Je ni kweli miwa inayooteshwa pembeni ya bafu ina madhara yoyote?

Mbona unatumia ndomu ambayo hauhoji kama imetengenezwa na nini sembuse miwa?
 
ndo ina virutubisho vya kutosha.ushawai kule tembele la nyuma ya choo ni tamu sana tena ndio limekuza vijana shupavu uswahilini
 
Case Closed...Sio Salama kama hujui unachokifanya
 
Miwa ya bafuni au sehemu yenye mbolea nyingi huwa na chumvi na sio mitamu kivile, kuhusu madhara sina hakika labda mtaalamu atujuze
 
Wasukuma utawajua tu.
Bafuni siyo mahali pa kukojoa

Sent from my SM-G970U using JamiiForums mobile app
 
Unajua samaki wanakula nini? Ukiachana na hao kambale.
Kuna mizoga ya wanyama,vinyesi nk.


Sent from my SM-G970U using JamiiForums mobile app
 
Hakuna madhara, mimea huchukua maji na chumvi chumvi za madini ili kujitengenezea chakula ambacho ndiyo hiyo sukari ya muwa uliokula. Kua na amani. Mwambie anikatie na mimi muwa !! Ulishamuona nyuki akiokoteza viambata vya kutengenezea asali ?!

Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Mimi kwangu Maji ya Bafuni nimeyaelekeza kwenye Migomba na miti Mingineyo kwenye Bustani.. Tunafurahia Ndizi na matunda mbalimbali hata Kiangazi.

Usiogope mizizi Inachuja Uchafu na kutumia maji safi kutengeneza Chakula Chake.. muhimu kusafisha kabala ya kutumia isijekuwa imerukiwa na vijidudu au Wadudu watambaao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…