Je ni kweli ndg. Mulugo (n/waziri wa elimu )kasema haya?

Je ni kweli ndg. Mulugo (n/waziri wa elimu )kasema haya?

Kwa Mulugo lolote lawezekana. Kama katumia majina ya watu wengine, mmojawapo ni Lecturer pale DUCE na kama pia anajua muungano wetu na Zimbabwe imo, washangaa nini kwa hayo mapya? Baraza la Mawaziri ni zaidi ya baraza.
 
Mwacheni mzee wa watu apumue maana mwaka huu !! hatousahau
 
Tehe tehe jamaa kweli wa ajabu sana anapaswa kujiunga ze comedy
 
Waziri wenu ni noma kweli halafu eti wanataka "BIG RESULTS NOW" ... Walimu tunasema "BIG RESULTS NO"
 
Mmmm! nina mashaka na hii taarifa kama ni ya kweli,kama ni kweli itakua katika level za juu sana ya kauli tata za viongozi wa juu hapa Tanzania!
 
Mmmm! nina mashaka na hii taarifa kama ni ya kweli,kama ni kweli itakua katika level za juu sana ya kauli tata za viongozi wa juu hapa Tanzania!

Sasa ile aliyosema kuwa Tanzania ni muungano wa visiwa vya Pemba na Zimbabwe sio kauli tata? Mbaya zaidi aliizungumza nje ya TZ si bora hii aliyosema hapa kwetu.
 
inamana hakuna wanatukuyu humu, aidha wathibitshe ama wakanushe hili??? Nachelea kukubali hili, nisaidieni kuamini.
 
Siku mkuu anaanza kuteua mawazir alisema "uwazir hausomewi" nikajua lazima vilaza na kaurafiki katahusika,ikawa kweli.mwisho wa siku madudu yanajitokeza.bora msimu huu uishe,uje msimu wa mabadiliko.
 
Kwa Mulugo chochote kinawezekana ila kama ni kweli haya sasa ni majanga
 
Wakuu nimeikuta hii katika moja ya mtandao wa kijamii

" MAAJABU MENGINE YA NAIBU WAZIRI WA
ELIMU,MH MULUGO
Akiwa katika ziara ya kutembelea chuo cha ualimu
Tukuyu. Wakufunzi walimuuliza swali kwanini
hawapandishwi madaraja kwa muda mrefu.
Mmoja wa wakufunzi alilalamika toka aajiriwe
yuko daraja D ingawa ana mwaka wa kumi kazini.
Mulugo akajibu kwamba atahakikisha anapanda
daraja mpaka A mwaka huu. Akidhani daraja A ni
kubwa kuliko E wakufunzi wote wakabaki
kumshangaa akiwamo mkuu wa chuo wa pale.
Akiongea na wanafunzi wanafunzi walimuomba
serikali iwaajili hata kama wame fail somo moja
yaani kama wana supplementary moja katika
mtihani wao wa mwisho. Mulugo akajibu kwamba
suppementary ni somo kama masomo mengine hivyo
ni lazima wafaulu supplementary asiyefaulu
atakiona. Yeye akidhani supplementary ni
mojawapo ya somo katika course ya ualimu.
Swali:
Alipewaje wizara nyeti kama hiyo wakati haijui
kabisa?"

Duh, hiyo kali
 
jamaa kabla ya kugombea ubunge alikuwa anapiga temporal ya shule moja ya msingi kule mbeya
 
Back
Top Bottom