Bob Manson
JF-Expert Member
- May 16, 2021
- 4,158
- 7,787
Habarini za wakati huu wadau...
Tupo katika dunia au kizazi cha teknolojia na mapinduzi makubwa katika nyanja zote ambazo zinahusu teknolojia na ujuzi, lakini haina maana kwamba waliopita waliishi katika dunia au kizazi cha giza kama ambayo tunaambiwa.
Ukitizama majengo ambayo yalijengwa zamani utagundua kuna utofauti mkubwa na sasa, ubunifu na ufanisi katika ujenzi ulikuwa mkubwa hapo zamani.
Leo hii kuna architecture's ambao wanadai wanabuni na kuunda majengo ya kisasa lakini ukiyatazama hakuna ubunifu zaidi ya matumizi ya rangi na vioo tu.
Majengo ya zamani yana ubunifu mkubwa na yamewekwa nakshi ambazo bado hatujui walitumia nini kujengea au kuchorea. Licha ya ubunifu, majengo hayo pia yana uimara wa kudumu kwa muda mrefu.
Bado hakuna maelezo rasmi ya ni namna gani walijenga majengo hayo au ni vifaa gani walitumia katika ujenzi huo.
Japo wengi wanaamini kwamba kwa sasa ujenzi wa majengo umerahisishwa na kuwa simple lakini mimi naamini ni ukosefu wa ubunifu na uvivu wa kubuni na kufikiri.
BAADHI YA MICHORO ILIYOMO KATIKA MAJENGO YA ZAMANI.
Katika hali ya kushangaza, kumekuwepo na majengo ya zamani ambayo ndani yake kuna michoro au miundo ambayo inafanana na ile iliyopo katika vifaa vya kiteknolojia vya kisasa.
Ni dhahiri kwamba michoro hiyo imeigwa kutoka kwa stadi za watu wa zamani, Je lengo la michoro hiyo katika vifaa vya kisasa ni lipi?
Kama picha inavyo onyesha, huo ni mchoro mmoja katika sehemu mbili tofauti. Baadhi ya wachunguzi wanadai huo ni mchoro unao ashiria flow of energy na Hilo jengo lilikuwa ni Temple kwaajili ya ibada.
Bado najiuliza kuna uhusiano gani kati ya mchoro ndani ya nyumba ya ibada na kifaa cha kiteknolojia? Yaani (Chip device)
Mdau, unadhani au kufikiri ni ipi sababu ya kuiga na kuiweka michoro ya zamani katika vifaa vya kisasa?
Karibu........