Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 6,238
- 8,194
Kuna watu wanaosema kwamba Mungu alishusha Torati, Zaburi na Injili lakini wanadamu wakavichezea na kuvipotosha vitabu hivyo. Kwa sababu hiyo ikabidi Mungu ashushe kitabu kingine baadaye, ili kusahihisha maandiko yaliyovurugwa!
Kama ni hivyo, Covax na wenzako, naomba mnisaidie kujibu maswali haya kwa hoja nzito:
Je, kweli Mungu mwenye enzi na uweza wote, asiye na upungufu wala kosa, angeweza kushindwa kulilinda Neno lake alilolishusha mwanzoni?
Tunaamini kuwa Mungu ni Mkuu, mwenye hekima isiyo na mwisho, na anayetawala historia ya mwanadamu, kwa nini basi aliruhusu maandiko yake matakatifu yapotoshwe kabisa? Na je, alipoona yamepotoshwa, kwa nini hakuyafanyia masahihisho wakati huo huo? Kwanini alisubiri karne zipite, ndiyo alete “masahihisho”?
Na kama kweli alihitaji “kusahihisha” yaliyodaiwa kupotoshwa, kwa nini afanye hivyo kwa kuleta masahihisho hayo kidogo kidogo kwa kipindi cha miaka 23? Je, Mungu huyo huyo ambaye alisema “na iwe nuru, ikawa nuru,” hakuwa na uwezo wa kurudisha ukweli wa Neno lake mara moja na kwa ukamilifu?
Kwanini alisubiri yapite mamia ya miaka baada ya maandiko ya awali kuandikwa, ndipo aanzishe mchakato wa kuyasahihisha? Je, alitaka watu waishi kizazi baada ya kizazi katika upotovu wa maandiko bila msaada wowote?
Kama tunakubali kwamba Mungu alishindwa kuyahifadhi maandiko yake ya awali hadi akalazimika kuyasahihisha baadaye, basi ni dhahiri tunamvua Mungu ukuu na utukufu wake, na kudhoofisha mamlaka yake na uwezo wake usio na kifani. Mimi sikubaliani na hilo. Kwangu mimi Biblia ni Kitabu cha kweli ndiyo sababu shetani anakipiga vita.
www.jamiiforums.com

Biblia ni nini? Maelezo ya kina kuhusu kitabu hiki ambacho shetani anakichukia kuliko vitabu vyote!
Biblia ni mkusanyiko wa vitabu 66 vilivyoandikwa na waandishi mbalimbali kwa muda wa takriban miaka 1,500, lakini vyote vina ujumbe mmoja unaotuelekeza kwa Mungu na jinsi ya kupata wokovu kwa njia ya Yesu Kristo. Biblia imegawanyika katika sehemu kuu mbili: Agano la Kale – Linaeleza uumbaji wa...