carnage21
JF-Expert Member
- Jan 24, 2023
- 591
- 1,382
Kwa Ujumla jibu ni HAPANA.
Namna ya ushangiliaji wa Mashujaa FC umekua ukihusishwa na imani za uchawi jambo ambalo kiuhalisia siyo kweli bali ni namna ya kujitofautisha na ushangiliaji wa Mashabiki wa timu nyingine.
Tuanzie kwenye logo ya Mashujaa FC ukiiangalia ni logo inayotambulisha Mnyamapoli ambaye ni wa asili, Hapo kwenye "ASILI" ndipo na ushangiliaji wa mashujaa FC ulipoanzia na hatimaye Mashabiki wa mashujaa kuja na ushangiliaji wao wa kipekee ukiwahusisha watu waliobeba zana za jadi na kuvalia kijadi au kiasili.
Namna ya uvaaji wa nguo hiyo nyekundu inaitwa "Lubega" kwa Kiha. Hiyo ndiyo namna ya asili ya uvaaji ya watu wa kigoma "Waha" kama ilivyo kwa wamasai.
Chungu na mapambo yake ikiwemo kioo ni namna ya kunogesha tu mwonekano na wala siyo kwamba kimebeba uchawi ndani yake.