Je ni sahihi kondakta wa daladala kupiga kelele za kuita abiria? Au abiria hawajui wanakokwenda? Je abiria wanakuwa hawaoni usafiri? (vipofu)

Je ni sahihi kondakta wa daladala kupiga kelele za kuita abiria? Au abiria hawajui wanakokwenda? Je abiria wanakuwa hawaoni usafiri? (vipofu)

Mr Why

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2019
Posts
2,235
Reaction score
4,252
Je ni sahihi kondakta wa daladala kupiga kelele za kuita abiria? Au abiria hawajui wanakokwenda? Je abiria wanakuwa hawaoni usafiri?

Hii tabia ya kondata kuita abiria na kutangaza vituo daladala zinakoelekea inanipa maswali mengi sana

Huwa napata maswali makubwa matatu?

1: Abiria hawafahamu wanakokwenda mpaka watangaziwe?
Kama hawafahamu wanakokwenda walifuata nini vituoni

2: Je abiria ni vipofu?
Kama abiria ni vipofu walifikaje vituoni
Mbona daladala zimechorwa alama pembeni na kuandikwa majina ya vituo zinakoelekea kuna haja gani ya kupiga kelele

3: Kwanini kondakta atangaze huku gari lake limechorwa alama na kuandikwa majina ya vituo?
Ama ni tabia ya kondata kusumbua abiria!
 
Hizi akili zako wanazo pia baadhi ya makonda wanadhani kila abiria ni mwenyeji wa hiyo route hivyo anakuwa hataji vituo.

Sio kila abiria ni mwenyeji wa anakoenda,halafu sio vituo vyote vimeandikwa kwenye gari.Pia sio kila safari unapanga kutokea nyumbani.
 
Mbona dart vituo vina majina! Ukifika gerezani utaambiwa kabisa

Abiria wa kimara garii linaondoka sasa!

Nadhani sio vibaya kutangaza maake hatujafikia level ya gari kuja kupakia na kuondk......
 
Je ni sahihi kondakta wa daladala kupiga kelele za kuita abiria? Au abiria hawajui wanakokwenda? Je abiria wanakuwa hawaoni usafiri?

Hii tabia ya kondata kuita abiria na kutangaza vituo daladala zinakoelekea inanipa maswali mengi sana

Huwa napata maswali makubwa matatu?

1: Abiria hawafahamu wanakokwenda mpaka watangaziwe?
Kama hawafahamu wanakokwenda walifuata nini vituoni

2: Je abiria ni vipofu?
Kama abiria ni vipofu walifikaje vituoni
Mbona daladala zimechorwa alama pembeni na kuandikwa majina ya vituo zinakoelekea kuna haja gani ya kupiga kelele

3: Kwanini kondakta atangaze huku gari lake limechorwa alama na kuandikwa majina ya vituo?
Ama ni tabia ya kondata kusumbua abiria!
Je machinga nao ni sahihi kupiga makelele tunau,a blabla kwani wateja hawaoni
 
Mwafrika bado hajafikia level ya kuwa binadamu kamili.

Kwa nchi za wazungu hakuna utakacho ambiwa. Ni wewe unatakiwa kujua usafiri huu unakwenda wapi na unatakiwa ushuke sehemu gani.

Hakuna waku muuliza.
 
Kuna tofauti Gani kati ya kondakta na mwanasiasa huku kwetu bongo!?,wote tunajua tunamtaka nani ila wanakuja kutudanganyadanganya kama ilivo ada kwa msimu wa uchaguzi

NB:Kuna mkoa waliwahi subiria barabara ya lami miaka 20 ,na Kila baada ya miaka mitano ndio sound hiyohiyo , mpaka waamerika ndio wakajenga barabara, Sasa Hawa wanasiasa sio sawa na makondakta wa stand ya basi hawa
 
Back
Top Bottom