Je, ni kweli wanasiasa wanachochea migogoro ya ardhi?

Je, ni kweli wanasiasa wanachochea migogoro ya ardhi?

Nyabukika

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2022
Posts
1,440
Reaction score
1,046
Katika hotuba ya Rais Samia Suluhu leo amegusia suala la migogoro la ardhi amesema kuwa:

"Wakati wananchi wanavamia maeneo, wanasiasa hatuwaambii wananchi ukweli, tunawaangalia wakivamia na badala yake tunakuja kusimama kutetea wavamizi wa maeneo yale [..] lengo ni kupata kura huko baadaye wasikuone wewe ni mbaya.” Rais Samia Suluhu

Rais Samia Suluhu anaendelea kuhakikisha wananchi hawaingii katika migogoro ya ardhi na Wizara ya ardhi ikishilikiana na mawaziri mbalimbali wapatao sita walianza ziara kuzuka katika vijiji zaidi ya 900 ili kutatua migogoro ya ardhi.
 
Huu ni ukweli.

Dodoma Matuli na Ndachi Diwani na Mkewe Wameuza Mashamba yenye hati Viongozi wa Jiji nao wamejigawia maeneo yawatu wamepanga maeneo ya vituo vya mafuta mahoteli na kujimilikisha bill kufuata sheria za hatimiliki.

Hatari wizi kama maduka ya kubadili fedha ya Arusha ulivyo fanyika. Waziri waArdhi komaa na jiji la Dodoma ukweli utauona
 
Hata Gwajima kule jimboni Kawe ni hivyo hivyo tu yuko bega bega na wavamizi wahuni wa maeneo ya watu.

Badala ya kusimama kwenye ukweli na haki anatetea wavamizi wa maeneo ya watu.

Fikiria kuna wananchi wamekopa hela nyingi na wakanunua maeneo yao halafu kikundi cha wahuni wanavamia na kuuza maeneo ya watu [emoji848][emoji848]

Wengine ni wazee wastaafu wamenunua Kwa viinua mgongo vyao halafu wahuni wanavamia na kuuzia watu mbali mbali.

Gwajima wewe ni Mwana wa Mungu unatetea wavamizi wahuni sababu ya kutafuta kupigiwa kura uchaguzi ujao ?

Kwanini utetetee wahalifu ?

Tunajenga jamii ya aina gani?

Hata RC alishaweka wazi kuwa wavamizi wa maeneo ya watu ni wahalifu kama wahalifu wengine kwenye jamii.
 
Gwajima migogoro ya ardhi ya Kata ya Mabwepande hususa Mbopo unatakiwa kusimama kwenye ukweli haki ipatikane wenye maeneo yao warejeshewe haraka.

Simama upande wa haki .

Toa support kwa watendaji wa serikali katika kutatua mgogoro huo,

Us ifanyike kikwazo.
 
Nilikupigia campaign kubwa ushinde ubunge Kawe wakati wa uchaguzi ulopita.

Tulikuwa na matarajio makubwa sana ya wewe kuwa utakuwa unapendezwa na haki Kama Mtumishi wa Bwana Mungu.

Sasa usituangushe.
 
Pitia nyuzi za campaign utaona nilijitoa mhanga kukupigia debe ushinde pamoja na upinzani mkubwa ambao ulikuwepo.
 
Mheshimiwa Rais ameongea ukweli kabisa.

Tunategemea achukue hatua sasa stahiki na kuwa encourage watendaji wafanye maamuzi magumu [emoji123]
 
Huu ni ukweli.

Dodoma Matuli na Ndachi Diwani na Mkewe Wameuza Mashamba yenye hati Viongozi wa Jiji nao wamejigawia maeneo yawatu wamepanga maeneo ya vituo vya mafuta mahoteli na kujimilikisha bill kufuata sheria za hatimiliki.

Hatari wizi kama maduka ya kubadili fedha ya Arusha ulivyo fanyika. Waziri waArdhi komaa na jiji la Dodoma ukweli utauona
Rais Samia Suluhu ni mpenda haki and i hope atasimamia haki za wananchi wake ipaswavyo
 
Hata Gwajima kule jimboni Kawe ni hivyo hivyo tu yuko bega bega na wavamizi wahuni wa maeneo ya watu.

Badala ya kusimama kwenye ukweli na haki anatetea wavamizi wa maeneo ya watu.

Fikiria kuna wananchi wamekopa hela nyingi na wakanunua maeneo yao halafu kikundi cha wahuni wanavamia na kuuza maeneo ya watu [emoji848][emoji848]

Wengine ni wazee wastaafu wamenunua Kwa viinua mgongo vyao halafu wahuni wanavamia na kuuzia watu mbali mbali.

Gwajima wewe ni Mwana wa Mungu unatetea wavamizi wahuni sababu ya kutafuta kupigiwa kura uchaguzi ujao ?

Kwanini utetetee wahalifu ?

Tunajenga jamii ya aina gani?

Hata RC alishaweka wazi kuwa wavamizi wa maeneo ya watu ni wahalifu kama wahalifu wengine kwenye jamii.
Hawa wote wakigundulika lazima watawajibishwa maana kikudi cha watu wachche ndio wanaifitinisha serikali ya Rais Samia Suluhu na wananchi
 
Mheshimiwa Rais ameongea ukweli kabisa.

Tunategemea achukue hatua sasa stahiki na kuwa encourage watendaji wafanye maamuzi magumu [emoji123]
Mungu ni mwema atamuongoza Rais Samia Suluhu ili kuendelea kusimamia haki za watanzania wanazozulumiwa
 
IMG_6878.png
 
Back
Top Bottom