POTOSHI Je, ni kweli Lema amesema tuwachangie CHADEMA ili viongozi wanywe bia?

POTOSHI Je, ni kweli Lema amesema tuwachangie CHADEMA ili viongozi wanywe bia?

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1


1781248005772.png
 
Tunachokijua
Madai

Kumekuwapo na video inayosambazwa mtandaoni ikimuonesha mjumbe wa kamati kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) akidaiwa kuwataka wafuasi wa chama hicho kuchangia ili viongozi wanywe bia.


Je, ni upi uhalisia wa video hiyo?

Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck umejiridhisha kuwa video imepotoshwa kwa kukata na kuunganisha vipande visivyohusiana hivyo kutengeneza maana tofauti na ile ilyopo kwenye video halisi.

Kupitia Reverse image search JamiiCheck imebaini video halisi ambapo Lema alieleza kuwa CHADEMA haipokei ruzuku yoyote kutoka serikalini kwa sasa, hivyo viongozi wanatumia nguvu na gharama zao wenyewe kuzunguka nchi nzima. Wanaomba michango hiyo ya "Toni kwa Toni" ili kupata fedha za uendeshaji zitakazowawezesha viongozi kusafiri maeneo mbalimbali kwa ajili ya kujenga chama na kueneza demokrasia.

"Hapa tumefika kwa gharama zetu. Mimi nchi hii nikiizunguka ni gharama zetu na msaada wa marafiki, na wenyewe wanachoka wakati mwingine. Huwezi kumwomba mtu mara kwa mara nini? Mafuta, mafuta, mafuta. Kwa hiyo gharama ni kubwa sana...

Kila mwezi tutumie pesa sasa hivi ukiwa unakunywa bia tutumie pesa.

Zamani tulikuwa tunapokea ruzuku, sasa hivi hatuna ruzuku hata shilingi moja. Ukiona viongozi wanatembea barabarani ni tunatumia nguvu zetu wenyewe. Tunaomba msaada wenu, msaada wa chama chenu...

Tuma pesa sasa hivi itaingia. Mshirikishe rafiki yako kwenye kundi la WhatsApp, mshirikishe jirani yako, mshirikishe mchumba, ni boyfriend na mume wako. Tunaomba sana uweze kutusaidia ili viongozi wetu waweze kutembea sehemu mbalimbali kwa ajili ya kujenga chama na kujenga demokrasia." - Lema alisema
​
Inahitaji akili ya uwendawazimu kuamini hii, kwamba ww huoni video imeungwaungwa ili kutengeneza story, au ili mradi uanzishe mada?
 
Akili za kimbavu sana hizi,hata mtoto wa darasa la kwanza anaweza tambua kuwa huu ni upuuzi.

Au wewe lengo lako ni kumfurahisha Samia tu!?
 
Back
Top Bottom