Inategemea audience ni nani na how relevant hiyo title ipo kwenye audience hiyo, miongoni mwa wasomi progressive wa sasa, kujitambulisha kama Dr. (mostly non medical doctors, academicians) inaonekana ni kujionyesha. Ukiwa katika mazingira ya academia, unaandika papers, unapresent mambo, unafundisha etc etc then ni proper kuitwa Dr.
Wengi wanaona kwamba wao ni more than Drs, na kujitambulisha kama Doctors ni ulimbukeni, kama vile that is the biggest achievement ya maisha yako wakati kuna miwatu ni mi philanthropist Nobel laureate humanitarian diplomat war heroes etc etc, utam reduce vipi kwa kumuita Dr.
Kwa mfano, mtu anayetaka kuweka titles za Mnigeria ambaye ana Phd, ni Chifu wa kabila lao na balozi wa nchi yake atamuitaje?
Chief Doctor Ambassador So and So?
Au hata balozi wetu wa UN ambaye si chifu bali ni Dr, utamuitaje? Dr Ambassador Mahiga? au Ambassador Dr. Mahiga?
Ndiyo maana wengine wanaona kama venue / story si academic, baada ya kumuintroduce kama balozi wanamuita tu Mr. Mahiga.
Hizi habari za kutaka kulazimisha kuitwa Dr, au Eng zinaonyesha ulimbukeni, kwamba wewe unakuwa defined na elimu yako badala ya who you truly are. Ni namna moja ya kusema "mimi nimebahatisha huu u Dr au U Engineer, na nataka kila mtu ajue ninavyolimbuka"
Sasa kila mtu akilazimisha kuitwa kwa kulingana na profession yake si itakuwa tabu.
Hizi guilds za 19th century kumbe zinaendelea mpaka leo jamani? Complete with the classism and elitism they represent?