Pre GE2025 Je, ni sahihi kuruhusu wajinga wengi kuchagua viongozi au wachache wenye akili kufanya hivyo?

Pre GE2025 Je, ni sahihi kuruhusu wajinga wengi kuchagua viongozi au wachache wenye akili kufanya hivyo?

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Kule Marekani wachache wanaitwa "SUPER DELEGATES", hao wana nguvu kuliko kura milioni!

Hatuhitaji mabonanza ya uchaguzi, tunapoteza mahela mengi sana na muda kwenda kuchagua watu tusiowajua vizuri.

Mimi kwenye uchaguzi wa 2020 nililetewa orodha ya wagombea ubunge zaidi ya 10, madiwani zaidi ya 20. Nitawajulia wapi wote hao zaidi ya kuweka tiki kishabiki tu, kivyama tu?. Tena kuna wengine kwa sababu hawawajui wagombea vizuri wanaangalia nani ana sura nzuri kwenye karatasi ya kura!.

Tunahitaji chombo cha kutupa viongozi bora, Hii kazi haiwezi kufanywa na raia wengi wasio na uelewa mpana wa mambo. Tutaishia kuweka watu madarakani kwa sababu wanajua kuchonga tu majukwwani lakini hawana track record yeyote ya maana ya kuonnyesha kuwa wanauweza uongozi.
Hata hapa CCM inao super degates kwenye chama chao kama ilivyo Republicans na Democrats huko Marekani.
 
At least we should have a parliament system kama South Africa.... yaani rais achaguliwe na bunge sio wananchi. Imerahisisha hata kuwang'oa kina Zuma na Mbeki. Sema hapo ni kuhakikisha vigezo vya ubunge viwe sawasawa na alivyoainisha Warioba.

Yaani ni degree holder na majimbo yawe strictly 75 walau itasaidia kufanya informed decisions. Kingine wangekua prone to scrutiny na wapiga kura na wanaweza tolewa hata kabla ya uchaguzi so wasingeweza mess up!!

Such internal control mechanisms zingewezesha super group kuwepo in tandem with parliamentary democracy!!
Mbeki na Zuma waling'olewa na chama chao cha ANC kama vile Ndugai alivyong'olewa na CCM uspika hapa bongo.
 
Democracy vs Aristocracy

Moja wapo ya udhaifu wa mfumo wa demokrasia ni wajinga kupata nafasi za kuwa viongozi.
Hata kwenye aristocracy wajinga huwa wanapata nafasi za uongozi, historia imejaa mifano tele ya wafalme na madikteta wajinga, majuha, wapumbavu na makatili sana.
 
Usiige marekani hapakwetu hatuna hatahao wachache wenye akili. Tumejaa wajinga mwanzo mwisho kaunabisha nitajie mwenyeakili mmoja
 
Back
Top Bottom