Je, ni kweli Royal Tour imesaidia kukuza utalii?

Je, ni kweli Royal Tour imesaidia kukuza utalii?

Nyabukika

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2022
Posts
1,440
Reaction score
1,046
Kwa mujibu wa Takwimu kutoka NBS, Tanzania katika kipindi cha mwaka 2022 ilifanya vizuri zaidi katika sekta mbalimbali zenye mchango wa moja kwa moja katika maisha ya wananchi na pia katika pato la Taifa.

Katika Sekta ya Utalii, kati ya Jan - Oct 2022, Watalii 1,175,697 waliingia nchini ikiwa ni ongezeko la 64% ukilinganisha na idadi ya watalii 716,741 kwa mwaka 2021.

Jitihada nyingi zimefanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ikiwa ni pamoja na kuendesha program ya Royal Tour kote Duniani kutangaza vivutio vya utalii, kuimarishwa kwa ushirikiano kati ya Tanzania na Mataifa mengine na zaidi kuimarishwa kwa hali ya kisiasa na mifumo ya utoaji haki.

Asante Rais wetu kwa kutekeleza ahadi zako.
 
Tungepata mrejesho toka kwa wahusika wa nyanja hiyo ingekua bora san!!
 
Tanzania Royal Tour ilipata airtime tusisahau baada ya uzinduzi watu wengi maarufu walikuja nchini
 
Tuwaulize CHADEMA kama wanajua haya au makovu ya risasi

USSR
Hahahha Chadema hakuna wanachokijua zaidi ya kulalamikia polisi na kutembea na ushuhuda wa Lissu kupigwa risasi lakini ukiwambia hata Miundombinu imeboreshwa, watalii wanazidi kuongezeka nchini kupitia filamu ya royal tour hawaelewi kabisa
 
Utalii uliporomoshwa na Covid, na umenyanyuka baada ya Covid kupungua/kuisha.
Hakuna cha Roho Tour wala nn.
Watu kama nyinyi huwa hamkosekani lakini utaliii ulishuka sana watu ni kama walisahau tena kama Tanzania kuna vivutio vizuri vya utalii ndio manaa Rais Samia Suluhu akaja na wazo la kufanya royal tour iliyowaibua mataifa mbalimbali ikiwemo watu maarufu kuja kutembea nchini kwetu na kupelekea pato la taifa kuendelea kupanda siku hadi siku
 
Mkuu ukifanya ulinganishi na takwimu
Katika Sekta ya Utalii, kati ya Jan - Oct 2022, Watalii 1,175,697 waliingia nchini ikiwa ni ongezeko la 64% ukilinganisha na idadi ya watalii 716,741 kwa mwaka 2021.

kama hizi na nchi nyingine yeyote Duniani, unakuta uwiano unakaribia sawa.

Sasa sijui ni Nchi ngapi nazo zilifanya sarakasi za royal tour kupata ongezeko la watalii nchini mwao..

Hata kama ni pongezi, tusipike na kulazimisha ongezeko hilo na Royal tour.
 
Royal tour haina lolote zaidi ya;;
Ooh yes..
Pitaaa🤣🤣
 
Tungepata mrejesho toka kwa wahusika wa nyanja hiyo ingekua bora san!!
Mimi na wewe ni wahusika maana hapa tunaiongelea Tanzania na sio nchi jirani hata wewe unajua kuwa baada ya royal tour watalii wameongeza na kupelekea kupandisha uchumi wa nchi na wananchi kupitia biashara mbalimbali ikiwemo ya chakula na mahoteli maana hoteli zingine zilifungwa ila baada ya kuongezeka kwa watalii hoteli zinaendelea kujengwa
 
Kipimo cha kujua imeleta tija kuna vitu vingi vya kuzingatia ila nitasema nilichokiona mimi ni T.R.T imeleta tija tunaona takwimu za wageni kuja Tanzania zimeongezeka , kuiweka Tanzania kwenye ramani ya duinia na kuongelewa mara nyingi imewezekana Royal tour imeleta tija
 
Unataman saiv ungekua unasema marehem LISSU lkn MUNGU alikataa uovu wenu!!!
Kweli Mungu ni mwema alikataa uonevu Lissu alipona na akaenda kujificha Ubelgiji lakini Rais Samia Suluhu alipoingia madarakani aliimarisha hali ya ulinzi na usalama na Lissu sasa anakuja Tanzania na kuondoka kama anavyotaka Watanzania tunamshukuru san aMungu kutupa Rais kama Samia
 
Tuwaulize CHADEMA kama wanajua haya au makovu ya risasi

USSR
Sio jambo la wanachadema tu ni la watanzia kwa ujumla ni wote,maana ni kodi zetu zile zimeweka pale,tume invest je zikerudisha faida ndiyo swal tunatdakiwa kujiuliza kujua ROI is it postive or negative?
 
Back
Top Bottom