gango2
JF-Expert Member
- Aug 31, 2011
- 1,958
- 2,293
Hivi karibuni nimesikia mkuu wa mkoa fulani akipiga marufuku umoja wa makabila yoyote yaliyopo mkoani kwake na kuhimiza kuundwa kwa umoja wa makabila yaliopo mkoani kwake! Hoja zilizotolewa ni kuwa ni chanzo cha ukabila! Nimefikiria mara kadhaa na kuja kuona hakuna sababu ya kufika au kuchukua hatua kama hizi kwa hapa tulipofika
Kwanza kabisa lazima tujue nini huwa ya chanzo au madhumuni ya kuanzishwa umoja hizi! Binafsi naona karibu 90% ya vyama hivi huwa ni kwaajili ya kusaidiana katika shida na pia kuwa pamoja katika mambo mbalimbali. Tumeona umuhimu wa vyama hivyi mikoani ambapo mmoja wao akipata matatizo basi wengine wamekuwa msaada mkubwa kwa wenzao
Pia umoja au vyama hivi vimekuwa moja ya nguzo za kuendeleza tamaduni na mila za makabila husika. Tumeona mara nyingi vyama hivi vimekuwa vinajaribu kuendeleza mila na tamaduni zao kwa namna moja au nyingine! wengi tumeona ikitokea misiba au matatizo wamekuwa wakwanza kuhakikisha mila zao zinalindwa
Mwisho nimeona mkuu huyu wa mkoa amefika mbali kwa kusema vianzishwe vyama vya makabili yaliyoko mkoani kwake! haoni kwamba hii ni hatari sana kuliko hii ya sasa! ni yale yale huwezi wazuia watu au ukawalazimisha waingie kwenye umoja wa watu wa kabila lingine!