Je, ni mfuko gani wa UTT AMIS uko vizuri zaidi?

Je, ni mfuko gani wa UTT AMIS uko vizuri zaidi?

Uza tu mkuu wala hautajutia.
Unajua ndio maana wahindi wengi hawajengi. Sio kwamba wanaogopa ila wanajua hasara ya kuweka pesa chini isiyozalisha, Imagine mtu ana nyumba ya 200m lakini napata shida na ada ya mtoto ya sh 4m wakati pesa aliyoweka chini anaweza kupata 20m kwa mwaka. Usishangae wahindi kwa biashara ndogo tu watoto wanasoma shule za maana, hata nje ya nchi.
Asante sana ndugu. Mimi nimeshajenga nyumba ya kuishi, nina milioni 20 nataka nikawekeze UTT. Nataka kila nikipata hela nakuza mtaji wangu. Sitaki kujenga nyumba za kupangisha maana naona zitanisumbua. Nina uwezo wa kusave 20m kwa mwaka kwenye mshahara wangu.
 
Mkuu uko sahihi.

Mimi niongezee kuwa nina nyumba ya kupangisha - lakini usumbufu ninaopata kukusanya kodi, na pia fedha ipatikanayo - nikipata mteja nitauza hiyo nyumba na kuweka fedha zote utt (au Treasury bonds za muda mrefu zikipatikana).
Nyumba ipo wapi na ukubwa wa eneo upoje
 
Nashukuruni nyote mliochangia kwa mawazo ya kina na Yakinifu kuhusu mifuko mbalimbali ya UTT mbarikiwe Sana na mzidishiwe

Ningependa kushauri watu wajifunze zaidi kupitia nyuzi kama hii,mitandaoni kama You TUBE ,kuwasilina na UTT kupitia namba za huduma kwa wateja Ili kuepusha malalamiko yasiyo na msingi kwamba mtu amejiunga na mfuko asioupenda
 
Nitoe shukurani kwa elimu iliyotolewa humu hasa hasa kwa michango ya mwaka jana. Baada ya kusoma maelezo yaliyotolewa humu nimeshawika kujiunga lakini wakati nafungua APP nimekutana na maswali kuhusu mfuko wa Bond na mfuko wa Ukwasi

1. Kwenye mfuko wa Bond, wanaposema kianzio cha Ths.50,000/= kwa lengo la kukuza mtaji maana yake ni nini? Utapata faida kwa hiyo elfu 50 yako au utaanza kupata faida na gawio baada ya kufikisha Mil.5+?

2. Huo mtaji unakuaje? Yaani una kuzwa na faida itakayozalishwa au inakua kwa wewe kuendelea kuweka kidogo kidogo? Maana hawajataja kiasi cha kuendelea kununua vipande kama mifuko mingine walivyotaja

Mwisho, nimeona wachangiaji wengi wanataja uwekezaji wa mamilioni ya pesa (Mil.10, 20,...) lakini hii isitukatishe tamaa sisi wenye vi elfu kumi kumi au vi laki laki maana waendeshaji wenyewe wa mfuko wanajua hali zetu ndio maana wameweka kima chini. Huku kwa maoni yangu ni sahihi kutunza pesa zako kuliko hata SACCOSS
View attachment 2853182View attachment 2853183
 
Mkuu samahani naomba kueleweshwa
Kwa mfano nimewekeza kiasi cha sh 10 milioni sasa nikakaa miezi 2 nikapata changamoto nikataka kutoa kiasi kidogo kama cha 2 milioni, je inakubalika kutoa kiasi kiasi kidogo au mpaka utoe hela zote ulizowekeza kama mtaji wako?
Mkuu hata ukitaka kwenda kutoa zote ni ruksa. uamuzi ni wako. Ila itakuwa sawa na kupanda mbegu leo kisha kesho unaenda kuzifukua 😎
 
Nina swali nje ya mada kidogo

Hivi mfano nimewekeza mfuko wa UTT nina say miaka 25, nikawa nimeoa

Baada kama ya miaka 20 ndoa ikavunjika

Sasa kwenye zile sarakasi za mahakamani za kugawana mali kwenye talaka huwa zinagusa mpaka kwenye uwekezaji wako huko UTT??
 
1. Kwenye mfuko wa Bond, wanaposema kianzio cha Ths.50,000/= kwa lengo la kukuza mtaji maana yake ni nini? Utapata faida kwa hiyo elfu 50 yako au utaanza kupata faida na gawio baada ya kufikisha Mil.5+?

2. Huo mtaji unakuaje? Yaani una kuzwa na faida itakayozalishwa au inakua kwa wewe kuendelea kuweka kidogo kidogo? Maana hawajataja kiasi cha kuendelea kununua vipande kama mifuko mingine walivyotaja
View attachment 2853182View attachment 2853183

Mkuu, mtu akinunua vipande vya elfu 50 kwa mpango wa kukuza mtaji Bond fund, faida itakayopatikana, badala ya mwekezaji kupewa kama gawio, itatumika kukununulia vipande zaidi. Hivyo idadi ya vipande itaongezeka kwa jinsi hiyo na pia kwa mtu kuwekeza pesa zaidi.

Ongezeko la mtaji kwa mpango wa kukuza mtaji litatokea kwa:
a) vipande vinavyonunuliwa badala ya mtu kupewa gawio;
b) kuwekeza pesa nyingine kununua vipande zaidi;
c) Kukua taratibu kwa thamani ya kipande.
 
Nina swali nje ya mada kidogo

Hivi mfano nimewekeza mfuko wa UTT nina say miaka 25, nikawa nimeoa

Baada kama ya miaka 20 ndoa ikavunjika

Sasa kwenye zile sarakasi za mahakamani za kugawana mali kwenye talaka huwa zinagusa mpaka kwenye uwekezaji wako huko UTT?? k

Kwa mtazamo wangu sidhani kama ulijaza taarifa za kuwa mmiliki ni mmoja manake taasisi inakutambua ww (Jasho lako ) hawa wengine wanakuwa warithi tu mpaka pale utakoamuwa kuwapa au utakapoaga dunia,hivyo hata mkigombana mali ni zako tu ........KWA ufafanuzi zaidi wacheki UTT AMIS wenyewe kwa majibu Yakinifu
 
Nina swali nje ya mada kidogo

Hivi mfano nimewekeza mfuko wa UTT nina say miaka 25, nikawa nimeoa

Baada kama ya miaka 20 ndoa ikavunjika

Sasa kwenye zile sarakasi za mahakamani za kugawana mali kwenye talaka huwa zinagusa mpaka kwenye uwekezaji wako huko UTT??
Unagusa mali zote zinazojulikana, kwahiyo inategemea hapo

Nimewaza tu lakini
 
Labda kama mdau hpo juu alivyosema kuwa apart from hyo 1% ya kila mwezi kuna 14% ya mwaka, kama ni hvyo hpo angalau inamake sense.
mi nilivyoelewa ni kwamba 1% imezidishwa mara miezi 12 kupata 12% so hakuna riba nyingine tena tofauti na hiyo labda kama kuna ile compound interest alisema mchangiaji mmoja
 
Kwa vile thamani ya kipande (Net asset value per unit) hukokotolewa kila siku kwa kila mfuko wao, unaweza kukokotoa thamani ya uwekezaji wako kila utakapo.

Mimi kwa mfano huwa ninakokotoa thamani ya uwekezaji wangu mara 1 kila wiki. Unaweza kukokotoa hata kila siku.

Thamani za vipande siku kwa siku zinapatikana katika website ya utt, kwenye application ya utt ukiwa nayo, na mara nyingine huchapwa katika baadhi ya magazeti.
mnaposema vipande hasa hua mna maanisha nini? na je riba hua ina kokotolewa kwa kila kipande au kwa jumla ya vipande?
 
Back
Top Bottom