Naogopa sana kutumia vitabu vya kidini kama vyanzo vya kihistoria. Lakini kwakuwa umechangia basi naomba nikujibu kwa kupitia hivyohivyo The Book Of Jubilees (The Book of Divisions) kinachozungumzia jinsi ambavyo Nuhu aliigawa dunia kwa wana wake ukisoma vizuri na ramani zake utaona matatizo yalipoanza.
Japheti, Shem na Ham walikutana na kuchagua kugawana dunia kwa vizazi vyao na baadae wakampeleka baba yao Nuhu hayo mapendekezo ambayo yeye kama mzazi aliyapitisha na kuongezea baadhi ya vitu. Alimpa Japheti eneo la Ulaya kuanzia kwenye ncha ya kaskazini ya dunia kuelekea mashariki, hapa ni ulaya yote. Alimpa Shem Asia maeneo ya mashariki ya kati na Asia. Ham alipewana maeneo ya bara la Afrika na Marekani kusini.
Tatizo lilikuja pale ambapo Kanaani alikataa kwenda Afrika kwenye eneo ambalo alipewa na babu yake na kuamua kubaki kwenye eneo lisilo lake. Ukisoma Jubilee 10:30-32 inaonyesha jinsi ambavyo Ham, Kushi na Mizarhimu walikuwa wanamkemea. Yeye bado akapinga na kukataa kuondoka, wakamlaani wakisema kwasababu umekaa kwenye ardhi isiyo ya kwako ulaaniwe wewe na vizazi vyako, vitaanguka na kufa vibaya katika hilo eneo. Wakaanani yaliwakuta kweli na walifutiliwa mbali na wahebrania.
Sasa mimi ninachouliza ni hiki tena:
Kwanini hivi vizazi vipotee tu kirahisi wakati huko Marekani kusini ushahidi wa weusi upo mkubwa ??
Hapo Mashariki ya kati kwa wana wa Ibrahimu wa kipalestina ambao baba yao Ishmaili alizaa sana na wanawake wuesi wa kikaanani na kuchanganya nao damu hadi leo hii ni kimetokea hao weusi hawapo ?