Je, ni kweli kwamba vyakula vya mbegu vya GMO viko kwa ajili ya kuua kizazi cha watu weusi?

Je, ni kweli kwamba vyakula vya mbegu vya GMO viko kwa ajili ya kuua kizazi cha watu weusi?

Katika miaka ya hivi karibuni Watanzania tumekua tukisikia kuhusu swala la kuwekeza katika kilimo ambacho wanasiasa wanakiita "KILIMO CHA KISASA" ambacho kinahusisha utumiaji wa mbegu ambazo ni Genetically Modified. Lakini ni nini hasa maana ya GMO?, Je ni salama kwa kula?.

GMO ni aina ya mbegu na mimea ambayo imebadilishwa vinasaba (genes) katika maabara ili kuboresha aina fulani ya traits au tabia inayohitajika, kwa mfano kuongeza virutubisho, na kuongeza uwezo wa kujikinga na madawa.

Marekani ndio inaongoza kwa utengenezaji wa aina hii ya mbegu zikizambazwa na makampuni kama Monsanto, Syngenta AG, na DOW Chemicals ambazo nyingi tumekua tukiziona nchini. Hatari zitokanazo na aina hii ya mimea ni nyingi kuliko faida, na nchi nyingi duniani tayari zimezuia matumizi ya aina hii ya mbegu ikiwemo Canada, Argentina, Australia, India na Mexico na msimamo wa EU Ukiwa "Zuia GMO".

Nilibahatika kukaa na msomi mmoja wa Chuo Kikuu Cha elimu ya juu cha Nelson Mandela na akanitajia baadhi tu ya athari nyingi zikiwemo; Kuharibu mfumo wa ikolojia, kuharibu ama kubadilisha kabisa virutubisho katika mimea, Kansa, kuharibu rutuba ya ardhi na kusababisha wakulima kua tegemezi wa madawa ya kilimo, kujitokeza kwa magugu ambayo yanajikinga na madawa ya kuua magugu, na hasara kwa wakulima kutokana na ununuzi wa kiasi kikubwa cha madawa.

Faida chache alizonitajia ni pamoja na ongezeko la mimea inatojikinga na wadudu na magonjwa, kuongezeka kwa food supply, na kua na mimea inayostahimili ukame. Pia aliniambia "Hakuna Mwanasayansi duniani ambaye yuko serious atakayetoa support kwa GMO, UNLESS yuko katika payroll ya hayo makampuni", kwa sababu kiuhalisia, ni makampuni ya Biotech ambao ndio watengenezaji na wasambazaji watakaonufaika kutokana na mauzo ya mbegu na madawa!

Swali la kujiuliza; Je ni Watanzania wangapi wanazijua athari zitokanazo na GMO's?, au wengi wetu tumeangalia faida za kiuchumi kuliko athari za kimaziangira na kiafya?. TUAMKE NDUGU ZANGU
Huyo msomi wa nelson mandela hapo arusha kuna vitu amekupotosha

Na hakuna tafiti alifanya zaidi ya kusoma mitandaoni...

Kwa kukusaidia, fika halmashauri moja ktk mkoa wa mwanza inayo lima pamba kwa wingi...

Waulize watakusaidia kukujibu maswali yako kuliko huyo msomi aliye kuaminisha

Nakusaidia kwa hawa ambao walifika site na kushuhudia vinavyo endelea na tafiti zinazo fanyika na zilozo fanyika
 
Za chini kabisa ya kapeti ni kwamba hata sisi binadamu ni GMO! Unaambiwa mwanzo tulikua masokwe tu porini, wajanja wakaja wakatu injinia na kutubadilisha ndio tukawa hivi. Yaani unavyoona parachichi halina mbegu na sisi ndio ivyo ivyo tulifanyiwa tukapoteza manyoya, mikia nk. Ndio maana kila siku mnajiuliza kwanini masokwe ya sasa hayabadiliki yawe watu jibu ndio hilo apo.
Changanya na zako.
 
Kwa nini masikini wanapanda daladala wanajazana wakati matajiri wanatembea katika magari yao binafsi ?
Jiulize kwanini GMO produtcs bei iko chini kuliko zile organic? Lazima tuanzie hapo na kwa nini GMO products hula maskini wakati zile Organic wanataka wale matajiri au wenye uwezo na sina hakika kama mwanasiasa anayehubiri ule GMO products kama yeye anazitumia na nakumbuka serikali yetu ilipinga na kusema mbegu zetu tutazalisha wenyewe kama sijasahau
 
Kaka tafiti ina pingwa na tafiti, hakuna wanasayansi walio fnya tafiti na kuona tatizo lilipo

Na hayo makampuni yana karibisha watu kufanya tafiti na wana kulipa pesa ufanye tafiti kuhusu gmo na hata kwenye maabara zao wana kukaribisha

Na baadhi kutoka tanzania wameenda ktk hayo mashamba yao na maabara zao

Kama una lia wana lipwa na ushahidi unao weka wazi jamii ijue na sio kusema zina madhara lakini hakuna tafiti iliyofanyika kuona madhara yalipo
Dunia inaongozwa na uwongo, ukweli unafichwa sana na hautakiwi kujulikana
 
Back
Top Bottom