Nchi yetu kutoka kwenye umasikini bado tuna kazi kubwa sana yaani, nadhani ccm ifike hatua sasa iache dharau, ifikirie zaidi future ya nchi kuliko kuendekeza uchama, sasa mtu hajawahi kufanya jambo lolote remarkable eti awe rais, awe kiongozi, huaga mnategemea nini? Kwamba tu, Yes tumefanya uchaguzi wa rais? Kama ni kweli Mkapa alimpendekeza Magufuli kua rais and wale waliomtaka Lowassa kua mgombea na akakatwa then (kwa mtazamo wangu ) hao ndio walikua wazalendo halisi wa nchi hi, both Magufuli na Lowassa kuna vitu wamewahi kuvifanya na vikaoneka wakiwa mawaziri; huyu Amina kawahi kufanya nini? Rose Migiro or Bernard Membe same, nini wamewahi kufanya ambacho kimeweka historia kwa Tanzania? Binafsi sina kumbukumbu. Nadhani tumchague mtu kwasababu ya SIFA, kwamba huyu anaweza kututoa hapa na kutufikisha pale, sio kwasababu ni mzuri wa sura au mpole au mkali or hana makundi; havitusaidii hivo, ndio sasa unakua na rais ambaye hata yeye hajui kwanini Tanzania ni masikini.