Je ni Nani ni mtenda dhambi ? katika hawa vijana watatu

Je ni Nani ni mtenda dhambi ? katika hawa vijana watatu

MELEKAHE

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2023
Posts
1,340
Reaction score
5,588
-kijana wa kwanza Ameiba biblia kanisani kwa ajili ya kwenda kujisomea nyumbani

-Kijana wa pili Ameiba pesa nyumbani na kwenda kuitoa yote kanisani kwa njia ya Sadaka

-Kijana wa tatu Ameiba Sadaka kanisani na kwenda kuwapa maskini na yatima

Je ni nani mtenda dhambi ?
 
Mkuu, ukishasema ameiba, hakuna tena swali hapo.

Ni sawa na kusema mmoja amembaka mwanafunzi, mwingine kambaka mfanyakazi wake, na wa tatu kambaka mkewe!

Kubaka ni kubaka tu! Kadhalika, wizi ni wizi tu. Ndiyo maana kulinda kura ni haki na wajibu wa kila raia mzalendo!
 
🤣Inategemea na mubakwa ataichukuliaje kwa uzito
 
Yahweh hakusema tukwaze binadamu wenzetu kwa ajili ya kumfurahisha yeye.

Tunatakiwa tuwe wema kwa binadamu wenzetu, na tuwe wema kwake.

Hizo kanuni mbili zinapaswa zifuatwe kwa pamoja
 
ivi usiibe ni amri ya ngapi vile,,ila swali tata sana hilo
 
Wote wakipelekwa mahakamani wanashtakiwa kwa mujibu wa sheria 😜
 
Aliye iba sadaka kanisani na kwenda kuwapa yatima na maskini yupo sahihi , kafanya kile kanisani walipaswa kufanya ila kanisa wakaiba.
 
-kijana wa kwanza Ameiba biblia kanisani kwa ajili ya kwenda kujisomea nyumbani

-Kijana wa pili Ameiba pesa nyumbani na kwenda kuitoa yote kanisani kwa njia ya Sadaka

-Kijana wa tatu Ameiba Sadaka kanisani na kwenda kuwapa maskini na yatima

Je ni nani mtenda dhambi ?
Mimi niliiba hela ofisini kwa ajili ya kwenda kumtibu mtoto wangu sasa sijui na mimi ninadhambi?
 
Nani mtenda dhambi?
Aliyeiba...
Dhambi ni kufanya tendo ulilokatazwa usitende.
Katazo ni amri na amri ikitekelezwa inakuwa sheria.

Aliyeiba katenda kosa.
 
Back
Top Bottom