Je, ni mfuko gani wa UTT AMIS uko vizuri zaidi?

Kwa hakika ni bora zaidi kuweka fedha zako liquid fund kuliko kuiacha kwenye akaunti za savings au hata most fixed deposits za benki.

Liquid fund ni bora kuliko akaunti za benki kwavile:
1) Riba zake per annum ni kubwa zaidi, >11%;
2) Riba hukokotolewa na kuingizwa kila siku kwa njia ya ongezeko la thamani ya kipande - na unaweza kukokotoa faida uipatayo siku kwa siku;
3) Ukitaka fedha zako unajaza fomu ya kuuza vipande (vyote au baadhi) na malipo huingizwa katika akaunti within 3 working days at most.
 
Asante sana mkuu kwa ufafanuzi zaidi, je ukitaka kudeposit pesa mpaka uende kwenye ofisi zao?
 
Na je hii maturity yake ni ya mda gani?? Yaani ni miezi mitatu, sita, mwak au miaka mingapi?
 
Na ukishajaza hiyo fomu ya kuuza vipande ni mpaka wafanikiwe kuuza ndo upate pesa zako?? Nauliza hvi coz nina hisa za voda nilinunuaga nikaweka sokoni mpk leo mwaka wa pili hawajafanikiwa kupata wateja.
 
Na ukishajaza hyo fomu ya kuuza vipande ni mpk wafanikiwe kuuza ndo upate pesa zako?? Nauliza hvi coz nina hisa za voda nilinunuaga nikaweka sokoni mpk leo mwaka wa pili hawajafanikiwa kupata wateja.
Hapana mkuu.

Kwa liquid fund hakuna kungojea kwa vile wao wenye mfuko ndio wananunua vipande vyako. Ni garantii ndani ya siku 3 za kazi pesa zinaingizwa katika akaunti yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…