Je ni kweli wajenzi wa zamani walikuwa na uwezo wa kubuni na kuunda kwa ustadi na ufanisi mkubwa kuliko wa sasa?

Kitu kingine ambacho watu wanashindwa kuelewa ni kwamba, jengo kama hili sisi tunaliona jinsi lilivyo leo.
Pata picha wakati ndio limekamilika, halijapigwa na vumbi, mvua, wala kupaushwa na jua. Lilikuaje?
Kweli kabisa, mpaka leo bado lipo imara. Haya majengo ya sikuhizi baada ya miaka kadhaa tunaanza kuziba nyufa na viraka vya rangi iliyo liwa na fangus.
 
Tatizo wanajenga hidden roof kwa kudanganywa na mafundi kuwa ni ujenzi rahisi kumbe hata mafundi wenyewe hawana ujunzi sahihi wa kujenga hizo nyumba
Alafu kuna zile nyumba za uswazi, baada ya miaka kadhaa nyumba inazidi kuzama chini, dirisha linafikia ardhini kabisa.
 
Kuna sehemu huku matofali yanatengenezwa na wafungwa tofali zege msumali haupiti halafu kuna sehemu tofali linatengenezwa na wapigaji kitu mchanga wa kutosha ukipiga kofi hakuna tofali hapo yaan lazima majengo yatofautiane zamani walikua wanajenga kwa kutumia mawe kabla ya ugunduzi wa saruji
 
Walitumia vitu vingi zaidi ya mawe, lakini ubora wa majengo yao ni jawabu kwamba walikuwa na ufanisi mkubwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…