Dalton Elijah
JF-Expert Member
- Jul 19, 2022
- 968
- 1,978
Kumekuwepo na chapisho lililosambazwa kwenye mitandao ya kijamii likidai kuwa mwanamke mmoja kutoka nchini Afrika Kusini mwenye umri wa miaka 31 amezeeka ghafla na kuonekana kama bibi mwenye umri wa miaka 80.
Chapisho hilo linaeleza kuwa mwanamke huyo anayefahamika kwa jina la Sinenhlanhla Khoza alianza kukumbwa na hali hiyo akiwa na umri wa miaka 27, muda mfupi baada ya kuhusiana kimapenzi na mwanaume mmoja raia wa kigeni. Kutokana na tukio hilo, mwanamke huyo anadaiwa kuhisi kuwa huenda mwanaume huyo alimroga na kusababisha mabadiliko hayo ya ghafla katika mwonekano wake.