- Source #1
- View Source #1
Nimekutana na hii video TikTok na maelezo haya, kuna uhalisia wowote wa hili?
==
Taswira inayozidi kujitokeza ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) inazidi kuibua maswali mengi kuliko majibu, huku vitendo vya baadhi ya viongozi vikionekana kukiondoa chama hicho kwenye misingi ya kidemokrasia na kukisogeza karibu na mtindo wa magenge ya kihuni.
Katika video inayosambaa kwa kasi, baadhi ya wanachama na viongozi wanaonekana wakizushiana vurugu kufuatia maswali yaliyoibuliwa kuhusu kampeni ya kuchangisha michango inayofahamika kama ‘Tone kwa Tone’.
Badala ya kutoa majibu ya kistaarabu na ya uwazi kuhusu matumizi ya fedha hizo za wanachama, baadhi ya viongozi wanatuhumiwa kutoa amri ya kushambuliwa na kupigwa kwa wanachama wanaojaribu kuhoji haki yao.
Hali hii inadhihirisha sura mbaya ya uongozi ndani ya chama hicho, ambapo sauti mbadala na uwajibikaji vinajibiwa kwa mabavu na vitisho, jambo linalowafanya wachambuzi wengi kuhoji kama kweli hiki ni chama cha siasa au kimeshaingiliwa na mifumo ya kihuni inayolinda maslahi ya wachache kupitia mifuko ya wanachama wanyonge.

- Tunachokijua
- Kumekuwapo na video inayosambazwa mtandaoni inayowaonesha wafuasi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wakilalamikia jambo na kuambatanishwa na kichwa cha habari kinachosomeka "Viongozi wa CHADEMA waamuru wapigwe wanaohoji kuhusu Tonetone"
Je, ni upi uhalisia?
Ufuatiliaji wa JamiiCheck umejiridhisha kuwa video inapotosha kwani inatumiwa katika muktadha tofauti na uhalisia wake. Kupitia Google Reverse Image search imebainika kuwa video hiyo si ya mwaka 2026 bali ni ya 2024 kutoka kwenye uchaguzi wa CHADEMA mkoa wa Arusha.
Novemba 13, 2024 Ulifanyika uchaguzi wa CHADEMA mkoa wa arusha ambapo wakati wa uchaguzi huo ziliiibuka vurugu ambapo baadhi ya wanachama walidai uchaguzi huo kughubikwa na rushwa, huku wakimtuhumu aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho Kanda ya Kaskazini, Godbless Lema kuvuruga uchaguzi huo kwa kutaka baadhi ya wagombea wachaguliwe.
Akizungumza nje ya ukumbi ulipofanyika uchaguzi huo, mmoja wa wanachama wa Chadema Jimbo la Arusha, Boniface Kimario, alidai kuwa uchaguzi huo umeghubikwa na rushwa huku akidai Lema kupanga safi ya viongozi.
Alipozungumzia tukio hilo, aliyekuwa Katibu wa CHADEMA Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa alisema kuna watu wasiohusika ambao hawakuwa wajumbe hawawezi kuingia kwenye uchaguzi, kanuni zinataka wajumbe peke yao ndiyo wanaruhusiwa.
“Kuna watu kwa sababu ambazo hatukuwa tumezielewa waling’ang’ania kutaka kuingia kwenye uchaguzi, mfano uchaguzi wa wanawake wanaingia wanawake pekee, kuna baadhi ya wanaume walitaka kuingia kwenye uchaguzi wa wanawake pia kuna watu ambao kwenye mchujo walikatwa, kwa sababu za kikanuni baadhi yao waliendelea kubeba hisia kuwa wanaonewa,” alisema Golugwa.
“Kwa mfano Baraza la Vijana linahitaji vijana kuanzia miaka 30 na usizidi miaka 35 kwenye uongozi, sasa mtu hana hicho kigezo. Kilichofanyika ni kuwazuia wanachama wachache, kwenye vyama hivi kuna watu wa kila namna hata wehu na wendawazimu tunao,wengine walikuja wamelewa,”
“Walizuiwa na walipotaka kutumia nguvu, nguvu zilitumika kuzuia, kwa hiyo walizuiwa hatuwezi kusema tumepigana. Huu ndiyo ufafanuzi halisi, dunia nzima kanuni za uchaguzi zinataka wajumbe pekee ndiyo waingie kwenye kikao, ni wendawazimu mtu anang’ang’ania awepo,”