Kimsingi tuanze kuhoji uvaaji wenyewe kabla hatujafika huko kwenye kukataza cha kuvaa. Kwa binti ambaye umekulia na kulelewa katika maadili yenye staha na kujiheshimu huwezi kutana na matatizo ya kurumbana na mpenzi wako.
Kwann uvae mavazi ya kushawishi na ukijua wazi yatavutia na kuwapa mfadhaiko wanaume ambao wanatakufuata na kukutaka kimapenzi kisha uanze sema unasumbuliwa.....
Sijawahi kuona mwanamke mwenye uvaaji wa heshima akisumbuliwa ila hawa wavaaji viwalo vya kisasa mnavyoita ni fasheni....
Kuna mavazi na fasheni inatakuwa ujue tu kuwa zitakupita bila wewe kupita nazo..... Hii ni kwa wale wanaojua kuwa mbeleni wanafuture ya kuishi hivyo hawatafanya upuuzi leo utakaowaletea shida mbeleni.
Kwahiyo mwenzako kukukataza mavazi ya aina fulani na kukutaka ufute baadhi ya picha katika mtandao ni mojawapo ya namna ya kukwambia anataka ujieshimu usimharibie amani yake ya moyo...... Mbona tukizeeka hatuvai tena nguo za kuachia maungo ili makunjanzi na matumbo yetu ya uzazu yaonekane....!!
Ni busara na hekima tu humuweka mwanamke katika uhalisia wake....
Yangu ni hayo tu
Sent using
Jamii Forums mobile app