Pre GE2025 Je, ni sahihi kuruhusu wajinga wengi kuchagua viongozi au wachache wenye akili kufanya hivyo?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kule Marekani wachache wanaitwa "SUPER DELEGATES", hao wana nguvu kuliko kura milioni!

Hatuhitaji mabonanza ya uchaguzi, tunapoteza mahela mengi sana na muda kwenda kuchagua watu tusiowajua vizuri.

Mimi kwenye uchaguzi wa 2020 nililetewa orodha ya wagombea ubunge zaidi ya 10, madiwani zaidi ya 20. Nitawajulia wapi wote hao zaidi ya kuweka tiki kishabiki tu, kivyama tu?. Tena kuna wengine kwa sababu hawawajui wagombea vizuri wanaangalia nani ana sura nzuri kwenye karatasi ya kura!.

Tunahitaji chombo cha kutupa viongozi bora, Hii kazi haiwezi kufanywa na raia wengi wasio na uelewa mpana wa mambo. Tutaishia kuweka watu madarakani kwa sababu wanajua kuchonga tu majukwwani lakini hawana track record yeyote ya maana ya kuonnyesha kuwa wanauweza uongozi.
 
Ipi ni njia bora ya kupata waliobora ?

Je, ni kuruhusu wajinga wengi wasiojua chochote kuhusu masuala ya siasa na maendeleo kuchagua viongozi?

Au watu wachache/ kijikundi kidogo kijuacho kuhusu siasa na maendeleo kuchagulia watu uongozi makini wa nchi?

Demokrasia ya wengi wape hata kama ni kundi la wajinga na wapumbavu limeamua ina afya kwa taifa au upuuzi ?

Kwa kutumia mtazamo wa kidunia sio kitaifa pekee.
Labda utueleze kigezo sahihi cha 'wajinga' tuweze kutoa maoni
 
Bila shaka unaongea kuhusu wapiga kura. Basi hilo wazo lako ni dhana potofu sana (fallacy).

Kwanza ni kina nani hao nchini wenye mamlaka ya kujua na kuamua wananchi wepi wenye akili na wepi ni wajinga wasiruhusiwe kushiriki kuchagua viongozi?

Vigezo vya kuamua wajinga na wenye akili vinaainishwaje na ni kina nani nchini wenye ujuzi usiohojika wa kuweka vigezo hivyo?

Tukijibu hayo maswali kwa utimilifu bila shaka tutajua uwezekano wa kuwa na “kikundi cha weledi wachache” kuchagua viongozi badala ya “wajinga wengi” kuhusishwa.

Aidha, tujifunze kwenye historia ya Ugiriki na Marekani (USA) jinsi walivyosumbuka kupata mfumo wa utawala sahihi kuwakilisha maslahi ya wananchi wote. Vile vile tupitie harakati za kina Lenin walioamini katika wachache wenye “mwanga” (the vanguard) kuongoza maslahi ya wengi.

Ndivyo itikadi kuu za demokrasia na ukomunisti zilivyozaliwa.

Pendekezo la “wenye akili wachache” kuchagua viongozi linawezekana tu kwenye mfumo wa kikomunisti wa chama kimoja cha siasa, in fact chama dola kinachohodhi mamlaka ya kuongoza nchi.

Haiwezekani, kwenye mfumo wa demokrasia ya vyama vingi kuwa na “vanguard party”. Labda kinafiki.

Swali la mtoa mada ni la msingi sana.

Democracy ni kuheshimu maamuzi ya wengi..... tatizo linakuja hao wengi "wanajua" maana ya wanachokiamua?

Leo hii UK inapata tabu kwa sababu ya kuwapa "wengi" uwezo wa kuamua kuwa wabaki au waondoke EU, na hao "wengi" sasa hivi wanajuta wakisema "walidanganywa".

Lakini pia, alternative yake ni nini? Hao wachache ambao "wanajua" mpaka wapewe uwezo wa kuamua mambo ya kila mtu mwingine, ni kweli "wanajua", how can we be sure?

Hakuna jibu jepesi hapa
 
Bila shaka unaongea kuhusu wapiga kura. Basi hilo wazo lako ni dhana potofu sana (fallacy).

Kwanza ni kina nani hao nchini wenye mamlaka ya kujua na kuamua wananchi wepi wenye akili na wepi ni wajinga wasiruhusiwe kushiriki kuchagua viongozi?

Vigezo vya kuamua wajinga na wenye akili vinaainishwaje na ni kina nani nchini wenye ujuzi usiohojika wa kuweka vigezo hivyo?

Tukijibu hayo maswali kwa utimilifu bila shaka tutajua uwezekano wa kuwa na “kikundi cha weledi wachache” kuchagua viongozi badala ya “wajinga wengi” kuhusishwa.

Aidha, tujifunze kwenye historia ya Ugiriki na Marekani (USA) jinsi walivyosumbuka kupata mfumo wa utawala sahihi kuwakilisha maslahi ya wananchi wote. Vile vile tupitie harakati za kina Lenin walioamini katika wachache wenye “mwanga” (the vanguard) kuongoza maslahi ya wengi.

Ndivyo itikadi kuu za demokrasia na ukomunisti zilivyozaliwa.

Pendekezo la “wenye akili wachache” kuchagua viongozi linawezekana tu kwenye mfumo wa kikomunisti wa chama kimoja cha siasa, in fact chama dola kinachohodhi mamlaka ya kuongoza nchi.

Haiwezekani, kwenye mfumo wa demokrasia ya vyama vingi kuwa na “vanguard party”. Labda kinafiki.
At least we should have a parliament system kama South Africa.... yaani rais achaguliwe na bunge sio wananchi. Imerahisisha hata kuwang'oa kina Zuma na Mbeki. Sema hapo ni kuhakikisha vigezo vya ubunge viwe sawasawa na alivyoainisha Warioba.

Yaani ni degree holder na majimbo yawe strictly 75 walau itasaidia kufanya informed decisions. Kingine wangekua prone to scrutiny na wapiga kura na wanaweza tolewa hata kabla ya uchaguzi so wasingeweza mess up!!

Such internal control mechanisms zingewezesha super group kuwepo in tandem with parliamentary democracy!!
 
Ni jambo nzuri endapo sheria itapita kwamba mpiga kura na mpigiwa kura wote wawe na elimu kuanzia degree moja. Hapo utapata kundi maalum la wasomi ambao wanaweza kupembua uongo wa wanasiasa na wakafanya uamuzi sahihi kwenye sanduku la kura.
Kuwa na elimu ya darasani ni jambo moja na kuwa na akili ni jingine.
Changamoto kubwa ni kwamba wengi wasio na akili hawawezi kutofautisha.
Hata hivyo, inakuwa bora zaidi mtu akiwa na vyote viwili.
 
Ni jambo nzuri endapo sheria itapita kwamba mpiga kura na mpigiwa kura wote wawe na elimu kuanzia degree moja. Hapo utapata kundi maalum la wasomi ambao wanaweza kupembua uongo wa wanasiasa na wakafanya uamuzi sahihi kwenye sanduku la kura.
Hoja yako ina matatizo mengi.

1. Degree si elimu. Mtu anaweza kuwa na degree bila elimu, halafu mwingine akawa na elimu bila degree. Kuna vijana wengi wana graduate na degree hawajui hata kuandika barua, halafu kuna watu wengine wanajua mitishamba ya kutibu magonjwa mengi lakini hawana cheti.

2. Elimu ya kuelewa mambo ya uongozi wa nchi na maendeleo inaweza kutolewa kwa watu wengi wenye elimu isiyofika degree. Hivyo kulazimisha degree kwenye hili ni kulazimisha exclusivity isiyo na lazima.

3. Unaweza kuwa na watu wengi walio na elimu rasmi ambao hawana maadili, wakajiona wao ndio wanastahili kuendesha nchi, wakatuongoza vibaya. Uongozi wetu wa sasa ni mfano. Uongozi huu hauna uhaba wa degrees, tuna mpaka Ph.Ds. Lakini kwa kiasi kikubwa umekosa maadili. Kwa nini tunataka ku solve tatizo la maadili kwa kutumia degrees?

4. Nchi yetu watu wengi hawana degree si kwa sababu wao ni wajinga. Watu hawana degree kwa sababu hakuna nafasi nyingi za kusoma, kuna matatizo mengi ya kiuchumi. Kabla ya kufikiria kulazimisha watu kuwa na degree ili kuchagua viongozi, unatakiwa angalau kuwa na nafasi kubwa na sawa kwa watu wote kuipata hiyo degree.

5. Kuna watu wengi wana busara za asili kama za kujua historia, mazingira, mitishamba, tamaduni zetu, na mambo mengi ambayo hayapo katika elimu rasmi. Watu kama hawa kuwanyima nafasi ya kupiga kura ni kutojitambua wenyewe kama jamii.

6. Mwisho kabisa, sababu kubwa ya kifalsafa, jamii yoyote inayoshindwa kuwaelimisha watu wake wengi kiasi cha kujua kupiga kura, ikategemea wasomi wachache, mpaka hapo imejitengenezea matatizo makubwa ya utabaka na kura kukosa uwakilishi, matatizo haya yatakuwa na mabaya makubwa yatakayozidi mazuri ya uchaguzi wa wasomi.

Kwa maneno mengine, ni bora kuruhusu kila mtu mzima kupiga kura, na kuboresha elimu kwa watu wote, kuliko kulazimisha wapiga kura wawe na degree, halafu ukajikuta unatengeneza matatizo mengi sana ya kifalsafa, ya haki za msingi za watu, ya kidemokrasia, ya maendeleo endelevu, etc, kwa kufanya hivyo.
 
Ipi ni njia bora ya kupata waliobora ?

Je, ni kuruhusu wajinga wengi wasiojua chochote kuhusu masuala ya siasa na maendeleo kuchagua viongozi?

Au watu wachache/ kijikundi kidogo kijuacho kuhusu siasa na maendeleo kuchagulia watu uongozi makini wa nchi?

Demokrasia ya wengi wape hata kama ni kundi la wajinga na wapumbavu limeamua ina afya kwa taifa au upuuzi ?

Kwa kutumia mtazamo wa kidunia sio kitaifa pekee.
Sijui lengo la huu uzi wako, lakini hapa Tanzania viongozi huchaguliwa na kigenge kidogo kijiitacho system, halafu wajinga wengi ndio huwa wanapangishwa mistari kwenye igizo la kuchagua viongozi. Lakini kiuhalisia viongozi wanakuwa tayari wameshaguliwa na hicho kigenge kidogo kijiitacho system.
 
At least we should have a parliament system kama South Africa.... yaani rais achaguliwe na bunge sio wananchi. Imerahisisha hata kuwang'oa kina Zuma na Mbeki. Sema hapo ni kuhakikisha vigezo vya ubunge viwe sawasawa na alivyoainisha Warioba.

Yaani ni degree holder na majimbo yawe strictly 75 walau itasaidia kufanya informed decisions. Kingine wangekua prone to scrutiny na wapiga kura na wanaweza tolewa hata kabla ya uchaguzi so wasingeweza mess up!!

Such internal control mechanisms zingewezesha super group kuwepo in tandem with parliamentary democracy!!
Mkuu umeelezea jinsi Rais anavyopatikana ndani ya mfumo wa parliamentary democracy. Ninachojua ni kuwa wingi wa wabunge wa chama chake hasa ndio humpa uRais akiwa kama kiongozi wa chama kinachoshinda uchaguzi. Bunge halifanyi uchaguzi wa Rais. Still, bado, ni wananchi ndio wanaochagua kupitia uchaguzi wa bunge wakijua viongozi wa vyama wanaoweza kuwa Rais/Waziri Mkuu.

Lakini hicho unachoongea ni tofauti na anachomaanisha mleta mada - labda afafanue zaidi.

Yeye anataka watu maalum “wenye akili” kama kikundi hivi (nafikiri) ndio wawe na dhamana ya kuchagua viongozi. Sidhani kama anafikiria wabunge kama wote ni “watu wenye akili”. Pia sidhani pia kama anafikiria kuwa watu wenye digrii ndio wenye akili.

Hapa JF, kuna watu wasiokubali demokrasia wanaopenda kuleta mada za “deep state” kama ndio taasisi inayojua maslahi ya nchi. Kwamba haiwezi kuruhusu watu fulani kushika madaraka hata wakishinda kwa kura!

Ndio hoja za namna hii zinapoanzia. Kwamba wananchi hawawezi kuaminiwa kuchagua viongozi sahihi! Kwamba inahitajika kikundi cha wateule “kinachoelewa vizuri maslahi ya nchi” (the vanguard) ndicho kiwachagulie viongozi!

Democracy is messy but indispensable. Haina short-cut. Kama tunapitia presidential system au parliamentary system bado haiwezekani kukwepa wananchi wote kupiga kura ambazo, hatimaye, zitaamua nani awe Rais wa nchi.

Tunaweza kuchezea mfumo tunavyotaka, lakini ukweli utaturejesha kwenye uhalisia.
 
Sijui lengo la huu uzi wako, lakini hapa Tanzania viongozi huchaguliwa na kigenge kidogo kijiitacho system, halafu wajinga wengi ndio huwa wanapangishwa mistari kwenye igizo la kuchagua viongozi. Lakini kiuhalisia viongozi wanakuwa tayari wameshaguliwa na hicho kigenge kidogo kijiitacho system.
Ushuzi wanajamba "wasomi".

Lawama tunawapa "wajinga".
 
Hii mada ni muhimu sana.

Kama ambavyo si wote wanaingia bungeni, hivyohivyo inabidi iwe SI WOTE wanaochagua viongozi.

Hiyo kazi inabidi tuidelegate kwa watu wachache sana waaminifu, wenye hekima, wenye maadili mazuri, Watusaidie kupata viongozi. Nje ya hapo mambo ya uchaguzi ni ushabiki kama ulivyo ushabiki mwingine kama vile mpira.
Changamoto tulizonazo ni kubwa. Ili kuondoka ujinga lazima uende/upelekwe shule waalimu wakufundishe. Je, una kumbuka waalimu hawa hawa ndio chombo cha ccm kuibia kura? So issue sio kupambana na ujinga tu. Tuna maadui wengine: unafiki, ubinafsi tamaa, na hivi karibuni uchawa, nk.
 
Democracy vs Aristocracy

Moja wapo ya udhaifu wa mfumo wa demokrasia ni wajinga kupata nafasi za kuwa viongozi.
 
Ipi ni njia bora ya kupata waliobora ?

Je, ni kuruhusu wajinga wengi wasiojua chochote kuhusu masuala ya siasa na maendeleo kuchagua viongozi?

Au watu wachache/ kijikundi kidogo kijuacho kuhusu siasa na maendeleo kuchagulia watu uongozi makini wa nchi?

Demokrasia ya wengi wape hata kama ni kundi la wajinga na wapumbavu limeamua ina afya kwa taifa au upuuzi ?

Kwa kutumia mtazamo wa kidunia sio kitaifa pekee.
KATIBA MPYA + TUME HURU YA UCHAGUZI NDO VIONGOZI WA KWELI HUPATIKANA SIO UHUNI WA MACCM
 
Ipi ni njia bora ya kupata waliobora ?

Je, ni kuruhusu wajinga wengi wasiojua chochote kuhusu masuala ya siasa na maendeleo kuchagua viongozi?

Au watu wachache/ kijikundi kidogo kijuacho kuhusu siasa na maendeleo kuchagulia watu uongozi makini wa nchi?

Demokrasia ya wengi wape hata kama ni kundi la wajinga na wapumbavu limeamua ina afya kwa taifa au upuuzi ?

Kwa kutumia mtazamo wa kidunia sio kitaifa pekee.
Wajinga ndiyo waliwao.
 
Sijui lengo la huu uzi wako, lakini hapa Tanzania viongozi huchaguliwa na kigenge kidogo kijiitacho system, halafu wajinga wengi ndio huwa wanapangishwa mistari kwenye igizo la kuchagua viongozi. Lakini kiuhalisia viongozi wanakuwa tayari wameshaguliwa na hicho kigenge kidogo kijiitacho system.
Na mbaya zaidi hilo genge (system) limejaa wapumbavu walio jivika ngozi ya uzalendo uchwara.

Ndio maana kushiriki uchaguzi ndani ya taifa hili ni ishara ya upumbavu ulio katika ukomavu wa kipekee zaidi.
 
Huwezi kwepa kanuni inasema wajinga wengi ndio uweka viongozi wabovu madarakani
 
Ipi ni njia bora ya kupata waliobora ?

Je, ni kuruhusu wajinga wengi wasiojua chochote kuhusu masuala ya siasa na maendeleo kuchagua viongozi?

Au watu wachache/ kijikundi kidogo kijuacho kuhusu siasa na maendeleo kuchagulia watu uongozi makini wa nchi?

Demokrasia ya wengi wape hata kama ni kundi la wajinga na wapumbavu limeamua ina afya kwa taifa au upuuzi ?

Kwa kutumia mtazamo wa kidunia sio kitaifa pekee.
Yote ni ujinga maana wanao gombea ni wapumbavu ...tatizo linaanzia kwenye wagombea.
 
Kamwe usibeze nguvu ya wajinga walio wengi.

Unakumbuka darasa la saba walichomfanya Dr. Mwakyembe?

CCM mtaji wake ni wakulima, wavuvi, wafugaji na machinga.
 
Back
Top Bottom