Mimi ndio naiona hii leo ila kitu ambacho unatakiwa kujua kuhusu UTT ni mutual funds au tukisema a collective investment scheme ambapo ni kama unachangia pesa katika utekelezaji wa jambo fulani alafu pesa inarudi na faida kutokana na kile kilichowekezwa. Na wewe kama mwekezaji unatakiwa kujua lengo lako la uwekezaji, muda unaotaka na ukwasi(liquidity). Na uwekezaji unawakilishwa na kipande ambao ni uwiano wa umiliki wako kwenye mfuko. Alafu wakati wa gawio mwenye ana vipande vya juu basi na gawio linakua uko juu. Sasa UTT ina mifuko 6 nadhani na mfuko ulioambiwa unaitwa liquid na ni mfuko wa wazi wa muda mfupi/kati na unaweza kupewa riba nzuri kabisaaaa na kianzio chake ni 100,000