POTOSHI Je, ni kweli Picha hii inamuonesha George Bush akiwa Osama Bin laden huko marekani

POTOSHI Je, ni kweli Picha hii inamuonesha George Bush akiwa Osama Bin laden huko marekani

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1
Osma.jpg
 
Tunachokijua
Osama Bin Laden anajulikana kama mwanzilishi na kiongozi wa kwanza wa kundi la kigaidi la al-Qaeda amefahamika zaidi duniani kote kwa kupanga na kusimamia mashambulizi ya kigaidi ya Septemba 11, 2001 (9/11) nchini Marekani yaliyosababisha vifo vya karibu watu 3,000 kwa uapnde mwingine George .W bush alikuwa Rais wa 43 wa Marekani, akihudumu kwa mihula miwili kuanzia mwaka 2001 hadi 2009.

Madai

Kumekuwepo na picha inayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, ikidaiwa kuwaonesha aliyekuwa Rais wa Marekani, George W. Bush, na viongozi wengine wa serikali ya Marekani wakiwa wameketi pamoja na aliyekuwa kiongozi wa kundi la kigaidi la al-Qaeda, Osama bin Laden.

Uhalisia

Hata hivyo, uchunguzi wa picha hiyo kwa kutumia njia ya Google Reverse Image Search umebaini kuwapicha hiyo imehaririwa kwa njia za kidijitali ili kuonesha sura ya Osama bin Laden katika picha ya awali ambayo haikuwa na sura yake.

Picha halisi ilichapishwa na Wizara ya Ulinzi ya Marekani, Septemba 12, 2001, katika mkutano uliofanyika Pentagon, siku moja baada ya mashambulizi ya kigaidi ya Septemba , 2001.

Kwa mujibu wa taarifa kutokwa kwenye ya Wizara hiyo, picha ya awali inamuonesha Bush akiwa na Waziri wa Ulinzi wa wakati huo, Donald Rumsfeld, na Naibu Waziri wa Ulinzi, Paul Wolfowitz, pamoja na maafisa wengine wa serikali. Sura ya Wolfowitz ndiyo iliyobadilishwa na kuwekwa sura ya Osama bin Laden katika picha iliyohaririwa.

Hivyo, madai kwamba picha hiyo inamuonesha Osama bin Laden akiwa katika mkutano na George W. Bush si ya kweli. Picha hiyo imehaririwa kwa njia za kidijitali
1791896065446-png.3689912
Back
Top Bottom