Wayahudi na Wapalestina ni watoto wa baba moja lakini mama tofauti. Baba yao ni mtu wa Ukaldayo ambako ndiyo Iraki ya sasa. Mtoto wa kwanza wa Abraham, Ishmael alikiwa na mama mwafrika aliyetokea nchi ya Misri au Kemet.
Sasa kuna ile nadharia ya kusema hawa Wayahudi wenye asili ya Ashkenazi siyo watoto wa Abrahamu bali ni wazungu wa Ulaya. Bila kusahau kwamba kuna Wayahudi wa kiserphadi ambao wao hawakuwahi kutoka nje ya Palestina.
Kuna msemo unaotumika na baadhi ya watu na kudai kwamba Raisi wa zamani wa Misri Gamal Abdi Nasser aliwahi kusema hivi kuhusu Wayahudi "You left here black but returned white, we cannot accept that" Sasa kama jamii hii ilikuwa ya watu weusi kwanini leo hii ndugu zao wapalestina wawe ni waarabu na hakuna watu weusi kabisa ndani ya jamii ile.
Tatizo ni nini hapa, naomba kueleweshwa ?
Naomba nirejee maelezo yako hapa ambayo ndio msingi wa swali - Ni kweli Gamal Abder Nasser alipoulizwa kipindi cha vita kati ya Misri na Israel kuhusu Amani mashariki ya kati hasa Wayahudi kuishi kwa Amani katika nchi ya Israel - Jamaa alijibu hivi "
The Jews will never be able to live here in peace ,because they left here black but come back white"
Hapo hapo tuulize swali moja Je? Wayahudi kwa asili yao(race) - Wanahistoria wanakubaliana Wayahudi ni Semitic; Na neno hili linapotumika halijumuishi rangi ya ngozi isipokuwa linajumuisha Lugha zenye asili ya Kiafrika na asia.
Tukirejea mateso ya Wayahudi kipindi cha Utawala wa Manazi wakiongozwa na Hitler waliwasaka wayahudi kila kona ya Ulaya na Waliwajua kwa Nywele zao na pua,vernier caliper zilitumika kupima ukubwa wa pua ili kujua iwapo mtu huyo ni Mjerumani(Aryan) au Myahudi.Hii ikaja kujulikana kama Antisemitism.
Hivyo kwa asili ya neno semitic hatupati rangi ya Myahudi kwa asili bali tunapata phenotype yao ya Nywele na maumbile mengine ya nje pamoja na mfanano wa lugha yake ambayo inafanana sana na kiarabu na lugha baadhi za kiafrika kama vile maeneo ya ethiopia na misri.
Bruce Britten mmissionari swaziland anadai kuwa Myahudi original(Kutokana na utafiti wake) sio mweusi wala sio Mweupe! Yaani wale wayahudi waliobaki palestina baada ya 70 AD! Ni Dark Brown- Weupe na Waeusi wa wayahudi tunaowaona leo ni wale waliokwenda kaskazini wa dunia wakawa weupe na wale waliokwenda kusini wakawa weusi.
Katika Historia ya biblia Sijui kwanini Mjadala huu haupo! hakuna mkazo wa dhati juu ya rangi ya mtu isipokuwa mkazo ulikuwa juu ya Makabila na Mataifa yaliyowazunguka wayahudi( Myebusi,Mhivi,Mhiti,mfilisti na nk).
Katika Biblia kuna maeneo machache sana yanayoongelea rangi ya ngozi ya mtu.Hii inawezekana kabisa walibagua makabila sio rangi kwa sababu kama wangelibagua rangi walikuwa wanashabihiana sana na ingekuwa vigumu kudumisha huo ubaguzi! Mfano; Mzaramo na Mhehe! wote wanafanana sana kwa rangi na ngozi lakini wao wanajuana kuwa yule mhehe na yule ni mzaramo.
Wimbo ulio bora 1:5 - 6
Mimi ni mweusi mweusi, lakini napendeza, Enyi binti za Yerusalemu, Mfano wa hema za Kedari, Kama mapazia yake Sulemani. Msinichunguze kwa kuwa ni mweusi mweusi, Kwa sababu jua limeniunguza. Wana wa mamangu walinikasirikia, Waliniweka niwe mlinzi wa mashamba ya mizabibu; Bali shamba langu mwenyewe sikulilinda.
Lakini pia tunaona ulikuwepo Ubaguzi wa waziwazi iwapo myahudi alichangamana na watu wasio wa taifa lake,kwa kuoa au kukubali kuishi nao ilileta shida sana.
Hesabu 12:1
Kisha Miriamu na Haruni wakamnenea Musa kwa sababu ya mwanamke Mkushi aliyekuwa amemwoa; maana, alikuwa amemwoa mwanamke Mkushi.
Hivyo basi Myahudi kwa asili yake kabla ya Kuchangamana hasa kwenda Ulaya na Asia
1. Alifanana sana na waarabu kwa rangi na maumbile ya mwili
2.Myahudi hawezi kuwa mweupe kama Trump kulingana na sababu za kijiografia.
Myahudi wa Asilia,Sio Mweusi wala Mweupe! Jiografia inakataa Myahudi kuwa Mweupe! Na jiografia ni sayansi.
Wayahudi yaani kizazi cha Ancient Levant walikuwa na ngozi ngumu yenye Melanin yakutosha kuwasaidia kuhumili Jua kali la Maeneo hayo ya israel ya Leo.
Asante.
Courtesy :https://www.quora.com/Were-the-original-Jews-black