kila kona enzi za uvamizi wa 70AD.
India Pia walifika.
Ethiopia Pia.
Kingine Pale ilipokuwa ni Highway ya Dunia. Carravan za watu wa kila taifa zilipita. Hivyo intermarriage waliokatwazwa nyingi zilifanyika.
Sishangai hata akitokea mchina akasema asili yake ni Uyahudi.

maoni
 
Mada moto hii nitarejea..... Elungata Mnabuduhe mitale na midimu Wick Mshana Jr mpite huku
Mada ni moto.. au inategemea nani kafungua mada.!

hakuna kisichowahi kujadiliwa humu

Mada kama hii ni moja ya mada za kivivu zinazochosha akili na zenye kujirudiarudia bila kupata muafaka

Hao mnaowazungumzia ni jamii ya watu iliyokuwa na utaratibu wa kupenda wake wengi

Hivyo wala usishangae baadae ukikurejelea na wewe pia kama myahudi halafu ukashangaa...![emoji1][emoji56]

Ni uhuni mtupu_kama mna mtaalamu wa kujua nani alimtia nani Mimba..uwanja wote utakuwa wenu..sie tutakuwa wasindikizaji tu..[emoji120]
 
Tunapoongelea suala la waisrael weusi,sijui kwanini watu husahau kuangalia fact za kihistory,
kwamba kuna kipindi Cush empire iliuangusha ufalme wa misri,
kipindi hicho Egypt empire ikitawala mpaka caanan au palestine ama israel ilipo leo,
ufalme wa cush uliokuwa na makao makuu Meroe,Sudan ya leo ,ulikuwa ni wa watu weusi,
baada ya Cush empire kuiangusha Egypt empire,wakushi walitawala mpaka huko caanan kwa miaka mamia,hata kuna baadhi ya mafarao wa misri ni weusi,kwa maana ya walikuwa wakush,
baadae tena ufalme wa cush ulisukumwa kutoka maeneo ya caanan,misri na kurudi kuwa kingdom ndogo maeneo ya sudan,lakini tayari walikuwa wameshaacha mazalia yao,Levant(caanan),
hiyo ni historic fact,ukifuata history ya Cush empire na egypt dynasty utaona naongea nini,
sio kweli kuwa wakazi wa caanan walikuwa weusi,
asili ya waisrael ni Jacob,ambaye mamake Rebeka alikuwa wa kabila la Aramaic la huko Aram ambayo ndio Syria ya leo,
isaac alirudi kuoa syria na pia hata jacob alirudi kuoa syria,
asili yawatu wa Syria,sio weusi,
kwahiyo haya madai sio kweli
 
Tunapoongelea suala la waisrael weusi,sijui kwanini watu husahau kuangalia fact za kihistory,
kwamba kuna kipindi Cush empire iliuangusha ufalme wa misri,
kipindi hicho Egypt empire ikitawala mpaka caanan au palestine ama israel ilipo leo,
ufalme wa cush uliokuwa na makao makuu Meroe,Sudan ya leo ,ulikuwa ni wa watu weusi,
baada ya Cush empire kuiangusha Egypt empire,wakushi walitawala mpaka huko caanan kwa miaka mamia,hata kuna baadhi ya mafarao wa misri ni weusi,kwa maana ya walikuwa wakush,
Naam, naam mkuu wangu umenena vyema.
Lakini sasa Mfalme Piankhi na jehuri yake yoote ya kukamata Misri ya chini na ya juu histora inatuambia hakufika sehemu zote maana wakina Mfalme Sargon wa Ashuru waliwazuia wasipandishe zaidi juu zaidi na wakaja kuvamia Misri na kuwafukuza kabisa wanubi. Mimi swali langu ni kwamba kama kulikuwa na muingiliano baina ya watu wa masharaki ya kati na Afrika kwanini leo hii watu weusi ni wa kutafutwa sana hapo mashariki ya kati ??
 
Mada ni moto.. au inategemea nani kafungua mada.!

hakuna kisichowahi kujadiliwa humu

Mada kama hii ni moja ya mada za kivivu zinazochosha akili na zenye kujirudiarudia bila kupata muafaka

Hao mnaowazungumzia ni jamii ya watu iliyokuwa na utaratibu wa kupenda wake wengi

Hivyo wala usishangae baadae ukikurejelea na wewe pia kama myahudi halafu ukashangaa...![emoji1][emoji56]

Ni uhuni mtupu_kama mna mtaalamu wa kujua nani alimtia nani Mimba..uwanja wote utakuwa wenu..sie tutakuwa wasindikizaji tu..[emoji120]

Tatizo la mtanzania, huwaga anaamini kwamba akisoma kitu mara moja basi ameshamaliza kabisa. Hili ni moja ya tatizo nililoliona tangu nafundisha chuo kikuu kwamba mwanafunzi au mwalimu akifahamu kitu huwa anakuwa hana haja ya kukigusa wala kukipitia tena, anaamini kwamba ashakuwa Guru. And this is a reason Education Quality in the country is abysmally low than ever before.

Halafu umeongea hoja mufulisi sana, swala la wake wengi limekuwepo tokea kipindi cha The Mayans, The Aztecs, The Greeks, The Achaemenids to the Mongols. Hata huku Afrika wakina Mkwawa na Mnyigumba waliona wake wengi. Tabia ya kuwa na mke moja ilienezwa na umisheni wa mtume Paulo na kukufikia wewe mwafrika kwa kupitia meli za Vasco Da Gama na Karl Peters.

Mfalme Charlemagne alikuwa na watoto wengi mno lakini leo hii bado wanafahamika na kila Raisi wa Marekani na Mfalme wa Ulaya ana damu yake. Au Chingis Khan katika harakati za kuzaa tunaambiwa katika wachina 10 basi hukosi watu wanne wenye damu yake.

Sasa hao unaosema wewe walikuwa na hulka ya kuoa sana mbona leo hatuoni chembe chembe za vizazi vyao huko mashariki ya kati au hapa Afrika ? Vizazi vya wafalme wa nubia vipo mpaka leo hii na wanafahamika kuanzia Sudan, Somalia na Ethiopia. Hii hoja yako hii, inabidi uipitie tena kwa taratiibu.
 
Kuna uwezekano kukawa na waisrael wa karibu race zote maana wamejichanganya tangu miaka ya zamani.
Mfano, Boazi alioa Ruth Mmoabu. watoto lazima wawe chotara.
Irani waliishi utumwani wayahudi.
Ulaya walisambaa kila kona enzi za uvamizi wa 70AD.
India Pia walifika.
Ethiopia Pia.

Naogopa sana kutumia vitabu vya kidini kama vyanzo vya kihistoria. Lakini kwakuwa umechangia basi naomba nikujibu kwa kupitia hivyohivyo The Book Of Jubilees (The Book of Divisions) kinachozungumzia jinsi ambavyo Nuhu aliigawa dunia kwa wana wake ukisoma vizuri na ramani zake utaona matatizo yalipoanza.

Japheti, Shem na Ham walikutana na kuchagua kugawana dunia kwa vizazi vyao na baadae wakampeleka baba yao Nuhu hayo mapendekezo ambayo yeye kama mzazi aliyapitisha na kuongezea baadhi ya vitu. Alimpa Japheti eneo la Ulaya kuanzia kwenye ncha ya kaskazini ya dunia kuelekea mashariki, hapa ni ulaya yote. Alimpa Shem Asia maeneo ya mashariki ya kati na Asia. Ham alipewana maeneo ya bara la Afrika na Marekani kusini.

Tatizo lilikuja pale ambapo Kanaani alikataa kwenda Afrika kwenye eneo ambalo alipewa na babu yake na kuamua kubaki kwenye eneo lisilo lake. Ukisoma Jubilee 10:30-32 inaonyesha jinsi ambavyo Ham, Kushi na Mizarhimu walikuwa wanamkemea. Yeye bado akapinga na kukataa kuondoka, wakamlaani wakisema kwasababu umekaa kwenye ardhi isiyo ya kwako ulaaniwe wewe na vizazi vyako, vitaanguka na kufa vibaya katika hilo eneo. Wakaanani yaliwakuta kweli na walifutiliwa mbali na wahebrania.

Sasa mimi ninachouliza ni hiki tena:
Kwanini hivi vizazi vipotee tu kirahisi wakati huko Marekani kusini ushahidi wa weusi upo mkubwa ??
Hapo Mashariki ya kati kwa wana wa Ibrahimu wa kipalestina ambao baba yao Ishmaili alizaa sana na wanawake wuesi wa kikaanani na kuchanganya nao damu hadi leo hii ni kimetokea hao weusi hawapo ?
 
Wayahudi na Wapalestina ni watoto wa baba moja lakini mama tofauti. Baba yao ni mtu wa Ukaldayo ambako ndiyo Iraki ya sasa. Mtoto wa kwanza wa Abraham, Ishmael alikiwa na mama mwafrika aliyetokea nchi ya Misri au Kemet.

Sasa kuna ile nadharia ya kusema hawa Wayahudi wenye asili ya Ashkenazi siyo watoto wa Abrahamu bali ni wazungu wa Ulaya. Bila kusahau kwamba kuna Wayahudi wa kiserphadi ambao wao hawakuwahi kutoka nje ya Palestina.

Kuna msemo unaotumika na baadhi ya watu na kudai kwamba Raisi wa zamani wa Misri Gamal Abdi Nasser aliwahi kusema hivi kuhusu Wayahudi "You left here black but returned white, we cannot accept that" Sasa kama jamii hii ilikuwa ya watu weusi kwanini leo hii ndugu zao wapalestina wawe ni waarabu na hakuna watu weusi kabisa ndani ya jamii ile.

Tatizo ni nini hapa, naomba kueleweshwa ?
Mkuu hii topic ni sensitive kidogo maana kuna misinterpretation kibao mfano utakuta wanaosupport Israel wanaona waarab ni kama mashetani bila kufahamu mke wa yakobo yaani ISRAEL mwenyewe alioa muarabu kutoka Syria hivyo ikimaanisha Waisrael wote original wana damu ya waarabu pia!!!

Kingine Yakobo alizaa na Zilpah na Bilhah ambao walikuwa ni watumwa na walikombolewa na laban ambaye ndiye baba wa wake wawili wa yakobo yaani Rachel na Leah.

Hivyo hoja ya wayahudi kuwa weusi inapitia kwa Bilhah na zilpah ambao walikuwa ni watumwa weusi possibly wacush ama khemet ambao ndio walizaa watoto 4 wa yakobo yaani Gad,Dan,Asher,Naphtali hivyo hapa lazima kuna damu ya weusi kwenye race ya Israel.

Kuhusu Ismael naye alioa mwanamke kutoka Misri hivyo probability alikuwa mweusi ila kuhusu descendants kutokuwa wote weusi nafikiri ni intermarriage maana kama mtu mweusi umezungukwa na nchi za weupe probability ni kwamba utazaa na weupe hivyo with time asili yako inapotea sawa sawa tu wayahudi wanaoona waarabu kama maadui ila wanasahau mama yao alikuwa muarab pure!!

Anyway maadam makabila 10 yaliyopotea na hayo manne ya weusi basi huenda yako huku uzaramoni maybe!!
 
,
sio kweli kuwa wakazi wa caanan walikuwa weusi,
Canaan ilikaliwa na watoto wa HAM ambao kimahesabu walikuwa weusi tii ingawa waliongea semitic language..... Baada ya wayahudi kuichukua ardhi ya Canaan bado waliishi na hao wacanaan huko Jabbok,Amman,Gaza n.k hivyo probability ya kuwepo watu weusi Canaan kipindi cha Yakobo bado ni kubwa mkuu

,
asili ya waisrael ni Jacob,ambaye mamake Rebeka alikuwa wa kabila la Aramaic la huko Aram ambayo ndio Syria ya leo,
isaac alirudi kuoa syria na pia hata jacob alirudi kuoa syria,
asili yawatu wa Syria,sio weusi,

kwahiyo haya madai sio kweli
Uko sahihi Mkuu lakini kuna fact moja unairuka kuwa Yakobo alikuwa na wake wawili ila alizaa na wanawake 4 na wawili kati yao walikuwa watumwa kutoka afrika waliokombolewa na laban na waliishi naye alipoondoka na wake zake kurudi canaan..... Hivyo kama walikuwa weusi hao watumwa probability ni kwamba wale watoto 4 walikuwa weusi hivyo hoja ya kwamba kuna wayahudi weusi inapata mashiko hapo tokea hapo.
 
Mkuu hii topic ni sensitive kidogo maana kuna misinterpretation kibao mfano utakuta wanaosupport Israel wanaona waarab ni kama mashetani bila kufahamu mke wa yakobo yaani ISRAEL mwenyewe alioa muarabu kutoka Syria hivyo ikimaanisha Waisrael wote original wana damu ya waarabu pia!!!

Mkuu Zitto Jr,
Suala siyo kuunga mkono Wayahudi wala Wapalestina, suala ni kwamba ukweli ni upi ?? Hivi umewahi kujiuliza swali hili : Kama Wayahudi wenyewe ambao inadaiwa ni weusi wakarudi pale Israel ambako leo hii panakaliwa na Waarabu unadhani hao waarabu watawapokea kirahisi ???
 
Hawawezi kuwakubali mkuu maana kama hao waisrael (Judea) wenyewe tokea enzi waliwabagua wenzao wa samaria (kingdom of Israel) kisa walichangamana damu na makabila ya nchi jirani ndio sembuse waone ngozi nyeusi inajiita myahudi!!! Hapo lazima watawakataa ama kuwabagua kma walivyofanya kwa wale waethiopia wanaoishi Israel hadi kufanyiwa vitendo vya ubaguzi na kutimuliwa nchini humo licha ya connection kubwa ya Kush na Israel huko nyuma kiasi hadi walizaliana!!!

PS: Hivi mkuu kwanini waisrael hawaitwi waarabu ilihali wote ni semites wa middle East kama wenzao wa jordan ama palestine!!
 
😀😀😀😀.. kweli hii mada moto.. kabla hatujaenda mbali.. hebu tuangalie waarabu wa asili ni kina nani? Picha (Bani Rasheed people (Rashaida) - Camel herders at the Riyadh Camel market.) Albino wao huwaita slave decendants watu weusi wote walio nje ya bara la Africa.
 
Attachments

  • Rashaida_1.jpg
    Rashaida_1.jpg
    51.9 KB · Views: 154
Hawawezi kuwakubali mkuu maana kama hao waisrael (Judea) wenyewe tokea enzi waliwabagua wenzao wa samaria (kingdom of Israel) kisa walichangamana damu na makabila ya nchi jirani ndio sembuse waone ngozi nyeusi inajiita myahudi!!! Hapo lazima watawakataa ama kuwabagua kma walivyofanya kwa wale waethiopia wanaoishi Israel hadi kufanyiwa vitendo vya ubaguzi na kutimuliwa nchini humo licha ya connection kubwa ya Kush na Israel huko nyuma kiasi hadi walizaliana!!!

PS: Hivi mkuu kwanini waisrael hawaitwi waarabu ilihali wote ni semites wa middle East kama wenzao wa jordan ama palestine!!
Nakusoma vyema kiongozi. Lakini sasa:
Kama wayahudi asilia leo hii wakisema wanarudi kwenye nchi yao ya ahadi watakuwa wanafanya makosa ?
Zaidi ya kutumia sheria za kimataifa kuwazuia wasikae pale unahisi dini (historia) hazitakuwa upande wao ?

Maana kama hawa wakina Netanyahu siyo wayahudi asilia na wayahudi asilia wapo unadhani huko mbeleni hawatataka kurudi kwenye nchi yao ya ahadi ??? Wakitaka kurudi dunia nzima itawakubalia ??

Naomba kujua msimamo wako katika hili.......
 
😀😀😀😀.. kweli hii mada moto.. kabla hatujaenda mbali.. hebu tuangalie waarabu wa asili ni kina nani? Picha (Bani Rasheed people (Rashaida) - Camel herders at the Riyadh Camel market.) Albino wao huwaita slave decendants watu weusi wote walio nje ya bara la Africa.

Hapa sijakuelewa kidogo mkuu wangu naomba utolee maelezo zaidi.

Naongeza picha.. hao mnaoita waarabu wa siku hizi ni mullatos (chotara) wa waturuki/albino na weusi
For the love of God, hii picha ya pili aisee!
Ni ya karne ya ngapi ?? huyo afisa ni wa Ujerumani au Uturuki ??
 
Hakuna Biblia inayosema kuna wayahudi weusi na maana halisi ya neno myahudi ni mtu wa kabila la Yuda alikotokea Daudi na Kristo. Neno Israeli Lina maanisha makabila yote 12 ikiwemo Yuda!
 
Wayahudi na Wapalestina ni watoto wa baba moja lakini mama tofauti. Baba yao ni mtu wa Ukaldayo ambako ndiyo Iraki ya sasa. Mtoto wa kwanza wa Abraham, Ishmael alikiwa na mama mwafrika aliyetokea nchi ya Misri au Kemet.

Sasa kuna ile nadharia ya kusema hawa Wayahudi wenye asili ya Ashkenazi siyo watoto wa Abrahamu bali ni wazungu wa Ulaya. Bila kusahau kwamba kuna Wayahudi wa kiserphadi ambao wao hawakuwahi kutoka nje ya Palestina.

Kuna msemo unaotumika na baadhi ya watu na kudai kwamba Raisi wa zamani wa Misri Gamal Abdi Nasser aliwahi kusema hivi kuhusu Wayahudi "You left here black but returned white, we cannot accept that" Sasa kama jamii hii ilikuwa ya watu weusi kwanini leo hii ndugu zao wapalestina wawe ni waarabu na hakuna watu weusi kabisa ndani ya jamii ile.

Tatizo ni nini hapa, naomba kueleweshwa ?
mkuu unaweza kutoa vyanzo vya kihistoria vinavyokubaliana na haya ukiacha para ya mwisho.
maana naona kama ni maelezo kutoka kwenye vyanzo vya kiimani.
 
Yusufu Hakuwa uzao WA kabila la Yuda (yeye kazalisha makabila mawili, Manase na Efraimu) na hadi ninapoandika sasa ni kabila moja tu la Yuda (Wayahudi ndio wapo nchi Ya Israeli) makabila mengine 10 yatarudishwa na Mungu wenyewe siku za mwisho na kuwaunganisha na Yuda kama ilivyokuwa wakati wa wafalme Sauli, Daudi na Solomon!
 
Back
Top Bottom