Je, ni nini lengo la ziara ya Ghafla ya Paul Kagame hapa Tanzania 27-04-2023?

Je, ni nini lengo la ziara ya Ghafla ya Paul Kagame hapa Tanzania 27-04-2023?

Tunavyozidi kuendelea na maisha ya kila siku, hatuwezi kuacha kufikirisha bongo zetu.

Ziara ya Paul Kagame imenifanya nifikirie sana. Kwanini iwe ziara ya ghafla hivyo? Katika mawazo yangu nimewaza mambo kadha wa kadha.

1. Tayari huko Congo ya mashariki vurugu inaendelea. Na sote tunajua yule anayeleta vurugu hizo ni ndugu yetu huyu na wenzake wakisaidiwa na wafanya biashara mbalimbali wa madini duniani. Huku USA akiwa behind the scene.

Juzi juzi makamu wa rais wa Marekani alikuja hapa Tanzania. Na katika mambo mengi yaliyozungumzwa huenda na hili suala la amani katika eneo la kaskazini mwa congo. Maana Tanzania inapokea wakimbizi wengi sana na kushindwa kufanya mipango yake ya maendeleo.

2. Tayari Burundi, Uganda na DRC zimekubali kufanya biashara na Tanzania. Huku yeye akiwa na matakwa yake. Na ukiangalia mbele ya safari madini ya huko Congo na Burundi yatasafirishwa kupitia SGR ya Tanzania. Sasa hapa tunaongelea National Interest. Ukiyagusa maslah ya Tanzania maana yake umeingilia ulinzi na usalama wa Tanzania.

3. Tunapoelekea anaona kabisa anatengwa, Maana USA sasa hivi naye anapigana for her survival. Hizi operation zinazoendelea huko Ukraine zimewafumbua wengi. Kwahiyo wengi sasa wanaanzisha umoja wao na kuanza kujiweka mbali na USA. Huku wengi wakiwa karibu na China. Yeye hana mahusiano mazuri na China huku TZ tukiwa washirika wa karibu sana na China.

4. Tanzania imechaguliwa kuwa mwenyekiti wa majeshi ya Ulinzi na Usalama Duniani. Mwakani mkutano wa majeshi yote duniani utafanyika hapa Tanzania. Tanzania imekabidhiwa na Russia juzi juzi wiki hii huko Moscow. Kuwa mbali na Tanzania ni kujitenga na ulinzi wa kidunia.

5. Tanzania imeandaa mpango kabambe wa kumaliza na kutokomeza makundi yanayopigana na serikali huko DRC. Mpango wa Tanzania utaweza kumfanya yeye apotee kabisa kwenye ramani, kama alivyopotea Idd Amini Dadaa.

Karibu tuchangie. Hayo ni mawazo yangi binafsi kama raia mwema.
KUNA MENGI UMEONGEA POINTI ILA MACHACHE UMEWEKA USHABIKI WA KISIASA.HAKUNA NCHI DUNIANI ISIYOPENDA USHARIKA NA MAREKANI SABABU KIJESHI KUNA FAIDA YAKE NA MAREKANI ITABAKI SUPER POWER SIKU ZOTE WATU WAPENDE WASIPENDE UKWELI NDIO HUO NA YANAYOTOKEA UKRAINE YALIWAHI KUTOKEA AFGHANISTAN CHINI YA USSR HAKUNA JIPYA MKUU.NI KWELI CHINA NA URUSI ZINAJITAHIDI KUTAFUTA WASHIRIKA ILA KINACHOWAANGUSHA NI UCHUMI WAO USIOTABIRIKA NA SOCIAL INTEGRATION NA MIGRATION POLICY ZA NCHI ZAO.....KUHUSU KAGAME NI KWAMBA ANAMSHAWISHI MAMA SAMIA ASIKUBALI USHAWISHI WA MUSEVENI ILI MABAKI YA (FAR) WAWEKE KAMBI ZAO TANZANIA NA UGANDA HAKUNA JIPYA MKUU.
 
KUNA MENGI UMEONGEA POINTI ILA MACHACHE UMEWEKA USHABIKI WA KISIASA.HAKUNA NCHI DUNIANI ISIYOPENDA USHARIKA NA MAREKANI SABABU KIJESHI KUNA FAIDA YAKE NA MAREKANI ITABAKI SUPER POWER SIKU ZOTE WATU WAPENDE WASIPENDE UKWELI NDIO HUO YANAYOTOKEA UKRAINE YALIWAHI KUTOKEA AFGHANISTAN CHINI YA USSR HAKUNA JIPYA.CHINA NA URUSI ZINAJITAHIDI KUTAFUTA WASHIRIKA ILA KINACHOWAANGUSHA UCHUMI WAO NA SOCIAL INTEGRATION NA MIGRATION POLICY ZAO.....KUHUSU KAGAME NI KWAMBA ANAMSHAWISHI MAMA SAMIA ASIKUBALI USHAWISHI WA MUSRVENI ILI MABAKI YA (FAR) WAWEKE KAMBI ZAO TANZANIA NA UGANDA HAKUNA JIPYA MKUU.
Nikiona mtu anaandika maandishi kwa herufi kubwa automatic mtu huyo dish limeyumba
 
MKUU NILIDHANI WEWE MCHAMBUZI MKONGWE WA SIASA ZA DUNIA KAMA SISI WADAU.......KUMBE BADALA YA KUSOMA MAONI UNATUKANA......BASI HAINA HAJA YA MIMI KUCHANGIA ULICHOANDIKA
Ukipewa ushauri acha kushupaza shingo. Kuandika maandishi yote kwa herufi kubwa ni ushamba na unaonekana kama mtoto wa shule ya msingi.
 
KUNA MENGI UMEONGEA POINTI ILA MACHACHE UMEWEKA USHABIKI WA KISIASA.HAKUNA NCHI DUNIANI ISIYOPENDA USHARIKA NA MAREKANI SABABU KIJESHI KUNA FAIDA YAKE NA MAREKANI ITABAKI SUPER POWER SIKU ZOTE WATU WAPENDE WASIPENDE UKWELI NDIO HUO NA YANAYOTOKEA UKRAINE YALIWAHI KUTOKEA AFGHANISTAN CHINI YA USSR HAKUNA JIPYA MKUU.NI KWELI CHINA NA URUSI ZINAJITAHIDI KUTAFUTA WASHIRIKA ILA KINACHOWAANGUSHA NI UCHUMI WAO USIOTABIRIKA NA SOCIAL INTEGRATION NA MIGRATION POLICY ZA NCHI ZAO.....KUHUSU KAGAME NI KWAMBA ANAMSHAWISHI MAMA SAMIA ASIKUBALI USHAWISHI WA MUSRVENI ILI MABAKI YA (FAR) WAWEKE KAMBI ZAO TANZANIA NA UGANDA HAKUNA JIPYA MKUU.
Mkuu Hao FAR ni nani?
 
Ukipewa ushauri acha kushupaza shingo. Kuandika maandishi yote kwa herufi kubwa ni ushamba na unaonekana kama mtoto wa shule ya msingi.
MKUU UMESOMA NILICHOANDIKA AU WEWE SIO MCHAMBUZI WA SIASA ZA DUNIA BALI NI MSHABIKI WA SIASA ZA DUNIA???????SOMA KILICHOANDIKWA KWANZA AFU NDIO UTOE MAONI AU KEJELI HAKUNA SHIDA KATIKA HILO.
 
MKUU UMESOMA NILICHOANDIKA AU WEWE SIO MCHAMBUZI WA SIASA ZA DUNIA BALI NI MSHABIKI WA SIASA ZA DUNIA???????SOMA KILICHOANDIKWA KWANZA AFU NDIO UTOE MAONI AU KEJELI HAKUNA SHIDA KATIKA HILO.
Mzee andika kwa herufi za kawaida. Ukiandika kwa herufi kubwa hata content uliyoiweka inakuwa haina maana.
 
Back
Top Bottom