Je,ni mtandao gani wa wa kijamii wazawa huko Rwanda ambao tunaweza kuuita JF ya Rwanda

Je,ni mtandao gani wa wa kijamii wazawa huko Rwanda ambao tunaweza kuuita JF ya Rwanda

KISIWAGA

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2015
Posts
8,022
Reaction score
16,563
wakuu tumekuwa tukisikia sifa za wanyarwanda kuwa wako juu sana kwenye hizi issue za tech lakini cha kushangaza mbona hakuna mtandao hata mmoja wa kijamii uliotengenezwa na mnyarwanda ambao tunaweza kuulinganisha na hii JF ya Melo

afadhali wakenya wao wana kenyatàlk nk ambao kiuhalisia ni mkubwa kama JF ya Melo

wanyarwanda wamekwama wapi au ndio muda wa JF kujitanua huko kwa ndugu zake Genta
 
Angalien hii forum halafu mniambie Ina tofauti Gani Na JF?
Hii jamiiforums na mitandao mingine inatumia vbulletin nadhani ni programu unanunua na kuicustomize kwakuweka features zako ndio ndio maana inafanana. Usidhani ni rahisi kwamba unaweza kufanya bila knowledge maana utakuwa unarisk data za watumiaji wake
 
Historia ya wanyarwanda kisiasa na kijamii si sawa na watanzania au wakenya kidogo.

Mfumo wa utawala pia ,utawala wa mkono wa chuma wa pk si sawa na watawala wetu wakitanzania. Kule hakuna uhuru wa kutoa maoni wala kukosoa hasa kisiasa.kule rwanda hata majenerali wa jeshi hawako salama dhidi ya Pk.

Ukabila,chuki ya wahutu na watutsi haijakwisha bado ,amani ni ya kulazimisha hivyo kukiwa na uhuru kama tulionao hapa Jf mambo yatakuwa hadharani na amani kutoweka.
Mi naona ni haya machache,ndio sababu.
 
Haitatokea Sio East Africa tu,Africa nzima.Tuendelee kuomba huu Wa Kwetu Uendelee Kuishi.
 
Hii jamiiforums na mitandao mingine inatumia vbulletin nadhani ni programu unanunua na kuicustomize kwakuweka features zako ndio ndio maana inafanana. Usidhani ni rahisi kwamba unaweza kufanya bila knowledge maana utakuwa unarisk data za watumiaji wake
Sasa hapo hajatengeneza, amecustomize...
Kwani wale wanaocustomize magari Kwa kuyawekea mziki Na rims wanakuwa wameyatengeneza au kuyagundua?
 
Sasa hapo hajatengeneza, amecustomize...
Kwani wale wanaocustomize magari Kwa kuyawekea mziki Na rims wanakuwa wameyatengeneza au kuyagundua?
Mkuu, yote kwa yote ni mambo meng yameshaandaliwa, hata wanatengeneza softwares na systems unakuta kuna codes wanachukua huko open source ili kurahisisha mambo.
 
Back
Top Bottom