Venus Star
JF-Expert Member
- Dec 6, 2018
- 26,519
- 78,311
Tunavyozidi kuendelea na maisha ya kila siku, hatuwezi kuacha kufikirisha bongo zetu.
Ziara ya Paul Kagame imenifanya nifikirie sana. Kwanini iwe ziara ya ghafla hivyo? Katika mawazo yangu nimewaza mambo kadha wa kadha.
1. Tayari huko Congo ya mashariki vurugu inaendelea. Na sote tunajua yule anayeleta vurugu hizo ni ndugu yetu huyu na wenzake wakisaidiwa na wafanya biashara mbalimbali wa madini duniani. Huku USA akiwa behind the scene.
Juzi juzi makamu wa rais wa Marekani alikuja hapa Tanzania. Na katika mambo mengi yaliyozungumzwa huenda na hili suala la amani katika eneo la kaskazini mwa congo. Maana Tanzania inapokea wakimbizi wengi sana na kushindwa kufanya mipango yake ya maendeleo.
2. Tayari Burundi, Uganda na DRC zimekubali kufanya biashara na Tanzania. Huku yeye akiwa na matakwa yake. Na ukiangalia mbele ya safari madini ya huko Congo na Burundi yatasafirishwa kupitia SGR ya Tanzania. Sasa hapa tunaongelea National Interest. Ukiyagusa maslah ya Tanzania maana yake umeingilia ulinzi na usalama wa Tanzania.
3. Tunapoelekea anaona kabisa anatengwa, Maana USA sasa hivi naye anapigana for her survival. Hizi operation zinazoendelea huko Ukraine zimewafumbua wengi. Kwahiyo wengi sasa wanaanzisha umoja wao na kuanza kujiweka mbali na USA. Huku wengi wakiwa karibu na China. Yeye hana mahusiano mazuri na China huku TZ tukiwa washirika wa karibu sana na China.
4. Tanzania imechaguliwa kuwa mwenyekiti wa majeshi ya Ulinzi na Usalama Duniani. Mwakani mkutano wa majeshi yote duniani utafanyika hapa Tanzania. Tanzania imekabidhiwa na Russia juzi juzi wiki hii huko Moscow. Kuwa mbali na Tanzania ni kujitenga na ulinzi wa kidunia.
5. Tanzania imeandaa mpango kabambe wa kumaliza na kutokomeza makundi yanayopigana na serikali huko DRC. Mpango wa Tanzania utaweza kumfanya yeye apotee kabisa kwenye ramani, kama alivyopotea Idd Amini Dadaa.
Karibu tuchangie. Hayo ni mawazo yangi binafsi kama raia mwema.