Je ni kweli wajenzi wa zamani walikuwa na uwezo wa kubuni na kuunda kwa ustadi na ufanisi mkubwa kuliko wa sasa?

Je ni kweli wajenzi wa zamani walikuwa na uwezo wa kubuni na kuunda kwa ustadi na ufanisi mkubwa kuliko wa sasa?

Bob Manson

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2021
Posts
4,158
Reaction score
7,787
Habarini za wakati huu wadau...

Tupo katika dunia au kizazi cha teknolojia na mapinduzi makubwa katika nyanja zote ambazo zinahusu teknolojia na ujuzi, lakini haina maana kwamba waliopita waliishi katika dunia au kizazi cha giza kama ambayo tunaambiwa.

Ukitizama majengo ambayo yalijengwa zamani utagundua kuna utofauti mkubwa na sasa, ubunifu na ufanisi katika ujenzi ulikuwa mkubwa hapo zamani.

Leo hii kuna architecture's ambao wanadai wanabuni na kuunda majengo ya kisasa lakini ukiyatazama hakuna ubunifu zaidi ya matumizi ya rangi na vioo tu.

IMG_20230330_232332.jpg


Majengo ya zamani yana ubunifu mkubwa na yamewekwa nakshi ambazo bado hatujui walitumia nini kujengea au kuchorea. Licha ya ubunifu, majengo hayo pia yana uimara wa kudumu kwa muda mrefu.

Bado hakuna maelezo rasmi ya ni namna gani walijenga majengo hayo au ni vifaa gani walitumia katika ujenzi huo.

Japo wengi wanaamini kwamba kwa sasa ujenzi wa majengo umerahisishwa na kuwa simple lakini mimi naamini ni ukosefu wa ubunifu na uvivu wa kubuni na kufikiri.

BAADHI YA MICHORO ILIYOMO KATIKA MAJENGO YA ZAMANI.

Katika hali ya kushangaza, kumekuwepo na majengo ya zamani ambayo ndani yake kuna michoro au miundo ambayo inafanana na ile iliyopo katika vifaa vya kiteknolojia vya kisasa.

img_20221106_71138-jpg.3071140


Ni dhahiri kwamba michoro hiyo imeigwa kutoka kwa stadi za watu wa zamani, Je lengo la michoro hiyo katika vifaa vya kisasa ni lipi?

Kama picha inavyo onyesha, huo ni mchoro mmoja katika sehemu mbili tofauti. Baadhi ya wachunguzi wanadai huo ni mchoro unao ashiria flow of energy na Hilo jengo lilikuwa ni Temple kwaajili ya ibada.

Bado najiuliza kuna uhusiano gani kati ya mchoro ndani ya nyumba ya ibada na kifaa cha kiteknolojia? Yaani (Chip device)

Mdau, unadhani au kufikiri ni ipi sababu ya kuiga na kuiweka michoro ya zamani katika vifaa vya kisasa?

Karibu........
 
Wa sasa ni zaidi sababu wamepata elimu kubwa na teknolojia imesaidia hivyo wanaweza kubuni structure ya aina yoyote na ikawezekana kujengwa eneo lolote(rejea palm Jumeirah - Dubai)
Tatizo sio kubuni eneo la kujenga, zamani walijenga majengo imara na yenye design za kuvutia tofauti na sasa majengo ni vioo na rangi tu, hakuna cha zaidi
 
Habarini za wakati huu wadau...

Tupo katika dunia au kizazi cha teknolojia na mapinduzi makubwa katika nyanja zote ambazo zinahusu teknolojia na ujuzi, lakini haina maana kwamba waliopita waliishi katika dunia au kizazi cha giza kama ambayo tunaambiwa.
Watu wa zamani waliku na maarifa makubwa na elimu ndogo, na watu wa sasa wana elimu kubwa maarifa kidogo. Hiyo ndio point kuu hapo
 
Tofauti ipo kwenye Durability.

Ni wazi kuwa Majengo ya zamani ni imara sana kwasababu aina ya Cement waliyotumia haikuchakachuliwa ili kemikali kidogo itoe output kubwa yaani cement nyingi, pia mawe yaliyotumika yalikuwa makubwa na mazito...au matofali ya kuchoma, kama sio ya kuchoma basi ni matofali ya Miamba migumu

Aidha, kuna baadhi ya majengo yalikuwa ni miamba kabisa iliyochongwa

Kwasasa ubunifu mkubwa walionao ni kwa upande wa ramani ila materials hamna kitu

Ila kiujumla ukipima IQ za watu wa zamani na wa sasa ni tofauti kabisa na hata Wazungu wasasa wanakiri hilo...

Just imagine Ubunifu wa Gustave katika kujenga EIFFEL TOWER na Statue of liberty, Pyramids zile za Gaza, kuta ya China, madaraja ya zamani

Tazama hospitali, Shule na Makanisa ya zamani ya kikoloni East Africa
 
Just imagine Ubunifu wa Gustave katika kujenga EIFFEL TOWER na Statue of liberty, Pyramids zile za Gaza, kuta ya China, madaraja ya zamani

Tazama hospitali, Shule na Makanisa ya zamani ya kikoloni East Africa
Sahihi kabisa, watu wa zamani walikuwa wabunifu na wenye uwezo mkubwa wa kufikiri.

Umahiri wa majengo yao hauwezi kufikiwa na majengo ya sasa, pia mbinu walizo tumia kujenga hatuzijui au zimefichwa kama siri
 
Back
Top Bottom