Katika jamii za kiafrika hasa Tanzania kumekuwa na nadharia kuwa mtu aking'oa mvi moja kichwani inasababisha kuota nyingine nyingi.
Baadhi ya watu wakiwa katika umri ambao si wakuota mvi au wale ambao wanaanza kuota mvi, mvi zikianza kuchipua kichwani wanazing'oa wakiamini hazitaota tena lakini baadhi ya watu wanawaonya kuwa wasizing'oe kwasababu zitaota nyingine nyingi.
Je, ni upi ukweli kuhusu nadharia hiyo?
Baadhi ya watu wakiwa katika umri ambao si wakuota mvi au wale ambao wanaanza kuota mvi, mvi zikianza kuchipua kichwani wanazing'oa wakiamini hazitaota tena lakini baadhi ya watu wanawaonya kuwa wasizing'oe kwasababu zitaota nyingine nyingi.
Je, ni upi ukweli kuhusu nadharia hiyo?
- Tunachokijua
- JamiiCheck imefuatilia jambo hili kupitia tafiti na makala mbalimbali za kiafya na kubani kuwa madai hayo si ya kweli bali ni nadharia tu.Nadharia hii imekuwa ikieleza kuwa mtu aking’oa nywele moja yenye mvi inaweza kupelekea kuota kwa nywele nyingine 10 zenye mvi.
Kisayansi hakuna uwezekano wa mzizi mmoja wa nywele kuota nywele zaidi ya moja, hivyo Kung'oa mvi moja hakutopelekea kupata mvi nyingine zaidi, kwa sababu kuna nywele moja tu inayoweza kuota kwa kila mzizi wa nywele (follicle).
Nywele zinazoizunguka hazitabadilika kuwa nyeupe hadi seli za rangi (pigment cells) za mizizi yake zitakapokufa.
Ingawa kung'oa mvi inaweza kuonekana kama suluhisho la haraka na rahisi kwa changamoto zako za matunzo ya nywele, lakini kung'oa mara kwa mara kunaweza kuharibu mzizi wa nywele na kuisababisha nywele kukatika au kuwa nyepesi.
Sambamba na hayo kufanya hivyo mara kwa mara kunaweza kusababisha tatizo la ngozi kuwa na madoa meusi (post-inflammatory hyperpigmentation) na kufanya tatizo kuonekana zaidi kwa wengine.
Desmond Tobin, Profesa wa sayansi ya ngozi katika Chuo Kikuu cha Dublin anaeleza kuwa "Laiti kama ingekuwa kung'oa nywele moja kunaifanya iote zaidi, ingekuwa suluhisho kubwa kwa watu ambao nywele zao zinapungua na hawajafurahishwa na hali hiyo.