Je, ni nani huyu mwekezaji wa kutujengea reli kipande Cha Uvinza-Gitega?

Je, ni nani huyu mwekezaji wa kutujengea reli kipande Cha Uvinza-Gitega?

Mwande na Mndewa

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2021
Posts
1,117
Reaction score
3,153
Kwanza kabisa siungi mkono utaratibu wa kukatana kwa kusafirisha mzigo ni utaratibu mgumu sana.

Huu ni mkopo pia lakini usioeleweka kabisa, maana marejesho ni kukatana kwenye mizigo utafikiria biashara ya michele kule Mbeya.

Bora serikali ichukue mkopo kutoka kwake wawe na time frame ya kulipa kama mikopo mingineyo ya SGR, kisha huyo jamaa naye awe analipa gharama za usafirishaji kama wengine.

Kinyume na hapo kuna utapeli mkubwa sana unaenda kutokea kwenye eneo la usafirishaji mzigo, maana yeye anaenda kutumia miundombinu yote ya SGR kupitishia mizigo yake kwenye treni zetu.

Unaweza kukuta TRC inasafirisha mizigo, kila mizigo inasingiziwa yake. Je, hakuna harufu ya utapeli wa kimataifa?
Habari ya serikali kuchukua mkopo kienyeji kienyeji na kisha kukatana kwenye usafirishaji imetoka wapi?

Utaratibu wa wauza mazao wakileta mizigo kwa mafuso ndio serikali inataka kutumia kwenye SGR na treni zetu mpya ambazo zote ni za mkopo?

Awepo mwamba mmoja binafsi atatumia bure kwa kivuli cha kujenga kipande kidogo eti tunakata kidogo kidogo.
Kinachotakiwa serikali ichukue mkopo kokote kisha ijenge na marejesho yawe ya mikopo, siyo kukatana kwenye matumizi ya SGR na treni zote anakuwa anasafirisha mizigo kwa kukatana. Badala ya kukatana ni vizuri tulipe mkopo kwa utaratibu unaoeleweka rasmi.

ushauri wangu;

Utaratibu huu haufai, bora serikali ichukue mkopo kwake kisha iwe inamlipa yeye na yeye akitumia reli alipe kama wengineo. Kinyume na hapo kuna utapeli mkubwa sana unaenda kutokea.
 
Hizo model za public private partnership (PPP) kwenye Ujenzi wa miradi ndiyo best way ya kupiga hatua kwenye miundombinu. Hapa kuna models kama DBOT ( Design- Build-Operate- Transfer) na BOT (Build-Operate- Transfer)

Nchi za South East Asia zimetumia sana mtindo huu kujenga barabara hasa Makaysia. Mtu au Kampuni binafsi inajenga barabara, halafu inaruhusiwa kukusanya ushuru kwa muda fulani kisha baada ya gharama kurudi barabara inakuwa ya Serikali na watu wanapita Bure.

Ni kama NSSF wanavyokusanya Nyerere bridge pale Kigamboni.

Kinachotakiwa ni uwazi na kufuata Sheria ya PPP na PPRA katika kumpata mbia.
 
Mkuu umeniwahi ila naongezea tu kuwa mikataba iwe na uwazi na ushirikishwaji for the entire time maana wajinga hawakawii kuweka conditions zitakazo tubana tukaingia mkenge na wajinga wapo upande huu wetu
 
Mnatuletea mambo ya TRATAT ,TRAB mengine.
Aliyekwambia mbia hajapatikana nani?
nchi kila kitu vululuvululu tu,ukiona hilo limeongelewa ujue mbia yupo tu.
 
Nchi haiwezi endelea kwa serikali kujenga kila kitu..nchi zote zilizoendekea serikali zinakuwa ni wasimamizi tu..angalia zile barabara na flyovers karibu zote za Africa kusini zimejengwa kwa mtindo huo..unapita kwenye mkeka but after a certain distance Kuna road toll ya kulipia. Ucan imagine unatoka Dar hadi singida 8 lane road..min speed 100km hrs hakuna shimo Waka matuta.
Utaratibu wa serikali kufanya kila kitu ndo huu unasababisha tunakutakana na nahandaki barabarani due to poor maintainance..nafikiri Cha msingi ni uwazi na win win situation kwenye hiyo mikataba
 
Umeandika juu ya kitu gani mkuu, maana ni kama unatusimulia hadithi ambayo tulishaisikia toka utotoni, kumbe ndiyo mara ya kwanza kuisikia.

Ninavyoweza kukisia juu ya habari yako hii ni kwamba tayari serikali imeingia kwenye mpango wa PPP (Public Private Partnership); kama ndiyo hiyo unayoizungumzia, basi subiri kidogo, hiyo ni mvua ya rasharasha anayoigema Samia, mvua yenyewe ipo njiani inakuja.
 
Hizo model za public private partnership (PPP) kwenye Ujenzi wa miradi ndiyo best way ya kupiga hatua kwenye miundombinu. Hapa kuna models kama DBOT ( Design- Build-Operate- Transfer) na BOT (Build-Operate- Transfer)

Nchi za South East Asia zimetumia sana mtindo huu kujenga barabara hasa Makaysia. Mtu au Kampuni binafsi inajenga barabara, halafu inaruhusiwa kukusanya ushuru kwa muda fulani kisha baada ya gharama kurudi barabara inakuwa ya Serikali na watu wanapita Bure.

Ni kama NSSF wanavyokusanya Nyerere bridge pale Kigamboni.

Kinachotakiwa ni uwazi na kufuata Sheria ya PPP na PPRA katika kumpata mbia.
The problem is not the model, as we know that it is the way to go nowadays. problem ni hawa negotiators wetu, who are corrupt and incompetent. wengi wao additional 10% above everything else ndio name of the game. I am sure for 10% they will leave a loophole somewhere, and we will end up losers in every way or being sued for billions of dollars as a result
 
Negotiator wa nchi Mwiguluuuuu haaa haaaa haaaaa watanzania Mungu tu aingilie Kari

Umeona ehh!
Yaani ni kumlilia Mwenye Enzi Mungu mpaka atende walahi!
Atutoe kwenye janga la mafisadi sugu walahi [emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
 
Mshaanza siasa zenu ili kuchelewesha miradi ya kimkakati

Mlileta siasa kigamboni ikafeli kuendelezwa

Mlileta siasa bandari ya Bagamoyo ikafa kibudu huko Kenya wakaiga na sasa wamemzaliza kujenga Bandari ya Lamu

Mkaleta siasa tukaachana na miradi ya Gesi sasa tuna gesi ila kila siku kuna mgawo wa umeme kama mijitu isiyo na akili

Sasa mnaleta siasa serikali isitumie sekta binafsi kujenga reli ili tu reli ikwame

Hilo deni la taifa umeliona linavyokuwa? Unavyosisitiza tukope tukifikia kwenye ukomo wa kukopa utatoa hela wewe?

Jinga kabisa
 
Umeona ehh!
Yaani ni kumlilia Mwenye Enzi Mungu mpaka atende walahi!
Atutoe kwenye janga la mafisadi sugu walahi [emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
Huyu jamaa data zake hata akiwa bungeni utadhani yuko anapiga ramli.
 
Acha kuogopa mababdiliko mleta mada. Ukiyaogopa mabadiliko basi yatakubadilosha wewe.
 
Back
Top Bottom