Kweli Mkuu, watu wanaleta siasa njaa za kumsifu Bibi wakati kiuhalisia hakuna kitu.Mara kibao Mbuga ya Serengeti na Mlima Kilimanjaro zimekuwa zikipata tuzo za kimataifa.Utalii uliporomoshwa na Covid, na umenyanyuka baada ya Covid kupungua/kuisha.
Hakuna cha Roho Tour wala nn.
Acha uongo watu maarufu wamekuwa wakija Tanzania miaka ya nyuma kabla ya Royal Tour.Obama naye alikuja baada ya Royal Tour?Watu kama nyinyi huwa hamkosekani lakini utaliii ulishuka sana watu ni kama walisahau tena kama Tanzania kuna vivutio vizuri vya utalii ndio manaa Rais Samia Suluhu akaja na wazo la kufanya royal tour iliyowaibua mataifa mbalimbali ikiwemo watu maarufu kuja kutembea nchini kwetu na kupelekea pato la taifa kuendelea kupanda siku hadi siku
Kwanza hakuna Assessment ya kitaalamu iliyofanywa juu ya mchango wa Royal Tour na kuongezeka watalii.Mkuu ukifanya ulinganishi na takwimu
kama hizi na nchi nyingine yeyote Duniani, unakuta uwiano unakaribia sawa.
Sasa sijui ni Nchi ngapi nazo zilifanya sarakasi za royal tour kupata ongezeko la watalii nchini mwao..
Hata kama ni pongezi, tusipike na kulazimisha ongezeko hilo na Royal tour.
Inatakiwa ifanywe Assessment ya kitaalamu Ili tupate ukweli.Kipimo cha kujua imeleta tija kuna vitu vingi vya kuzingatia ila nitasema nilichokiona mimi ni T.R.T imeleta tija tunaona takwimu za wageni kuja Tanzania zimeongezeka , kuiweka Tanzania kwenye ramani ya duinia na kuongelewa mara nyingi imewezekana Royal tour imeleta tija
Lipo wazi mkuu mbona,haliitaji hata to hire an expert to do thatInatakiwa ifanywe Assessment ya kitaalamu Ili tupate ukweli.
Una lako jambo bila shaka.Utalii uliporomoshwa na Covid, na umenyanyuka baada ya Covid kupungua/kuisha.
Hakuna cha Roho Tour wala nn.
Kwanza hakuna Assessment ya kitaalamu iliyofanywa juu ya mchango wa Royal Tour na kuongezeka watalii.
Exactly hii haina kupinga Royal tour imewaibua hadi watu maarufu kwaiyo sasa watanzaniua tunakula matunda ya royal tour maana hadi muuza matunda ananufaika na ongezeko hili la watalii
Kwani wewe hujasikia Mamba aliyeuawa ?Kwa mujibu wa Takwimu kutoka NBS, Tanzania katika kipindi cha mwaka 2022 ilifanya vizuri zaidi katika sekta mbalimbali zenye mchango wa moja kwa moja katika maisha ya wananchi na pia katika pato la Taifa.
Katika Sekta ya Utalii, kati ya Jan - Oct 2022, Watalii 1,175,697 waliingia nchini ikiwa ni ongezeko la 64% ukilinganisha na idadi ya watalii 716,741 kwa mwaka 2021.
Jitihada nyingi zimefanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ikiwa ni pamoja na kuendesha program ya Royal Tour kote Duniani kutangaza vivutio vya utalii, kuimarishwa kwa ushirikiano kati ya Tanzania na Mataifa mengine na zaidi kuimarishwa kwa hali ya kisiasa na mifumo ya utoaji haki.
Asante Rais wetu kwa kutekeleza ahadi zako.