Je, ni sahihi kwa wamiliki wa Night Club kurusha picha au video za wateja wao kwenye Mitandao ya Kijamii?

Je, ni sahihi kwa wamiliki wa Night Club kurusha picha au video za wateja wao kwenye Mitandao ya Kijamii?

Dalton elijah

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
373
Reaction score
829
Kwa Miaka Ya Hivi Karibuni Kumeibuka Wimbi Kubwa La Wamiliki kuchapisha Picha Au Video Za Wateja Wao Katika Mitandao ya Kijamii Hali Ambayo Kwa Namna Moja Sio Nzuri Kwa Baadhi Ya Wateja.

Unaweza Kwenda Kwenye Baadhi ya Kumbi za Starehe Kipindi Ukipata Kinywaji Iadara Ya masoko Na Habari Wao hufanya Kazi Za Kurekodi Video Kwa Ajili ya Promotion .

Kwa Jicho La Marketing Strategy ni Nzuri Kwa Night Club hizo Kwani huongeza engagement Kwa Wateja Wao Na Kufikia Wateja Wengi Zaidi

Lakini Kwa uwanda Mwingine Huwa inashusha Heshima Na Hadhi hasa Pale unapojikuta Katika Mitandao ya Kijamii Bila ya Kuwa Na Idhini Mtaalam

Katika Hatua Nyingine Masters Of Ceremony Nao Wamekuwa Wakichapisha Picha Au Video Kipindi Cha Harusi Jambo Ambalo Sio Zuri Hasa Pale Ambapo Hakuna Ridhaa Kutoka Upande Wa Mteja

Watu Wengi Sana Wamekuwa Wakikuta Katika Mitandao ya Kijamii Jambo Ambalo Linatatiza Kuchanganya Katika Midhania Isiyo Sahihi

Kuna Mambo Ambayo Yanatakuwa Yafanyike Kuhakikisha kunakuwepo Na Usawa Katika ya Pande Mbili Ili kupunguza Migongano kati ya Wateja Na Wamiliki Wa Kumbi za Sherehe Au MC Katika Kazi Zao

Kisheria, wamiliki wa night club wanapaswa kuwa waangalifu wanapohusisha picha au video za wateja wao kwenye mitandao ya kijamii au kwenye matangazo bila idhini yao. Kwa ujumla, kuna kanuni kadhaa zinazopaswa kuzingatiwa:

1.Sheria za Faragha : Katika nchi nyingi, kuna sheria zinazolinda faragha ya watu binafsi. Kuchukua picha au video za mtu bila idhini yake inaweza kuzingatiwa kama uvunjaji wa faragha.

2. Idhini Wamiliki wa mali kama vile night club wanapaswa kupata idhini wazi kutoka kwa wateja kabla ya kuchapisha picha au video zao mtandaoni. Hii ni muhimu ili kuhakikisha kuwa wateja wanajua na kukubali kuwa picha zao zitashiriki Katika Machapisho ya Mitandao ya Kijamii

3. Matumizi ya Picha za Umma Katika hali fulani, kama vile matukio ya umma ambapo watu wanajulikana kuwa wanachukuliwa picha, sheria zinaweza kuwa tofauti. Hata hivyo, ni vyema kuzingatia maadili na kuheshimu haki za binafsi.

4.Mkataba wa Huduma Wakati wa kuingia katika night club, kunaweza kuwa na mkataba (kwa mfano, kupitia alama au matangazo) ambao unaweza kueleza jinsi picha na video zitakavyokuwa zikitumiwa. Ni muhimu wamiliki wajue ikiwa hilo linaweza kutumika kisheria.

Katika hali yoyote, ni bora kwa wamiliki wa night club kufuata taratibu za kisheria na maadili ili kulinda haki za wateja wao na kuepuka matatizo ya kisheria.

Soma Pia: Tahadhari kwa MC's wa maharusi bongo
 
Kwenye masherehe naunga mkono hoja!
Ila kwenye bata hapana tunajitakia - mtu na heshima zako unaendaje kitambaa cheupe?
Kuna mahala pa kwenda huko hata ukipigwa picha watu wanaogopa! Na pakistaarabu huwa wanafanyaga promotion wanamlipa mtu ama wakipiga picha unakuta zile za familia
 
Inaboa sana
Kuna night club moja hapa Dom pia Niliwahi kukutana na huo upuuzi Yaani nimekaa zangu nakunywa pombe na mchepuko wangu(mke wa mtu) nashangaa tunamulikwa na mwanga wa flash ya picha nilistuka sana na kumrukia yule mpiga picha ili nimng'oe meno ila yule dogo akajitetea kwamba amepewa kazi na wahusika ikabidi niombe kuonana na manager lakini naye akanijibu majibu ya kihuni tangu siku hiyo siendagi tena hapo Yaani ni upuuzi sana kupiga watu picha halafu wanaweka mitandaoni!
Imagine huyo afande jirani yangu angeona picha mitandaoni niko bar nakunywa pombe na mkewe ingekuwaje?!
 
Kwenye masherehe naunga mkono hoja!
Ila kwenye bata hapana tunajitakia - mtu na heshima zako unaendaje kitambaa cheupe?
Kuna mahala pa kwenda huko hata ukipigwa picha watu wanaogopa! Na pakistaarabu huwa wanafanyaga promotion wanamlipa mtu ama wakipiga picha unakuta zile za familia
Kitambaa cheupe Kuna nini Sasa, mbona mzabzab, Vishu Mtata na Half american ndio wahudhuriaji wapendwa😂🤣
 
We sema Kama ume pigwa Picha na mke wa mwarabu.
Kifuatacho ni 🔥 🔥 😂
FB_IMG_17392820349849510.jpg
 
Inategemea ulivyo mkuu,
Ila mara nyingi wanaomba ruhusa yenu kwanza, sasa bahati mbaya ukiwa unajiamini na ulevi unasema sawa tu bila kujali consequences...

Dunia imebadilika sana, kila mtu anafanya kaz ya habari, wanaita content.. hadi kwenye harusi unajikuta kwenye Social mediaza bongo unajadiliwa... Thats bad, very bad..

Wanaosifia huu utaratibu hawajui nguvu ya privacy....

Yote kwa yote kuomba ridhaa ni muhimu.
 
MCs wa maharusi naona ndio trend na wanamulika zaidi pale mtu anapofanya vitu vya kijinga hata sababu ni pombe.
 
Inategemea ulivyo mkuu,
Ila mara nyingi wanaomba ruhusa yenu kwanza, sasa bahati mbaya ukiwa unajiamini na ulevi unasema sawa tu bila kujali consequences...

Dunia imebadilika sana, kila mtu anafanya kaz ya habari, wanaita content.. hadi kwenye harusi unajikuta kwenye Social mediaza bongo unajadiliwa... Thats bad, very bad..

Wanaosifia huu utaratibu hawajui nguvu ya privacy....

Yote kwa yote kuomba ridhaa ni muhimu.
Nyasaka mbali, buhongwa nina nyumba Kali.

Ahh ndoa tamu wakuu
 
Utajiri nje nje, ukienda mahakamani mambo ni machache TU

*Umepigwa picha bila ridhaa

*Imekusababishia kushusha utu Wako

*Imekusababishia kuvuruga familia yako na jamii kwa ujumla

*Imekusababishia msongo wa mawazo

*Picha imefanyia biashara bila mkataba!!
Hivyo Naomba nilipwe fidia kiasi cha M10
😂😂😂
 
Back
Top Bottom