Je ni lazima kupima HIV hospitali?

Je ni lazima kupima HIV hospitali?

Kiteitei

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2009
Posts
1,595
Reaction score
1,540
Naomba kufahamu,

Nina kijana wangu wa shamba aliumia kidole last week kwa kuangukiwa na pipa,sasa leo nimekwenda shamba nakuta bado kidole hakijapona vizuri nikaonelea nimpeleke hospitali, nimemshusha hosp kufuatilia vitu vingine, kurudi namkuta anasubiria kuingia maabara na mojawapo ya vipimo alivyoandikiwa ni hiv test, nikamuuliza nesi/dokta kwa nini, akanijibu kuwa kila kijana lazima wampime hata kama hataki majibu, nikamuuliza taratibu najua lazima kabla mtu hajapimwa aandaliwe kisaikolojia kwa nini haiko hivyo?

Jibu alilonipa ni kuwa kila mtu siku hizi yuko anajua...hapa niko kwenye benchi namsubiria kijana atoke huko ndani....wakuu naomba kuuliza je ni sahihi kupima bila hiyari na bila councelling?
 
Si sawa!!!!
Anatakiwa aambiwe na akubali kwa hiari yake!!!

Kama ni random sampling basi wachukue specimen kwa lengo tofauti say widal then watapima kwa faida ya hao watafiti na sio kutingisha japo ukope wa client!!!!

Hospitali gani???!!
 
Sorry...sio hospitali ni dispensary inaitwa ikunda iko maeneo ya bunju b!
 
kwa matumizi yao thawa..ila ili upewe majibu ni lazima upewe counselling
 
Ajabu sana, vipimo vya lazima. Inaonekana kadri namba ya watu wanaopimwa na kuonekana wana hiv inavyoongezeka ndivyo serikali inavyoingiza pesa nyingi! huwa nashangaa pia kwanini mama mjamzito ni lazima apime UKIMWI wakati kupima ni hiari.
 
Ajabu sana, vipimo vya lazima. Inaonekana kadri namba ya watu wanaopimwa na kuonekana wana hiv inavyoongezeka ndivyo serikali inavyoingiza pesa nyingi! huwa nashangaa pia kwanini mama mjamzito ni lazima apime UKIMWI wakati kupima ni hiari.

Umesoma mpka level gan?..na usiwe na ufaham juu ya ukimwi toka kwa mama kwenda kwa mtoto....acha viroja
 
Hata kule Lindi kuna hospitali moja inaitwa sijui Birigita au Bigirita? Yaani ukienda tu kwa daktari lazima akuandikie kupima HIV hata kama umejikwaa umeendea Iodine tu! Sasa huko sasa mnaingia wanne wanne na mkifika tu unamkuta dogo mepinda anawaambia...'Mnajua mmekuja kupima Ukimwi eeh??'' Baada ya hapo bila hata stori ya kukuandaa unaambiwaleta kidole nichukue damu.
Wakati wa majibu ndio vioja sasa! Hata hawajakuaanda kisaikolojia unaulizwa maswali kibao...baadaye unaambiwa ni mara ya ngapi kupima ukimwi?...ukishajibu anakwambia...Kipimo chetu kinaweza kutambua maambukizo ya baada ya wiki 2, endelea kujilinda na urudi tarehe.....''
Hizi hospitali wasipoweka wtu wa kufanya counselling watakuja kusababisha mauaji bure kwa wanaoendea majibu!
 
Back
Top Bottom