Mutual funds (mfano UTT) zipo ulimwenguni pote na ziko reliable sana. Kwangu mimi naona ni reliable kuliko hata benki, kwa vile hata hapa kwetu Tz tumekwishashuhudia benki kadhaa kufilisika na kufa.
UTT ni mfuko ulioanzishwa na serikali, ambayo ilitoa waitayo seed money. Na serikali inailinda ili iendeshwe kwa kanuni za mifuko hiyo ulimwenguni. Wanawekeza asilimia kubwa ya fedha zao katika sehemu ambazo risk ni minimal, karibu na hakuna - mfano kwenye treasury bonds, Municipal bonds, baadhi ya hisa nk.
Ni wazi kukitokea machafuko katika nchi mfano ilivyo sasa Ukraine, mifuko ya jinsi hii inaweza kushindwa kujiendesha, kwa vile hata serikali yenyewe inaweza kushindwa kwa mfano kuhudumia bonds. Risk ya hali hii kutokea ni ndogo mno.
Hivyo wakuu, utt ni sustainable as long as nchi na serikali vinabaki viable.
Mimi nilianza kuwekeza UTT toka inaanzishwa, na ninaendelea kuifaidi. Na pia nimewekeza kwenye treasury bonds. Havijawahi kuniangusha.