Je ni sahihi kondakta wa daladala kupiga kelele za kuita abiria? Au abiria hawajui wanakokwenda? Je abiria wanakuwa hawaoni usafiri? (vipofu)

Je ni sahihi kondakta wa daladala kupiga kelele za kuita abiria? Au abiria hawajui wanakokwenda? Je abiria wanakuwa hawaoni usafiri? (vipofu)

Je ni sahihi kondakta wa daladala kupiga kelele za kuita abiria? Au abiria hawajui wanakokwenda? Je abiria wanakuwa hawaoni usafiri?

Hii tabia ya kondata kuita abiria na kutangaza vituo daladala zinakoelekea inanipa maswali mengi sana

Huwa napata maswali makubwa matatu?

1: Abiria hawafahamu wanakokwenda mpaka watangaziwe?
Kama hawafahamu wanakokwenda walifuata nini vituoni

2: Je abiria ni vipofu?
Kama abiria ni vipofu walifikaje vituoni
Mbona daladala zimechorwa alama pembeni na kuandikwa majina ya vituo zinakoelekea kuna haja gani ya kupiga kelele

3: Kwanini kondakta atangaze huku gari lake limechorwa alama na kuandikwa majina ya vituo?
Ama ni tabia ya kondata kusumbua abiria!
Atalipwaje bila kufanya kazi,atakuwa na kazi gani kwenye gari.Interview ya konda ni uwezo wa kuita abiria😀😀😀🔥
 
Yaani hayo maswali ndo umekosa ufumbuzi mpaka umeleta mada jf walau upate mwanga, yaani huelewi kabisa kwanini konda anataja vituo gari itakakopita??

Jombaa una safari ndefu sana.
 
Heri hata konda, kuna wale sasa wameweka maspika kwenye vituo vya bajaji afu wanatangaza sehemu flaniiiii panda hapa nauli elf mbilii aaah kmmk wanakera mno
 
Je ni sahihi kondakta wa daladala kupiga kelele za kuita abiria? Au abiria hawajui wanakokwenda? Je abiria wanakuwa hawaoni usafiri?

Hii tabia ya kondata kuita abiria na kutangaza vituo daladala zinakoelekea inanipa maswali mengi sana

Huwa napata maswali makubwa matatu?

1: Abiria hawafahamu wanakokwenda mpaka watangaziwe?
Kama hawafahamu wanakokwenda walifuata nini vituoni

2: Je abiria ni vipofu?
Kama abiria ni vipofu walifikaje vituoni
Mbona daladala zimechorwa alama pembeni na kuandikwa majina ya vituo zinakoelekea kuna haja gani ya kupiga kelele

3: Kwanini kondakta atangaze huku gari lake limechorwa alama na kuandikwa majina ya vituo?
Ama ni tabia ya kondata kusumbua abiria!
Ukipata majibu, jiulize tena mbona NIDA wanataka cheti cha kuzaliwa, inamaana hadi umeenda pale hawaamini kama umezaliwa!?
 
Mwafrika bado hajafikia level ya kuwa binadamu kamili.

Kwa nchi za wazungu hakuna utakacho ambiwa. Ni wewe unatakiwa kujua usafiri huu unakwenda wapi na unatakiwa ushuke sehemu gani.

Hakuna waku muuliza.
Kwakweli hili ni tatizo, kuna mambo mengine hatukutakiwa kufanya kabisa
 
Bado kuna kundi Kubwa walikimbia umande, hawajui kusoma unaweza usiamini lakini ndio ukweli.
 
Nachukia konda ambaye hataji vituo ,mtu mgeni unaweza vukishwa
Yamenikuta jana tu nimepanda gar nimemkuta jamaa mlangoni kashika pesa na vikaratasi nime mwambia nishushe stereo mi sio mwenyeji natoka buza hapo akasema tunapita hapo akuna shida kumbe sio konda mbele kashuka kaachiwa sjui 200 yake kasepa konda ajui gar mpaka kariakoo kumfata na kuta sura nyngne kumwambia akasema jamaa akumpa maagizo nilikereka kinoma
Lengo nishuke hapo nifanye mchakkato tena nifke sokota mataa nika elekezwa nipande gar inayofika usalama konda nikampqnga fresh ruti imeanza tumefka maeneo flani naon kituo cha polis mbele kuna kituo cha daladal gar ikasimam hapo nikamuuliza konda usalam bado akasema ndio hapa du nilishakusahau wangu aisee chupu chupu nipitilizwe tena alaf awataji vituo.
 
Katika mazingira ya usafiri wa umma, kama daladala, kuna masuala kadhaa yanayohusiana na utamaduni wa kupiga kelele ili kuwajulisha abiria. Hapa kuna baadhi ya mawazo:

1. Kondakta Kupiga Kelele: Kondakta anapiga kelele ili kuwajulisha abiria kuhusu maeneo ya kusimama, kuhamasisha watu wapande, na kusaidia katika kutoa huduma bora. Hii ni njia moja ya kuhakikisha kwamba abiria wanapata taarifa muhimu.

2. Taarifa kwa Abiria: Ingawa baadhi ya abiria wanaweza kujua wanakokwenda, wengine, kama vile wale wenye uoni hafifu au vipofu, wanaweza kutegemea sauti na maelezo kutoka kwa kondakta ili kuelewa mazingira yao. Hivyo, kupiga kelele kunaweza kusaidia abiria hawa kujua ni wapi wanapaswa kushuka.

3. Uelewa wa Abiria: Si abiria wote wanakuwa na maarifa ya kutosha kuhusu njia au maeneo wanayokusudia kutembelea. Hivyo, taarifa za sauti zinakuwa muhimu sana kwao.

Kwa hiyo, kupiga kelele kuna umuhimu wake katika kusaidia abiria kuelewa na kufikia maeneo yao, lakini pia kuna haja ya kujenga mifumo bora zaidi ya mawasiliano ambayo itawasaidia hata wale wenye ulemavu wa kuona.
 
Back
Top Bottom