Je ni mbinu ya kimkakati kuwapa uraia wachezaji wa kigeni kwa maandalizi ya CHAN na AFCON?

Dabil

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2021
Posts
6,823
Reaction score
15,293
Wakuu nadhani siyo jambo la kawaida uraia kutolewa kwa wachechezaji wa kigeni,ilianza kwa Singinda Big Stars sasa nasikia Simba nao wachezaji 9 wanaomba uraia.

Nimewaza tu je huu sio mpango kweli kwa mechi za kimataifa kama CHAN na AFCON ili tuwe na kikosi imara cha Taifa Stars? Tusishangae wachezaji zaidi wazuri wa Simba,Azam na Yanga kuomba uraia na wakapata. Nadhani kama ni kwa madhumuni hayo Taifa imeona mbali.

Soma: Singida Black Stars yawabadilisha Uraia wachezaji wanne wa Kigeni na kuwa raia wa Tanzania ili Kukidhi Kanuni

Soma: Idara ya uhamiaji yatoa ufafanuzi dhidi ya wachezaji wa kigeni Singida Black Stars, wote ni raia wa Tanzania kwa Tajnisi

Soma: Simba yatuma rasmi ombi kwa Idara ya Uhamiaji kuomba uraia wa wachezaji wake 9 wa kigeni
 
Kwamba vijana wa Tanzania hawana vipaji?
Mtaani kuna wakaka wengi wanasakata boli lakini hawapewi nafasi.

Akili hajawahi kutembelea nchi ya Tanzania.
 
Kasome kanuni za FIFA, hao hawawizi kabisa Kucheza stars labda ipite miaka 5
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…